Mawaziri 8 Wana Digriii bandia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mawaziri 8 Wana Digriii bandia

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Babuji, Apr 1, 2009.

  1. B

    Babuji Senior Member

    #1
    Apr 1, 2009
    Joined: Nov 27, 2008
    Messages: 198
    Likes Received: 0
    Trophy Points: 0
    VIGOGO wa Serikalini walio madarakani ambao walighushi shahada za degrii bandia wametakiwa kuachia nyadhifa hizo pia na kurudi shuleni.

    Msimamo huo umetolewa jana na Serikali kupitia Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Prof. Jumanne Maghembe.

    Kutolewa kwa msimamo huo ni baada ya uchunguzi wa kina uliofanywa na Serikali na kugundua kuwa kuna vigogo wengi Serikalini wakiwemo mawaziri nane wa Serikali ya sasa wametunukiwa digrii bandia baada ya kusoma vyuo feki vya nje ya nchi na ambavyo havitambuliki na Mamlaka ya Elimu nchini.

    Maghembe amesema kuwa, vigogo mbalimbali nchini wanaoshikilia nyadhifa mbaimbali kwa vyeti vya kughushi wanatakiwa waachie madaraka hayo mara moja na warudi tena darasani.

    Amesema kutokana na utata huo wa vigogo wengi walioshika madaraka katika idara mbalimbali nchini wenye digriii bandia walizozipata kwenye vyuo visivyotambulika na Tume ya Vyuo Vikuu nchini [TIC], Serikali imetoa ofa ya kuwalipia karo katika Chuo Kikuu Huria maofisa na watumishi wote waliokumbwa na tatizo hilo.

    “Wenye PHD za kughushi, shahada za uzamili na uzamivu wajitokeze hadharani na Serikali itawalipia gharama za masomo katika Chuo Kikuu huria” amesema Waziri Maghembe.

    Amesema kama watu hao wasipojitokeza na Serikali inawatambua basi hatua zitachukulia ikiwemo kuwaumbua hadharani endapo kama hawatajitokeza wenyewe.

    Source: Nifahamishe.com
     
  2. K

    Kiranja JF-Expert Member

    #2
    Apr 1, 2009
    Joined: May 19, 2007
    Messages: 754
    Likes Received: 4
    Trophy Points: 0
    waanze na Nchimbi , Batlida,Mathayo, Kamala,et all.
     
  3. M

    MzalendoHalisi JF-Expert Member

    #3
    Apr 1, 2009
    Joined: Jun 24, 2007
    Messages: 3,856
    Likes Received: 106
    Trophy Points: 160
    sasa kwa nini serikali tena iwalipie kwa makosa yao wenyewe?

    is it fair?
     
  4. M

    Mzawa Halisi JF-Expert Member

    #4
    Apr 1, 2009
    Joined: Feb 25, 2009
    Messages: 496
    Likes Received: 11
    Trophy Points: 35
    Hivi serikali imeshindwa njia za kuhakiki vyeti vya watendaji wake?
    Kwanini unampa option ya kurudi darasani mtu aliyegushi badala ya kumchukulia hatua za kisheria?
     
  5. Fidel80

    Fidel80 JF-Expert Member

    #5
    Apr 1, 2009
    Joined: May 3, 2008
    Messages: 21,982
    Likes Received: 77
    Trophy Points: 145
    Degrii lala hizo wengi wanajiita Madr. sijui wengine ni wale wa kienyeji?
     
  6. Msanii

    Msanii JF-Expert Member

    #6
    Apr 1, 2009
    Joined: Jul 4, 2007
    Messages: 6,271
    Likes Received: 126
    Trophy Points: 160
    Mary Nagu nasikia ni Dr. pia
     
  7. R

    Renegade JF-Expert Member

    #7
    Apr 1, 2009
    Joined: Mar 18, 2009
    Messages: 3,253
    Likes Received: 618
    Trophy Points: 280
    Amesema kutokana na utata huo wa vigogo wengi walioshika madaraka katika idara mbalimbali nchini wenye digriii bandia walizozipata kwenye vyuo visivyotambulika na Tume ya Vyuo Vikuu nchini [TIC],

    Mkuu Asante, ila siyo TIC,TIC ni Tanzania Investment centre, Hiyo ni TCU ,Tanzania Commission for Universities.
     
  8. Kamjingijingi

    Kamjingijingi JF-Expert Member

    #8
    Apr 1, 2009
    Joined: Mar 10, 2009
    Messages: 782
    Likes Received: 25
    Trophy Points: 45
    Hodi!!! ni mawaziri tu? au hata nawabunge ?
     
  9. Kamjingijingi

    Kamjingijingi JF-Expert Member

    #9
    Apr 1, 2009
    Joined: Mar 10, 2009
    Messages: 782
    Likes Received: 25
    Trophy Points: 45
    Hee!!maajabu ni haya wagushi vyeti halafu walipiwe karo??!! tena na fedha za wananchi??!! jamani, hawa watu!! wanafunzi wanaosoma wakitaka mkopo tu, ni matatizo, ni vurugu, ni kufukuzana vyuoni.. hao wagushaji wanabembelezwa?! hii mpaka lini?!! raia akienda kutafuta kazi, akachukua cheti cha kugusha, anafungwa..tena ni kesi kubwa.. je, hii ni haki ya binadamu?!
     
