Mawaziri watatu watajwa kashfa za ufisadi

Mawaziri watatu watajwa kashfa za ufisadi

Mengi ni jipu liloiva siku nyingi. Ashauriwe aendelee kulea wajukuu wake.
Umiliki wake vyombo vya habari imekuwa silaha ya kuchafua watu na kulipa visasi.
 
hakuna msafi hata mmoja kila mtu kwa wizi wake wooote kamata mengi lowasa na wote hatuangalii jina chama wala kabila haina haja ya kuwatenga hawa wezi kwa vyama wala vyeo kamata wote
Richmond ni ya Kikwete na Escrow unajua nani walichukua pesa, unafahamu waliouza mashirika na nyumba za Serikali wapo wapi?
 
Ukisoma post za wachangiaji wengine humu, kama MOSHI VIJIJINI, MULHAT, na MR GENTLEMAN..., utaweza kujua kwa nini CCM wanaweza kutawala miaka 200... Na ndio maana CCM haitaki kupeleka shule watu wa makabila fulani ili waendelee kuwa mandezi... Hata ukiangalia demografia ya uchaguzi..., kura na wizi mwingi umefanyika kwa makabila yaliyo nyuma kwa kila hali... Lakini tatizo kubwa hapa ni ELIMU ELIMU ELIMU,, lakini sio hii inayotolewa na CCM...
 
Gazet nipashe, heading mawazir 3 waingia kwenye kashifa,
Hiv unatarajia kabisa kwa akili ya nipashe inaweza kudika kizur juu ya hao iliyowataja?? Kwan jf members si inajulikana kuwa wana masilahi binafsi? Siku hizi naona mwananchi nao wameingia kwenye mkumbo huo,

Jana nlikuwa naangalia taarifa ya habar itv, wakati wanaliport bungeni habar ya kubenea kuongea dk2 nzima kwa kuwa anazungumzia escrow na zaidi kwa kuwa alikuwa anamtaja pr sos, ilipewa uzito, kimsingi hawa jamaa wa vyombo vya habar wanatumika kama dom,

Leo nasikiliza kipindi cha asb cha chenal10, olest na wenzie wametumia dk45 o more kuongelea swala la zanziba kwa upande mmoja bila kubalance story, napata taswira kuwa vyombo vyetu vya habar havina uhuru, ila vinaendeshwa kwa utashi wa mmiliki,

Niwape ushaur waandishi wa habar kabla hamjadai uhuru wa vyombo vya habari daini uhuru kwanza kwenye nyombo vyenu vya habar, ili muwe huru mtoke kwenye akili za kushikiwa, vinginevyo mtakuwa mnaupotosha uma...

Jipu pwaaaaaaaaaaaa
 
Mwakyembe, Lukuvi, Muhongo wahusishwa na kashfa za ufisadi.

Chanzo: NIPASHE


Labda huyo aliyelikana andiko lake kuhusu aina ya Muungao unaotakiwa hapa kwetu, lakini hao wengine wanaonekana wana manufaa kwa umma, tunaona what they deliver
 
Gazet nipashe, heading mawazir 3 waingia kwenye kashifa,
Hiv unatarajia kabisa kwa akili ya nipashe inaweza kudika kizur juu ya hao iliyowataja?? Kwan jf members si inajulikana kuwa wana masilahi binafsi? Siku hizi naona mwananchi nao wameingia kwenye mkumbo huo,

Jana nlikuwa naangalia taarifa ya habar itv, wakati wanaliport bungeni habar ya kubenea kuongea dk2 nzima kwa kuwa anazungumzia escrow na zaidi kwa kuwa alikuwa anamtaja pr sos, ilipewa uzito, kimsingi hawa jamaa wa vyombo vya habar wanatumika kama dom,

Leo nasikiliza kipindi cha asb cha chenal10, olest na wenzie wametumia dk45 o more kuongelea swala la zanziba kwa upande mmoja bila kubalance story, napata taswira kuwa vyombo vyetu vya habar havina uhuru, ila vinaendeshwa kwa utashi wa mmiliki,

Niwape ushaur waandishi wa habar kabla hamjadai uhuru wa vyombo vya habari daini uhuru kwanza kwenye nyombo vyenu vya habar, ili muwe huru mtoke kwenye akili za kushikiwa, vinginevyo mtakuwa mnaupotosha uma...

