Mawaziri na Wabunge mizigo CHADEMA hadharani

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
17,506
15,997
Igwe wana JF.

Kutokana na mwenendo wa Bunge la bajeti mjini Dodoma imefanyika tathimini kutokana na hoja mbalimbali za wabunge na mawaziri kivuli kutoka CHADEMA.Tathimini hii hailengi kushinikiwa KUB Mbowe kuwaondoa,kubadilisha hususan mawaziri kivuli.Tunaanza na wafuatao kutokana na ripoti ilivyotolewa;

1.Mbowe,huyu ni KUB aliyekosa mvuto katika historia ya KUB kwenye bunge..madaifu yake ni pamoja na uwezo mdogo kuchambua na kutoa hoja mbadala ya uendeshaji serikali,hana taarifa muhimu za nchi hutegemea kuambiwa na kuongea.Ana uwezo mdogo wa kuchambua mambo ya nchi na ripoti japo huwa si mtu wa kushambulia haiba za mtu/mpinzani.Anahitaji msaada kutoka naibu KUB mwenye uwezo.

2.Tundu Lissu,Huyu ana uwezo mkubwa wa ubishi ambao usipokuwa makini anaweza kukuchota japo ni mpotoshaji mara nyingi.Hoja yake huwa ni moja tu,mkanganyo wa sheria bungeni ni mara chache huongelea hoja za maendeleo kama maji,umeme nk.Baada ya wizara ya sheria kupita hana hoja mbadala hata leo bunge likiahirishwa yeye poa tu.

3.Saed Kubenea,Huyu ame"prove failure" bungeni mapema sana.Kanuni za bunge zinambana kupotosha umma.Hana msaada tena.Siongezi neno.

4.John Mnyika,katika hali isiyo kawaida ubora wake hasa katika eneo la nishati,madini na maji kashindwa kuleta hoja kuntu akaleta hoja kujadili watu.Kaumbuka na unafiki wa kusafisha "richmond".na kuponda escrow...ikumbukwe Mnyika hadi leo anamiliki ushahidi wa Lowasa kulindwa na ikulu kuwa inamlinda Lowasa.Hajawahi kukanusha.

5.Wengine,Sugu,Susane,Lema uwezo wao ni mdogo sana katika kujenga hoja.Mfano;Lema hana lolote zaidi ya Lugumi,Suzan Lyimo kwenye mambo ya elimu anazungumzia uchaguzi UDOM,Uchaguzi mkuu 2015 kayapa uzito kuliko elimu,bure kabisa,Sugu yeye anaomba semina zirudi sababu anataka kufungua hoteli,bure kabisa.

Nachukuwa nafasi hii kumpongeza Esther Matiku,Waziri kivuli Muungano,Peneza,Waitara,Heche nk kwa kusimamia hoja kwenye maeneo yao.Wabunge hawa wameomba miradi mingi ya maendeleo kama maji,elimu nk bila kuongelea watu.

Pongezi kubwa kwa ZZK,umekuwa "all around MP" umechangia kwa hoja kila wizara ni funzo kuu kwa upinzani.Umetoa hoja bila kujadili mtu.Wengi tumejifunza.

Naomba michango yenye tija kuboresha siasa za upinzani hapa tanzania.

Nawasilisha
 
Kweli aisee umemsahau yule wa chalinze
 
Matathmini mtumbua majipu, inasemekana katumbua nyama na si majipu ambayo hadi sasa watu wamepoteza maisha na kuitwa walikuwa waadilifu.
 
Kubenea, siku ya kwanza tu kaja na mada ya shanga daaah!! Nilimfuta siku ile ile nani alimwambia matatizo ya wana Ubungo ni shanga za kike.
 
Kama wabunge wenye upeo wa juu wa kujenga hoja ccm Ni milinga, mkamia na yule aliyetamani kulia bungeni basi kweli upinzani wameishiwa
 
Ukizidisha sana positivity au negativity katika kujadili hoja basi " lazima tutahoji" na lengo la mwandishi.
Una dhamira tofauti au chuki binafsi juu ya characters wako na hivyo kuharibu dhima yote ya andishi lako.
Asante kwa kuja[/]
Nia hapa ni kuwarekebisha mapungufu yao.
 
Ukizidisha sana positivity au negativity katika kujadili hoja basi " lazima tutahoji" na lengo la mwandishi.
Una dhamira tofauti au chuki binafsi juu ya characters wako na hivyo kuharibu dhima yote ya andishi lako.
Asante kwa kuja
Dogo hoja ya leo imeangazia umzigo wa baadhi ya wabunge chadema.Jikite hapo ili tuwakosoe wajirekebishe kwa faida ya wananchi.
 
Ndiyo great thinker huyo. Halafu tunataka nchi yenye maendeleo ya viwanda.
 
Back
Top Bottom