  10. K

    Kyachakiche JF-Expert Member

    #10
    Apr 1, 2009
    Joined: Feb 16, 2009
    Messages: 878
    Likes Received: 10
    Trophy Points: 35
    Usijali mkuu Fidel, kura za maoni za alibino zitawataja tu!
     
  11. Mujuni2

    Mujuni2 Senior Member

    #11
    Apr 1, 2009
    Joined: Jun 11, 2008
    Messages: 142
    Likes Received: 0
    Trophy Points: 33
    kuna utata wa tafsiri ya neno "kughushi" nadhani waziri alimaanisha kuwa wale waliopata degrees kutoka vyuo visivyotambulika(non-acredited universities).Kuwa na degree kutoka kati ya vyuo hivi haimaanishi kuwa umeghushi cheti. Cheti chako ni halali ila shule uliyosoma haijatimiza viwango vya kusajiliwa kama "acredited University" maana kughushi ni ciminal offense. I just wanted to clarify that.
     
  12. G

    Gozigumu JF-Expert Member

    #12
    Apr 1, 2009
    Joined: Mar 12, 2009
    Messages: 254
    Likes Received: 1
    Trophy Points: 0
    Mkowa wa Zanzibar nao unahusika?
     
  13. M

    Mfumwa JF-Expert Member

    #13
    Apr 1, 2009
    Joined: Aug 29, 2008
    Messages: 1,456
    Likes Received: 4
    Trophy Points: 135
    Kuna tofauti kati ya KUGHUSHI cheti na kusoma Chuo kisichotambulika. Ukighushi unatakiwa upelekwe katika vyombo vya sheria manake umefanya udanganyifu, lakini kama ulisoma chuo kisichotambulika basi huna kosa. Ni suala kurudia ile degree katika chuo kinachotambulika, lakini kama uliajiriwa kwa vigezo vya hiyo degree toka chuo kisichotambulika, basi unapoteza sifa ya hiyo ajira.
     
  14. N-handsome

    N-handsome JF-Expert Member

    #14
    Apr 1, 2009
    Joined: Jan 23, 2008
    Messages: 2,297
    Likes Received: 110
    Trophy Points: 160
    Wana JF huyu Mama alikua na scandal ya kujipa maallowance ya kufa mtu pale bunge la africa, issue iliishia vipi? na mijivyeo kibao aliyokuwa nayo ni lzm aeendelee kuwa mbunge wa ukerewe while ni Raisi wa Bunge la Africa?
     
  15. Killuminati

    Killuminati JF-Expert Member

    #15
    Apr 1, 2009
    Joined: Apr 24, 2007
    Messages: 319
    Likes Received: 7
    Trophy Points: 35
    Happy fools day!! This doesn't add up....walipiwe!!! says who???
     
  16. Masanilo

    Masanilo JF-Expert Member

    #16
    Apr 1, 2009
    Joined: Oct 2, 2007
    Messages: 22,320
    Likes Received: 133
    Trophy Points: 160
    Una maana mama Mongella ....I failed to link the dots....ama ndo April fools at large?
     
  17. Kikojozi

    Kikojozi JF-Expert Member

    #17
    Apr 1, 2009
    Joined: Mar 24, 2009
    Messages: 331
    Likes Received: 0
    Trophy Points: 0
    ....wametakiwa waachie.......????? Nani huyo anayetaka waachie? Hii nchi ina sheria ya kubana wanaoghushi? Kama ipo, ni nani mwenye mamlaka ya kuisimamia? Na kama "uchunguzi wa kina" umebainisha sheria imekiukwa, ni hatua gani zinapaswa zichukuliwe?

    WanaJF naomba mnisaidie na hayo maswali.

    Huu usanii na ushikaji utatupeleka pabaya.
     
  18. Kikojozi

    Kikojozi JF-Expert Member

    #18
    Apr 1, 2009
    Joined: Mar 24, 2009
    Messages: 331
    Likes Received: 0
    Trophy Points: 0
    Good clarification.

    I expected a better statement from the minister.
     
  19. KiuyaJibu

    KiuyaJibu JF-Expert Member

    #19
    Apr 1, 2009
    Joined: Aug 29, 2007
    Messages: 726
    Likes Received: 41
    Trophy Points: 45
    Hii habari nafikiri haiko sahihi,yaani naitilia mashaka kutokana na siku ya leo,halafu siyo TIC ni TCU(save this as provided herein).Na kama habari hii ni ya kweli basi serikali yetu ni kichwa cha mwendawazimu;katika hali ya kawaida kabisa hii ni kesi na kupoteza kazi kwa wote wataothibitishwa kuwa walikula shortcut ktk kupata hizo degree fake.Moja ya mfano mzuri si Kihiyo,mbona serikali inaremba hapa!!??
    Kama mpango huu utatekelezwa,itabidi serikali ishtakiwe.
     
  20. Cynic

    Cynic JF-Expert Member

    #20
    Apr 1, 2009
    Joined: Jan 5, 2009
    Messages: 5,156
    Likes Received: 618
    Trophy Points: 280
    Halafu sijui ni laana au ulevi wa usomi/PhD kwa wanasiasa wa kiafrica? za nini huko kwenye siasa?
     
Loading...