Jipu pwaaaaaaaaaaaa
Hujakatazwa kusikiliza redio Uhuru na kuangalia TBC ccm
 
Enyi ccm ni sawa na Magaratia aliyoyatuka mtume Paulo ezi zakuimalisha kanisa yalikuwa yakiambiwa jambo lamaana yanaingiza upuuzi kwenye mambo ya msingi , sasa ninyi ma ccm mtu kataja mafisadi waliotajwa na chanzo ni gazeti la nipashe, unakurupuka kumuigiza mzee wetu mengi Ujajiuliza mpaka Nipashe inahandika chanzo chake nikipi? ndoukataja majina ya watu au wengine mpo kwa kuzuia maoni yenye akili wapokee upuuzi wa ccm.
 
Mawaziri Watatu Watajwa kashfa za ufisadi mkubwa.
NA FREDY AZZAH
4th February 2016
B-pepe
Chapa

Rais Dk. John magufuli.
Mawarizi wa tatu wa Rais Dk. John magufuli, juzi walipata wakati mgumu Bungeni baada ya kuhusishwa na kashfa zilizotokea katika wiozara walizokuwa na wanazoendelea kuziongoza.

Mawaziri hao ni William Lukuvu wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; Profesa Sospeter Muhongo wa Nishati na Madini na Dk. Harrison Mwakyembe wa Katiba na Sheria.

Lukuvi alihusishwa na tuhuma za uporaji wa ardhi kwa kutumia nafasi yake wakati Profesa Muhongo akilipuliwa kuhusiana na sakata la Escrow ambalo lilimfanya ajiuzulu nafasi aliyo nayo sasa wakati wa serikali ya awamu ya nne chini ya Rais mstaafu Jakaya Kikwete.

Dk. Mwakyembe kwa upande wake, alihusishwa na kashfa ya ununuzi wa mabehewa mabovu kutoka India uliofanywa na Kampuni ya Reli Tanzania (TRL). Wakati wa ununuzi wa mabehewa hayo, Dk. Mwakyembe alikuwa Waziri wa Uchukuzi ambayo ndiyo yenye dhamana ya kusimamia reli.

Akichangia hotuba ya Waziri wa Fedha na Mipango, juu ya mwongozo wa kuandaa mpango wa bajeti ya serikali kwa mwaka 2016/17, Mbunge wa Viti Maalumu, Anatropia Theonist (Chadema), alisema Lukuvi anahusika katika uporaji wa viwanja vya wananchi.

Alisema katika sekta ya ardhi, kuna migogoro ya ardhi ambayo inarudisha maendeleo ya wananchi nyuma.
“Dar es Salaam sasa mnavunja nyumba za watu wa mabondeni, kutokana na zoezi hilo watu zaidi ya 99, 000 watakuwa hawana makazi.

“Mnavunja nyumba zao halafu viwanja hamuwapi, Lukuvi amehusika na uporaji wa viwanja wakati akiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam. Katika hali kama hii wananchi wataishi maisha gani?” alihoji.

Alisema baadhi ya mawaziri badala ya kufanya kazi, wanashindana kuoenakana kwenye vyombo vya habari.

Alisema kasi ya Serikali kuwaletea wananchi maendeleo ni ndogo, kwa kuwa katika kipindi cha miaka 15 Serikali imepunguza umasikini kwa asilimia 14 tu.

