Mawaziri wana umuhimu wowote?

Kithuku

JF-Expert Member
Nov 19, 2006
1,395
207
Baada ya Kenya kuendesha shughuli za serikali kwa miezi 5 bila mawaziri (isipokuwa wale wachache walioteuliwa kabla ya muafaka) wala waziri mkuu, tumejifunza nini? Kuna umuhimu wowote wa kuwa na hawa watu wanaoitwa mawaziri? Wamepata hasara gani kutokana na kutokuwepo watu hao? Mojawapo ya faida waliyopata ni kuwa wamepata savings ya ile gharama ambayo wangetumia kuwahudumia mawaziri kwa miezi hiyo mitano! Je kuna faida zaidi? Nadhani yaliyotokea Kenya ni fursa nzuri ya kutafakari upya umuhimu wa hawa tunaowaita mawaziri. Wakuu mnasemaje?
 
Principal secretaries ndiyo muhimu zaidi maana ndiyo watendaji na wanaelewa mamob in detail zaidi ya ministers
 
Ukimnukuuu Jk Anasema Hakuna Chuo Kinachofundisha Mawaziri ...wanaweza Kuwepo Na Yeyote Anaweza Kuchaguliwa.......kama Political Figure...tuu...ki Utendaji..katibu Mkuu/wakurugenzi Ndio Vichwa..
 
Mimi nadhani hizi post za uwaziri zifutwe tu! Naamini Kenya wameokoa hela nyingi sana katika kipindi hiki ambacho hakuna mawaziri wa kula hela hizo! Waondolewe hao mawaziri, hayo maswali wanayojibu bungeni ni usanii tu, majibu yote wanaandikiwa na wataalamu wanaenda tu kuyasoma pale bungeni! Nenda kwenye kikao cha bunge Dodoma utaona mengi. Siku za vikao vya bajeti nk, makatibu wakuu wa wizara na maofisa wengine nao huhamia Dodoma, wanaketi sehemu maalumu pale ukumbini kusubiri kuletewa vimeseji kutoka kwa mawaziri vinavyotaka kufafanua mambo fulani, waziri akipelekewa ni kusoma tu! Sasa hawa wa kazi gani? Wafanye kazi yao ya ubunge, serikali iendeshwe na maafisa waajiriwa ambao ni rahisi kuwadhibiti bila kuogopa mambo ya "mshikamano" wa chama wala mtandao. Ninahojifunza mimi kutoka Kenya ni kuwa tunaweza kufuta hawa mawaziri wote na bado tukaendesha serikali vizuri sana, tena kwa gharama nafuu zaidi!
 
Mfano mwingine hata ukiangalia ile line of responsibility, yaani ni nani anawajibika kwa nani, utaona waziri yuko redundant. System ya accountability huwa ni pyramidal, na kuwa kila mtu mmoja anaye bosi mmoja, na bosi mmoja anatawala watu wengi immediately chini yake. Kwa mfano wizarani, mkuu wa idara anawajibika kwa mkurugenzi, na mkurugenzi ana wakuu kadhaa wa idara chini yake. Mkurugenzi anawajibika kwa katibu mkuu, na katibu mkuu anao wakurugenzi kadhaa chini yake. Lakini ati katibu mkuu anawajibika kwa waziri, na waziri huyo anaye katibu mkuu huyohuyo mmoja! Waziri anawajibika kwa waziri mkuu, ambapo waziri mkuu anao mawaziri kadhaa chini yake. Waziri Mkuu anawajibika kwa Rais, ambapo Rais ni Mkuu wa Dola, mwenye chini yake Waziri mkuu, Makamu wa Rais, na vyombo vingine vya Dola. Kwa mtazamo huu utaona kuwa waziri wa wizara ndiye pekee anayeongoza mtu mmoja tu (Katibu Mkuu), wakati viongozi wengine wanaongoza na kupokea ripoti za watu wengi chini yao. Sasa huyu anayeongoza mtu mmoja tu aondolewe, hana kazi! Kazi ya waziri ni kuwa mdomo wa katibu mkuu, kusoma hotuba na kuweka saini mikataba! Hahitajiki mtu huyu, anatumalizia gharama bure!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom