Abdul Said Naumanga
JF-Expert Member
- Jan 28, 2024
- 745
- 1,470
Chama cha Mawakili wa Serikali (PBA) kimesema hatua zilizochukuliwa na viongozi wa Chama Cha Wanasheria Tanganyika (TLS) cha kuwataka mawakili wa kujitegemea kutoshiriki kwenye shughuli za utoaji wa msaada wa kisheria kwa wananchi ni kinyume cha sheria za nchi na miiko ya kazi za wanasheria.
Akizungumza na waandishi wa habari Jiini Dar eskali Salaam, Mwenyekiti wa chama hicho, Wakili Addo November, amesema TLS, kama taasisi ya kisheria, ina wajibu wa kikatiba wa kuhakikisha kwamba maamuzi yake hayapingani na sheria iliyoianzisha (TLS Act) na sheria nyingine husika kama Legal Aid Act.
Vilevile, amesema taasisi zote za kitaaluma zinapaswa kushirikiana kwa weledi katika kulinda misingi ya haki, usawa, na utawala wa sheria, badala ya kuchukua hatua zinazoweza kuzorotesha huduma za kisheria kwa wananchi wa kawaida nchini.
Nao baadhi ya Mawakili wa Kujitegemea, akiwemo aliyewahi kuwa Rais wa Chama Cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Wakili Francis Stolla, wamesema TLS inapaswa kutetea haki za wanachama wake wanaoingia kwenye migogoro na vyombo vingine vya kisheria, pasi na kuvunja sheria na katiba ya nchi.
Chanzo @TBC @FLOW MEDIA tz
PIA SOMA:

View: https://youtu.be/vATHWZ-f14E?si=xOcZponr2om48VIH