Kwa upande wake, Kubenea alisema licha ya Profesa Muhongo kujiuzulu kwa sababu ya kashfa ya akaunti ya Tegeta Escrow, anashangaa ni kwa nini amerudishwa bungeni akiwa waziri wa wizara ile ile.

Alisema mbali na Profesa Muhongo, mmoja wa mwenyekiti wa wa kamati ya Bunge lililopita aliyejiuzulu kwa sababu ya kashfa hiyo, sasa hivi ni Mwenyekiti wa Bunge.

Dk. Mwakyembe naye alikuwa na wakati mgumu baada ya baadhi ya wabunge wa upinzani kumtaka awajibishwe kwa kashfa ya mabehewa mabovu ambayo yalinunuliwa na serikali iliyopita.

Baadhi ya wabunge hao walionekana kumpania Dk. Mwakymbe tangu juzi ambapo kila wakichangia hoja ya mwongozo wa kuandaa mpango wa bajeti 2016/17, walikuwa wakimtaja kwa kuwa aliyekuwa mrithi wake, Samuel Sitta, alibaini ubovu wa mabehewa hayo.

Mbunge wa Viti Maalum, Jessica Kishoa (Chadema) ambaye ni mke wa aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila, alimtuhumu Dk Mwakyembe kuwa amehusika katika sakata la uingizaji wa mabehewa mambovu ambayo yameisababishia serikali hasara ya mabilioni.

Aisema taifa limeingia hasara ya sh. bilioni 238 kwa kununua mabehewa mabovu na aliyekuwa Waziri wa Uchukuzi kipindi hicho yuko bungeni na ameshindwa kuwasilisha ripoti ya sakata hilo.

“Kazi iliyopo ni kupanga mipango ambayo haitekelezeki mpaka leo. Tunahitaji ripoti ya mabehewa ipo wapi haipatikani na Dk. Mwakyembe yupo hapa hili nalo ni jipu,” alisema.

LUKUVI, MWAKYEMBE WAJITETEA
Kutokana na tuhuma hizo, mawaziri Lukuvi na Dk. Mwakyembe walikanusha kuhusika na kutaka wanaozisema wapeleke ushahidsi kama wanao.

Akijibu tuhuma hizo nje ya ukumbi wa Bunge, Lukuvi alisema hana kiwanja chochote alichopora na kusema hizo ni tuhuma za kupakaziwa.

Alisema mbunge huyo alilenga kuzungumzia viwanja vya Mabwepande ambavyo wakati vinatolewa hakuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam na hajawahi kufika huko hata siku moja.

“Kama anazungumzia kwa ujumla sina kiwanja hata kimoja nilichopora wakati nikiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam. Kama ana ushahidi aulete,” alisema.

Kwa upande wake, Dk. Mwakyembe alisema mbunge huyo amesema uongo na serikali haijawahi kutumia zaidi ya Sh. bilioni 60 kununua mabehewa na kwamba mbunge huyo amelidanganya bunge na kumtaka atoe vithibitisho juu ya jambo hilo na akifanya hivyo atajiuzulu.

Dk. Mwakyembe aliomba ufafanuzi kuhusu utaratibu kwa Mwenyekiti wa Kikao hicho, Mary Mwanjelwa, ambapo alisema ni vyema watu wakaacha kugeuza bunge kama kijiwe cha kubishana kwa mambo yasiyo ya msingi.

Kauli hiyo ya Dk. Mwakyembe ilizua sintofahamu kwani kabla Mwenyekiti wa bunge kutoa nafasi Kishoa kutoa uthibitisho, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema), alitumia kifungu cha 63 (4) akisema kwa mujibu wa kifungu hicho anayepaswa kutoa uthibitisho ni Dk. Mwakyembe ambaye anamtuhumu mbunge huyo.

Kufuatia kauli hiyo ya Mdee, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama, alilazimika kusimama na kusema ushahidi au uthibisho ambao Mdee amemtaka Dk. Mwakyembe atoe ameshaueleza na kusema serikali haijawahi kununua mabehewa ya zaidi ya Sh. bilioni 60.

