Mawasiliano ya TCRA kuhusu ving'amuzi vya TING

Mawasiliano ya TCRA kuhusu ving'amuzi vya TING

raky

JF-Expert Member
Joined
Nov 14, 2011
Posts
206
Reaction score
34
Wapendwa mwenye mawasiliano ya TCRA, hawa jamaa wa TING wanadharau sana halafu wahuni hawawezi kutukatia channels kwa mwezi mzima halafu bila majibu ya kuridhisha tena hata kuomba radhi kwenye media wao wapo kimya tu, tumechoka kama walikuwa hawajajiandaa si bora wangesubiri tu, lazima mkurugenzi wao ajiuzulu tu
 
TCRA ni sikio la kufa dawa mkuu;wameshavuta 10% hawana time na mwananchi mwenye kutumia hizo huduma!
 
Ting kwakweli wamefulia, ving'amuzi vya zamani walisema havitumiki tununue vipya. Najiuliza decoder gani nyingine itakuwa na channel za Kikristo niachane nao tu.
 
Hivi wadau naomba kuuliza tafadhali kwan chanel 10 na EATV ni za kulipia? Na zile chenel 5 walizosema TCRA ni za bure ni zipi hizo? Mpaka sasa nina ving'amuzi viwili ambavo nimevifungia kabatini maana havina maana tena kwangu
 
Ting kwakweli wamefulia, ving'amuzi vya zamani walisema havitumiki tununue vipya. Najiuliza decoder gani nyingine itakuwa na channel za Kikristo niachane nao tu.

yaan mimi mwenyewe nilinunua kwasbb niliona ina channels nyingi za dini, lakin wanachotufanyia sio vizuri kabsa, mi nahic wameshindwa biashara
 
TCRA ni sikio la kufa dawa mkuu;wameshavuta 10% hawana time na mwananchi mwenye kutumia hizo huduma!

duuh kazi tunayo hakuna mahali penye unafuu, watu wanawaza 10% tu, hawawazi hata hisia za mamilion wanazoziumiza,
 
Jamani. Kuwemi na huruma TING tuliichukua kwa sababu ya channel za dini. Tuambieni lolote basi kuhusiana na ukosefu wa EATV na zinginezo. Sasa tukimbile wapi, tushuhudie nini?
 
Wakati wa kununua kisimbuzi soma vizuri kuna maelezo kuwa kampuni itakuwa na uhuru wa kuondoa au kuongeza channel yoyote bila taarifa
 
Wapendwa mwenye mawasiliano ya TCRA, hawa jamaa wa TING wanadharau sana halafu wahuni hawawezi kutukatia channels kwa mwezi mzima halafu bila majibu ya kuridhisha tena hata kuomba radhi kwenye media wao wapo kimya tu, tumechoka kama walikuwa hawajajiandaa si bora wangesubiri tu, lazima mkurugenzi wao ajiuzulu tu
1
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
MAMLAKA YA MAWASILIANO TANZANIA

FOMU YA MALALAMIKO

A: MAELEZO BINAFSI
1. Jina la Mlalamikaji _______________________________________
_______________________________________________________
Anwani: ________________________________________________
_______________________________________________________
Kazi:
______________________________________________________
______________________________________________________

2. Jina la Mlalamikiwa: ____________________________________
_____________________________________________________
Anwani: ______________________________________________
______________________________________________________
______________________________________________________
______________________________________________________

2
B. AINA MAELEZO YA MALALAMIKO
(Toa maelezo ya wazi na kwa kifupi yatakayowezesha uchukuaji hatua)
1. ___________________________________________________________
2. ___________________________________________________________
3. ___________________________________________________________
4. ___________________________________________________________
5. ___________________________________________________________
6. ____________________________________________________________
7. ____________________________________________________________

C. AINA YA MALALAMIKO (Weka (v) kwenye aina yoyote ya malalamiko
yaliyoorodheshwa hapo chini)
o Bei kubwa
o Usambazaji usiotosheleza
o Utoaji duni wa huduma, utoshelevu na uaminikaji
o Matengenezo ya polepole
o Ankara zisizo sahihi na zisizojadilika
o Utendaji wa kirushwa katika upangiwaji wa huduma
o Matangazo ya uongo na yanayopotosha
o Ankara zisizo sahihi na zisizorekebishika viwango, gharama,
masharti na
o Uingiliaji wa siri.
o Taarifa zisizoeleweka na zisizokamilika kuhusu taratibu za bidhaa
zilizopo na zilizopendekezwa.
o Afya na Usalama.
o Kucheleswhewa Vifurushi
o Uharaibifu wa vifurushi/barua
o Usikivu hafifu wa matangazo
o Kukatizwa kwa matangazo bila taarifa 3
o Huduma kwa mteja.
o Nyingine (ainisha)

D. FIDIA INAYOTAKIWA (kwa ufupi sana)
________________________________________________________________
________________________________________________________________
_________________________________________________________________
_________________________________________________________________
_________________________________________________________________

E. UTHIBITISHO
Nathibitisha kuwa yote yaliyosemwa hapo juu ni ya kweli

.............................................................. ............................................................
Saini ya Mlalamikaji Tarehe

Imejazwa tarehe ................................ mwezi ..................... 200 .......................
.................................................................................
Mpokeaji wa Malalamiko wa TCRA

Imepokewa na Mlalamikiwa tarehe ............. mwezi..................... 200 ...............
..........................................................................
Mpokeaji Malalamiko wa Mlalamikiwa.

ukienda ktk website ya TCRA utakutana na fomu hiyo kwa ajili ya malalamiko ya aina hiyo na isitoshe TCRA wapo humu jamvini
 
Last edited by a moderator:
nashukuru sana, nitajaza hiyo form sitaituma nitaipeleka moja kwa moja kweny ofis zao,
 
Wapendwa mwenye mawasiliano ya TCRA, hawa jamaa wa TING wanadharau sana halafu wahuni hawawezi kutukatia channels kwa mwezi mzima halafu bila majibu ya kuridhisha tena hata kuomba radhi kwenye media wao wapo kimya tu, tumechoka kama walikuwa hawajajiandaa si bora wangesubiri tu, lazima mkurugenzi wao ajiuzulu tu

xiku nyingine unaponunua huduma uxixahau kauli mbiu hii ni muhimu
"VIGEZO NA MASHARTI KUZINGATIWA"
 
Back
Top Bottom