HISIA KALI
JF-Expert Member
- Oct 26, 2010
- 694
- 108
Wale wa zamani nao wang`ang`ania makazi yao
Serikali bado inaendelea kupoteza mamilioni ya fedha kwa kuwalipia Mawaziri na Naibu Mawaziri kuishi hotelini baada ya kukosa nyumba za serikali.
Uchunguzi wa NIPASHE JUMAPILI umebaini kuwa bado mawaziri wanaendelea kuishi mahotelini kwa madai kwamba nyumba zao zinafanyiwa ukarabati.
Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kwamba baadhi ya viongozi hao wamepangishiwa nyumba za gharama (apartments), kwenye hoteli kubwa jijini Dar es Salaam.
Baadhi yao wanaishi Ubungo Plaza ambako gharama ni dola za Marekani 105 kwa siku na Protea ambako kwa siku ni kati ya dola za Marekani 155 na 180.
Uchunguzi zaidi unaonyesha kwamba chakula katika hoteli ya Protea ni dola 20 wakati Ubungo Plaza, gharama ya pango inajumuisha mlo mmoja.
Hata hivyo, sababu za kukosa nyumba haziwekwi bayana wakati takwimu zinaonyesha kwamba katika baraza la Mawaziri lililopita, Naibu Mawaziri walikuwa 21 na sasa idadi ni hiyo hiyo.
Mapema Januari mwaka huu, gazeti hili lilijulishwa kuwa mawaziri hao wataondoka katika hoteli hizo mwishoni mwa mwezi huo, lakini hadi sasa wanaendelea kuishi katika hoteli hizo.
Chanzo cha kuaminika kutoka Wizara ya Ujenzi kimeliarifu gazeti hili kwamba bado kuna mawaziri wa zamani ambao hawapo kwenye baraza la sasa, bado hawajaondoka kwenye nyumba za serikali jambo linalowafanya baadhi ya mawaziri wapya kuendelea kukaa kwenye mahoteli.
Chanzo hicho kiliendelea kueleza kuwa sababu zinazotolewa bado zinautata kwa kile kinachoelezwa kuwa nyumba zinafanyiwa ukarabati.
Chanzo hicho kilifafanua kuwa majibu hayo bado ya utata kwani haijawekwa bayana ukarabati huo utamalizika lini wakati serikali inaendelea kupoteza gharama nyingi pasipo na sababu za msingi.
Ofisa mmoja wa Wizara hiyo ambaye hakupenda jina lake litajwe gazetini, alisema ni kweli bado mawaziri wanaendelea kuishi hotelini.
Hata hivyo, alisema kuna baadhi ya mawaziri wamegoma kuishi katika nyumba za serikali kwa madai ya kuwa zina masharti magumu.
Alifafanua kuwa masharti yaliyowakwanza ni kutoruhusiwa kujishughulisha masuala mbalimbali ikiwemo kutolima mboga wala kufuga.
"Unajua kuna baadhi ya mawaziri walikuwa wakiishi katika nyumba zao ambapo walikuwa wanajishughulisha na mifugo yao halafu leo hii waambiwe wasijushughulishe na masuala yoyote yale jambo ambalo wameona wamewekeo masharti magumu sana hiyo ndio sababu ambayo imewafanya wasije katika nyumba zao walizowekewa kwani wanajiona hawapo huru," alisema ofisa huyo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Balozi Hurbert Mrango, ili azungumzie suala, hakukanusha wala kuthibitisha lakini alisema asingweza kulizungumzia kwa maelezo kwamba alikuwa kwenye kikao.
Msemaji wa Wizara hiyo, Martin Ntemo, alipotafutwa alimtaka mwandishi kuandika maswali na kuahidi kuyapeleka kwa Balozi Mrango ili ayatolee ufafanuzi.
Hata hivyo, ni takribani wiki mbili sasa tangu maswali hayo yalipowasilishwa wizarani hapo bila kupatiwa majibu yoyote.
Ntemo alipoulizwa majibu ya maswali hayo alisema kuwa mpaka sasa bado hajapatiwa majibu hayo.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI