Mawazo amewavua magamba mabalozi wanne CCM kata ya Msalato, Dodoma

OMUSILANGA

JF-Expert Member
Jan 25, 2012
384
227
Ndiyo wakuu, heshima kwenu..

Katika kutimilika kwa usemi usemao "MJINGA AKIJITAMBUA ,MWELEVU UPO MATATANI " hali si nzuri upande wa ccm katika kampeini zinazo endelea nchi nzima za uchaguzi mdogo wa Madiwani kata 29.

Zikiwa zimebakia takribani siku 10, jana mabalozi wanne wa ccm wamehamia cdm katika kata ya Msalato, Dodoma chini ya Kamanda Mawazo Alophonce,diwani wa zamani kata ya Sombetini, Arusha. Miongoni mwao ni ndugu Tano Chigoje, balozi ccm wa mtaa wa Chisewo.

Kwa mujibu wa tathimini ya uhalisia ni kuwa lazima ccm wakinywee kikombe hiki. Naomba kuwasilisha.

SOURCE: MAWAZO MWENYEWE.
 
Uchaguzi huu kama CDM wakifanikiwa kuchukua udiwani kama kata 10- 14 basi 2015 kitaeleweka tu.
 
Kuna haja sana ya CDM kuweka mashambulizi ya kutosha Dodoma, Tanga, kule kusini na kwingineko ambako hawa jamaa wa thithimwewe wamewekeza sana!!!!
 
Wana CHADEMA tudumishe utulivu wakati wa kampeni, kupiga kura na kuzilinda pia. Magamba wanajua kupewa ridhaa na wananchi ni ngumu, kwa hiyo wanajitahidi kubuni njia mbadala ikiwemo kuiba kura.
 
Back
Top Bottom