Mawaziri hawa wana tatizo gani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mawaziri hawa wana tatizo gani?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by OSOKONI, Feb 16, 2012.

 1. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #1
  Feb 16, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,797
  Likes Received: 3,883
  Trophy Points: 280
  WAKATI tetesi za kupanguliwa Baraza la Mawaziri zikizidi kupamba moto, hali ya afya ya baadhi ya mawaziri imeelezwa kuwa tete hivyo kulazimika kupelekwa India kwa matibabu.Miongoni mwa Mawaziri hao ni wa Viwanda na Biashara, Dk Cyril Chami ambaye jana aliibuka na kuwataka watu aliowaita wanye uchu wa kuchukua nafasi yake, waache mara moja kutumia afya yake kupiga propaganda chafu za kisiasa.

  Hadi sasa, mawaziri ambao taarifa za kuugua kwao zinafahamika ni pamoja na Profesa Mark Mwandosya mwenye dhamana ya Maji, Naibu Waziri Ujenzi, Dk Harrison Mwakyembe na Dk Chami. Wengine ambao taarifa zinaonyesha kuwa walikuwa nje ya nchi kwa matibabu ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Mathias Chikawe na Waziri wa Sheria na Katiba, Celina Kombani.

  Ingawa haijafahamika maradhi yanayowasumbua hadi sasa, wadadisi wa mambo ya kisiasa wamekuwa wakichukulia hali ya afya ya baadhi yao kama moja ya sababu inayoweza kuwafanya wawekwe kando pale Rais Jakaya Kikwete atakapoamua kufanya mabadiliko ya Baraza la Mawaziri ili kuwapa fursa ya kupumzika na kuendelea na matibabu
  MWANANCHI
   
 2. B

  BMT JF-Expert Member

  #2
  Feb 16, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 570
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 45
  tmebaki na mawaziri wawili tu tibaijuka na magufuli,pamoja na naibu wetu mwanri,hao uliowataja wakapumzike tu jaman,na tena mwanri anafaa kuwa waziri mkuu
   
 3. Nyangomboli

  Nyangomboli JF-Expert Member

  #3
  Feb 16, 2012
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 2,307
  Likes Received: 649
  Trophy Points: 280
  kwa sababu ya kelele zake za juzi iringa? Au kuna cha ajabu kingine alikifanya wapi?
   
 4. mfereji maringo

  mfereji maringo JF-Expert Member

  #4
  Feb 16, 2012
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 1,003
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  mwanri anatoa macho sana hana lolote kada mahiri wa chama hawezi kuongoza ktk zama hizi za ustaarabu wa itikadi tofauti.
   
 5. nashy

  nashy JF-Expert Member

  #5
  Feb 16, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 679
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Pinda naye apumzike. Hivi sophia Simba naye bado ni waziri?
   
 6. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #6
  Feb 16, 2012
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,922
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  Hawa mafisi wanaosubiri miili ya mawaziri iingie kweny jeneza...watasubiri sana-by Chami
   
 7. Wambugani

  Wambugani JF-Expert Member

  #7
  Feb 16, 2012
  Joined: Dec 8, 2007
  Messages: 1,755
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Wewe umenena. Pia na Wakurugenzi wa Taasisi kama TBS na TAKUKURU nao wangepisha nafasi kwani utendaji wao una walakini.
   
 8. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #8
  Feb 16, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Kuvuja kwa pakacha nafuu ya mchukuzi, CELINA KOMBANI aendelee kuugua salama mpaka baraza jipya lipangwe.
   
 9. obsesd

  obsesd JF-Expert Member

  #9
  Feb 16, 2012
  Joined: Nov 23, 2011
  Messages: 1,226
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  yap, ni waziri bado, na yeye afya yake si nzurii sana ana matatizo ya moyo, huenda India kimyakimya kila kukicha!
   
 10. KOKUTONA

  KOKUTONA JF-Expert Member

  #10
  Feb 16, 2012
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 8,344
  Likes Received: 391
  Trophy Points: 180
  Hivi Rais hawezi kuteua wabunge wa vyama pinzani kuwa mawaziri?
   
 11. c

  chronic New Member

  #11
  Feb 16, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwa sababu ya kelele zake za juzi iringa? Au kuna cha ajabu kingine alikifanya wapi?[ AGREY mwanri Mbona ndio injini tangu kitambo.co kwa sababu ya kelele za iringa]
   
 12. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #12
  Feb 16, 2012
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,223
  Likes Received: 2,084
  Trophy Points: 280

  Tawire baba. Ingekuwa JK ni msikivu, angesham-sack Hosea miaka mingi sana, lkn kama unavyojua Hosea anajua inside out ya Richmond, ndo sababu yupo kazini hadi leo.
   
 13. pmwasyoke

  pmwasyoke JF-Expert Member

  #13
  Feb 16, 2012
  Joined: May 27, 2010
  Messages: 3,583
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Tibaijuka tu - sio huyo mwingine uliyemtaja
   
 14. commonmwananchi

  commonmwananchi JF-Expert Member

  #14
  Feb 16, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 2,149
  Likes Received: 476
  Trophy Points: 180
  Angel hebu tuhabarishe maana kweli kikao kilichopita pale dodoma hatukumuona huyu mama,kulikoni tena?
   
 15. R

  Renegade JF-Expert Member

  #15
  Feb 16, 2012
  Joined: Mar 18, 2009
  Messages: 3,767
  Likes Received: 1,072
  Trophy Points: 280
  Hivi na yule zeruzeru wa TRA Bado tu haijafika 60? Naona yule wa POLISI anafikisha 60 Sasa!Atastaafu au bado? Naona umri wa kustaafu unaongezwa kinyemela kila siku.
   
 16. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #16
  Feb 16, 2012
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,797
  Likes Received: 3,883
  Trophy Points: 280
  soma katiba yetu
   
 17. f

  faloyce2001 Member

  #17
  Feb 16, 2012
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tibaijuka nae kafanya nini hadi umsifie? Au kwa sababu alivunja ukuta wa mwarabu pale palm beach? Baada ya hapo nini kiliendelea kama si kuufyata mkia.
   
 18. odinyo

  odinyo JF-Expert Member

  #18
  Feb 16, 2012
  Joined: Feb 6, 2012
  Messages: 428
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  rafiki unajua gharama za baada ya kua waziri mkuu? kifupi ni noma
  ni bora aendelee pinda wetu kwanza ana busara sana la sivyo achaguliwe kiongozi ambaye tayari alisha kua rais au w.mkuu kuepuka hizo gharama.
  tuepende Tanzania yetu
   
 19. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #19
  Feb 16, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Taja wanaofaa na kwa wizara ipi?
   
 20. k

  kidumali Member

  #20
  Feb 16, 2012
  Joined: Feb 6, 2012
  Messages: 9
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hapo umesema kweli hakuna mabadiriko yoyote tunayotegemea ndani cha chama hiki, wote hawafai.
   
Loading...