Mawaziri Jenister Mhagama na Damas Ndumbaro hawana upendo kwa wafanyakazi kabisa

Tatizo watu hawataki kuamini kuwa cheo ni DHAMANA Wengi wao wana chukulia kuwa cheo ni MTAJI WA MAISHA ndio maaana hata kama akikosea yeye au walio chini yake kamwe hawezi kuwajibika kwa hiari yake mpaka awajibishwe.
 
Kwa miaka 6 Jensiter na Ndumbaro wamekuwa wakishikilia portfolios muhimu sana za kuangalia maslahi ya wafanyakazi. Hata hivyo mpaka sasa hamna chcochote cha kujivunia wanachoweza ongea kuhusu wafanyakazi. Jesnister tangu akute ile Wage Order ya mishahara ya watu wa sekta binafsi ya Mwaka 2013 hajawahi hata kuiongelea mahali.

Huyu mama na mwenzake Ndumbaro hawa-reflect kabisa roho nzuri za watu wa Ruvuma walizonazo. Sijui wamekuwaje hawa? Yaani bure kabisa! Na Mwenyezi Mungu awaangalie pamoja na nafasi zao zinazowapata kiburi wasije pata amani kamwe kwa matendo yao mabaya wakimaliza utumishi wa umma.

Ndumbaro mpaka ameingia Samia leo ndiyo anaona umihumu wa kuwalipa wa darasa la saba. Yaani wewe ni bendera fuata upepo tu - hufai pale utumishi. Na siku ukiondolewa ni lazima watumishi watapiga vigelegele! Ndumbaro ni msomi mzuri tu lakini hujali hata wale waliokumbwa na sakata la vyeti feki pia walihitaji kulipwa fedha zao kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii.

Hawa watu walifanya kazi na Katiba ya Nchi inawapa haki ya kulipwa ujira wao. Serikali yenyewe ilikuwa dhaifu kuajiri wa vyeti feki lakini yenyewe imeshindwa kujiwajibisha kwa makosa iliyofanya. Nchi hii mjenga chuki sana sana. Ndiyo maana Kiongozi mkubwa wa nchi anafariki wananchi wanashangilia.

Hata kama mnafikiri walioshangilia ni wachache bado pia wana impact. Hamjiulizi mbona Nyere na Mkapa walipofariki hamna hata mtu mmoja alionekana kushangilia?

Acheni roho mbaya - madaraka ni ya kupita tu! Mngemshauri vema Rais leo wafanyakazi wangekuwa wanafurahi na familia zao!
Kando ya barabara walikuwa wanalia, kushangaa, au kushangilia
 
Back
Top Bottom