Mfano mwingine hata ukiangalia ile line of responsibility, yaani ni nani anawajibika kwa nani, utaona waziri yuko redundant. System ya accountability huwa ni pyramidal, na kuwa kila mtu mmoja anaye bosi mmoja, na bosi mmoja anatawala watu wengi immediately chini yake. Kwa mfano wizarani, mkuu wa idara anawajibika kwa mkurugenzi, na mkurugenzi ana wakuu kadhaa wa idara chini yake. Mkurugenzi anawajibika kwa katibu mkuu, na katibu mkuu anao wakurugenzi kadhaa chini yake. Lakini ati katibu mkuu anawajibika kwa waziri, na waziri huyo anaye katibu mkuu huyohuyo mmoja! Waziri anawajibika kwa waziri mkuu, ambapo waziri mkuu anao mawaziri kadhaa chini yake. Waziri Mkuu anawajibika kwa Rais, ambapo Rais ni Mkuu wa Dola, mwenye chini yake Waziri mkuu, Makamu wa Rais, na vyombo vingine vya Dola. Kwa mtazamo huu utaona kuwa waziri wa wizara ndiye pekee anayeongoza mtu mmoja tu (Katibu Mkuu), wakati viongozi wengine wanaongoza na kupokea ripoti za watu wengi chini yao. Sasa huyu anayeongoza mtu mmoja tu aondolewe, hana kazi! Kazi ya waziri ni kuwa mdomo wa katibu mkuu, kusoma hotuba na kuweka saini mikataba! Hahitajiki mtu huyu, anatumalizia gharama bure!