Alisema aliyedanganya bunge ndiye anayetakiwa kuwasilisha uthibitisho kwa kuwa waziri ameshatoa ufafanuzi.

Dk. Mwanjelwa alimtaka Kishoa kumpelekea uthibitisho ndani ya siku tatu kuhusiana na tuhuma hizo.

Kadhalika, Dk. Harrison Mwakyembe alilazimika tena kutoa ufafanuzi wa ununuzi wa mabehewa 274 ya Kampuni ya Reli tanzania (TRL) baada ya Halima Mdee kudai kuwa ni mabovu.

Dk. Mwakyembe alisimama na kutoa ufafanuzi wa mabehewa hayo huku akisema yuko tayari hata kujiuzulu ubunge kama kashfa hiyo ni ya kweli.

Katika kikao cha sita cha Bunge ambacho kiliongozwa na Mwenyekiti wa Bunge, Najma Giga, Mdee alisema katika Mpango wa Maendeleo wa mwaka 2011/12-2015/16, serikali ilipanga kukarabati reli ya kati kilomita 2,700 lakini hadi sasa zimekarabatiwa kilomita 150 tu.

Mdee alisema Mabehewa ya Mwakyembe 274 ni feki kwa kuwa waliambiwa na Sitta na akaunda kamati ili kuchunguza.

Hata hivyo, Mdee alikatishwa baada ya Dk. Mwakyembe kuomba kuhusu utaatibu ambapo alisimamia ili amweleze Mbunge huyo kuwa bungeni hakuna ubabe na kwamba akimwambia Mdee ampelekee mabehewa ambayo hayafanyi kazi.

"Kwenye mikataba kuna kipengele kinaitwa ‘defect liability period' wewe ni msomi wa sheria unajua," alisema Mwakyembe ambaye pia alikatishwa na wabunge wa upinzani waliotaka kutoa taarifa.

Hata hivyo, Mdee aliposimama tena alimtaka Dk. Mwakyembe aseme kama amevunja kanuni gani ili aijibu lakini Dk. Mwakyembe alijibu kwa kuhoji kama wako kwenye kikao au vurugu kama Kariakoo.

"Halima sikiliza, kama ni ubabe kaufanye huko nje,” alisema Dk. Mwakyembe huku akisoma kanuni ya 63 (3) na (4).

Hata hivyo, Mwenyekiti wa bunge alisema bunge linaendeshwa kwa kanuni na sheria huku akiwataka watoa taarifa kufuata utaratibu.

Katika hatua nyingine, Mbunge wa Mwibara, Kangi Lugola (CCM), alisema serikali isiwe na kigugumizi kuhusu kutaja kujenga reli ya kati na michepuko yake katika kiwango cha 'standard gauge' katika mpango huo.

Alisema ni vyema kutaja ili reli ya kati isiishie tu kwenye ukarabati na kuishia kujenga reli kutoka Tanzania hadi Rwanda.

"Mkiacha kutaja sehemu mnayoenda kujenga reli kwa kisingizio hamuwezi kutaja kila kitu wakati maeneo mengine mmetaja. Kama mtakuja hapa bila mwelekeo wa reli ya kati nitakuwa mtu kwanza kusema rasimu ya mpango siikubali," alisema.

Alisema mpango huo ni mzuri isipokuwa unahitaji kutekelezeka na wakiuacha, wataacha mapendekezo ya wabunge hautaweza kutekelezeka na itabaki hadithi na porojo.

Imeandaliwa na Freddy Azzah na Augusta Njoji
CHANZO: NIPASHE
 
Kumbe taarifa yenyewe imeandaliwa na GAZETI LA UKAWA!
 
ImageUploadedByJamiiForums1454576820.618182.jpg
 
Back
Top Bottom