OSOKONI
JF-Expert Member
- Oct 20, 2011
- 10,965
- 5,336
WAKATI tetesi za kupanguliwa Baraza la Mawaziri zikizidi kupamba moto, hali ya afya ya baadhi ya mawaziri imeelezwa kuwa tete hivyo kulazimika kupelekwa India kwa matibabu.Miongoni mwa Mawaziri hao ni wa Viwanda na Biashara, Dk Cyril Chami ambaye jana aliibuka na kuwataka watu aliowaita wanye uchu wa kuchukua nafasi yake, waache mara moja kutumia afya yake kupiga propaganda chafu za kisiasa.
Hadi sasa, mawaziri ambao taarifa za kuugua kwao zinafahamika ni pamoja na Profesa Mark Mwandosya mwenye dhamana ya Maji, Naibu Waziri Ujenzi, Dk Harrison Mwakyembe na Dk Chami. Wengine ambao taarifa zinaonyesha kuwa walikuwa nje ya nchi kwa matibabu ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Mathias Chikawe na Waziri wa Sheria na Katiba, Celina Kombani.
Ingawa haijafahamika maradhi yanayowasumbua hadi sasa, wadadisi wa mambo ya kisiasa wamekuwa wakichukulia hali ya afya ya baadhi yao kama moja ya sababu inayoweza kuwafanya wawekwe kando pale Rais Jakaya Kikwete atakapoamua kufanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri ili kuwapa fursa ya kupumzika na kuendelea na matibabu
MWANANCHI