Kanda2,
MKANDARA
IKITOKEA UNAUMWA MOYO NA NCHIMBI AKAJA NA CHETI FEKI CHA UDAKTARI AKATAKA AKUFANYIE OPARESHENI UTAKUBALI?
AKIJA KAMALA NA LESENI YA URUBANI AMBAYO NI FEKI AKASEMA ANATAKA KUPAKIA ABIRIA UTAKUBALI? KUWA NI KIONGOZI NI ACCOUNTABILITY TUMOENA BUNGE LA UINGEREZA WABUNGE WAKIJIUZULU KWA KUTUMIA POUNDS TANO-SAWA NA ELFU KUMI ZA TANZANIA.NAGU ANATUWAKILISHA MIKUTANO MINGAPI YA BIASHARA KAMA WAZIRI MWENYE PHD? KINA KOMBA WAMEKOSA UWAZIRI KWA VILE ELIMU YAO INAONEKANA NDOGO. HAWA WENYE PHD FEKI HAKUNA HATA MMOJA ASIYE WAZIRI.WAMEDANGANYA WAFUKUZWE KAMA NI JAMAA ZAO SORRY.WEWE UKO CANADA UNASHINDWA KUJUA NINI MAANA YA KUWAJIBIKA
Mkuu wangu Nchimbi hawezi kuwa daktari wa kufanya Operation ikiwa hakusoma na hana cheti cha kufanya kazi hiyo.. Sii kila daktari anafanya upasuaji hata kidogo wala rubani wa ndege ya abiria hawezi kuajiriwa pasipo kupitishwa na pia mwanachama wa marubani.. ila waziri anaweza kuwa waziri pasipo cheti wala digrii ya taaluma fulani (specific), hivyo digrii ya chuo fulani kinachotambulika sio kigezo cha uwaziri pamoja na kwamba binafsi ningependa iwe hivyo.
Tatizo langu ni kwa wale waliosoma shule za Open University kuwa nao wamegushi vyeti, hivi mlitaka waweseme kitu gani?..kusoma wamesoma kweli lakini sii vyuo vinavyotambulika kwa hiyo kosa ni lazima liwe tofauti. Mkuu hata mahakamani upande wa mashtaka wakikosea ku register shtaka, hakimu huwa hana sababu ya kubadilisha hukumu yake hata kama itaonekana kuna makosa yamefanyika, itakuwa hana budi ila kuwachia mshtakiwa.
Hilo la Nchimbi, lilitakiwa toka mwanzo mtu huyu asiajiriwe, kutokana na kutoridhishwa na hizo degree zake lakini mnapomshuku kitu ambacho mlikifahamu toka mwanzo machizi ni sisi wenyewe.
Kusoma sii kuhitimu..na ndilo kosa kubwa tunalofanya. Mkuu wangu sote tumeenda shule na wengine tumetoka watupuuuu, pamoja na kwamba nilikuwa mtu wa mwisho toka shule ya msingi. Lakini maadam nilifanya mtihani wa mwisho kwa elimu yangu yamadrasa kwa nini nisiandike nilisoma hadi darasa la saba?. Hata kama niliruka au kurushwa madarasa kulingana na taratibu ilikuwa jukumu lenu kufahamu kwa nini nimechukua muda mfupi hivyo kabla sijaajiriwa. Sasa nini sababu ya kuwa na interview ikiwa leo cheti ndicho kinatoa ajira badala ya elimu kuwa ni uwezo wa mtu huyo ktk kuimudu nafasi anayogombea.
Hivyo kipimo cha elimu ya mtu ni lazima kiambatane na maswali yanayohusu kazi husika, ikiwa wewe kabuntas utatoka kapa, kama kweli Nchimbi hakusoma ama hana elimu anayodai yapo maswali madogo sana yangemwengua toka ktk wagombea, wala asingethubutu kujitangaza. licha ya yote haya aliyemchagua ni JK, yeye anajua zaidi sifa alozitaka toka kwa kiongozi ngazi ya Nchimbi.. pengine jamaa mchawi mzuri wa tungule, wee unaweza kucheza uchi usiku wa manane makaburini!
Mkuu wangu ikiwa leo tunaweza kuwaengua wagombea Ukatibu kata kwa vigezo vya ajabu ajabu unategemea nini huko juu. Wa kulaumiwa ni Mkulu pamoja na washauri wake kina Lowassa na Rostam kwani hao ndio walikuwa waajiri.