Mawakili wa Joseph Mbilinyi(Sugu) wajipanga kukata rufaa

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,513
1.jpg

Baada ya mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi maarufu Sugu na Katibu wa CHADEMA Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga kuhukumiwa kifungo cha miezi mitano jela, wakili wao Peter Kibatala amesema wanakusudia kukata rufaa.

Sugu na Masonga wamehukumiwa adhabu hiyo leo Februari 26,2018 na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya, Michael Mteite.

Wawili hao wamehukumiwa kwa kosa la kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli, kosa walilotenda kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Desemba 30,2017 eneo la Uwanja wa Shule ya Msingi Mwenge jijini Mbeya.

Kibatala amesema baadaye watatoa taarifa ya nini kinaendelea ila wanakusudia kukata rufaa.

Baada ya hukumu kutolewa viongozi wa CHADEMA waliokuwepo mahakamani waliingia kwenye magari yao na kuelekea katika ofisi za chama hicho Kanda ya Nyanda za Juu Kusini.

Wakati wa usomwaji wa hukumu hiyo, nje ya jengo la mahakama ulinzi uliimarishwa kukiwa na askari waliotanda hadi maeneo ya jirani.

Sugu ni mbunge aliyeweka rekodi ya kupata kura nyingi kuwashinda wabunge wote wa majimbo katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

Katika uchaguzi huo, Sugu alipata kura 108,566 akiwaacha wapinzani wake kugawana kura 57,690.

Hukumu imetolewa na hakimu Mteite aliyesikiliza shauri hilo baada ya upande wa mashtaka na wa utetezi kukamilisha ushahidi Februari 9,2018.

Jamhuri iliwasilisha mashahidi watano na kielelezo kimoja cha sauti iliyodaiwa kurekodiwa na shahidi wa tano, Inspekta Joram Magova.

Upande wa utetezi uliwasilisha mashahidi sita wakiwamo Sugu na Masonga waliokana kutamka maneno waliyoshtakiwa kuyatoa.

Washtakiwa walitetewa na mawakili Sabina Yongo, Boniface Mwabukusi na Hekima Mwasipu kabla ya kujitoa na kazi hiyo kufanywa na Kibatala.

Kwa mara ya kwanza, Sugu na Masonga walifikishwa mahakamani Januari 16 na kusomewa mashtaka na Wakili wa Serikali Mkuu, Joseph Pande aliyeeleza upelelezi ulikuwa umekamilika na walikuwa tayari kuendelea na usikilizaji.



Mpekuzi
 
Kibatala anataka kupiga tu hela ya chadema
Kidhibiti kimewashika washitakiwa kwa 100% pasi na shaka yoyote anataka kukata rufaa ya nini kama si kutaka kumuongezea adhabu
Kwanza ashukuru hiyo miezi mitano,ingekua sita au zaidi angekosa sifa za kuwa mbunge
 
Upande wa utetezi uliwasilisha mashahidi sita wakiwamo Sugu na Masonga waliokana kutamka maneno waliyoshtakiwa kuyatoa.
Kama kweli wana uhakika na tuhuma walizozitoa jukwaani iweje mahakamani wakane kwamba hawakutamka? Kwa nini wasisimamie kile wanachokitamka jukwaani? Unapokana ina maana ulichokitamka kilikuwa hakina ukweli, kwa lugha nyingine ni uzushi. Sasa kwa nini uzushe mambo ambayo huna ushahidi nayo? Kama siyo uchochezi ni nini?
 
Kwa hiyo hana haki ya kukata rufaa.....!!?

Unaweza kuweka link ya ile video ...!!?
Kukata rufaa ni sawa na KUBET. Unaweza ukala au ukaliwa.
Kabla ya kukata rufaa inabidi kwanza aombe msamaha Magogoni, akishasamehewa ndio akate rufaa symbolically as a means to get out. Akiingia kichwa kichwa, rufaa itamcost. Note: These are staged events. They dont happen by chance.
 
Uamuzi wa mawakili kukata rufaa ni sawa na kucheza mchezo wa kubahatisha, "you either win or lose" na wakipoteza na Sugu wamempoteza sababu kamba aliyoning'inia nayo imekatika umebaki Uzi mmoja tu
 
Hayo ni mateke ya farasi anayekata roho.
Wakikata rufaa wanaweza kumcost mteja wao kwa kupewa kifungo kirefu zaidi kwa kuwa ushahidi wa makosa aliyotuhumiwa nayo upo na hauachi shaka yoyote.
kumbe na wewe hauko kama ninavyokufikiria. Unajua ingredients za sedition, incitement to violance. Is Magufuli synonymous toJohn Joseph Pombe Magufuli? Bila shaka mtu akisema "Magufuli"anamsema John Pombe Joseph Magufuli. Mtu akimsema "John" ana maanisha John Pombe Joseph Magufuli?



Sent from my HM NOTE 1LTEW using JamiiForums mobile app
 
Kibatala anataka kupiga tu hela ya chadema
Kidhibiti kimewashika washitakiwa kwa 100% pasi na shaka yoyote anataka kukata rufaa ya nini kama si kutaka kumuongezea adhabu
Kwanza ashukuru hiyo miezi mitano,ingekua sita au zaidi angekosa sifa za kuwa mbunge


Mkuu

Aisee una unaa wa hali ya juu.Una uhakika gani kidhibiti kilikua 100% pasi shaka?

Ulikuwepo tu hata mahakamani mkuu?

Haya tuchukulie basi hakimu katoa hukumu,ni sawa,ila inaweza iwe au isiwe ya haki pia.

Ndio maana sio vizuri kushabikia hukumu za watu.

Ila ni sawa pia,una ruhusiwa kushabikia chochote mkuu!You are entitled !
 
Wakijipendekeza kukata rufaa, wategemee adhabu kali zaidi. Utetezi wa Sugu ni kukana maneno yake au kukataa ushaidi wa audio ya polisi. Huu ni utetezi dhaifu, ashukuru tu hii adhabu imemstahi ubunge wake.
 
Mkuu

Aisee una unaa wa hali ya juu.Una uhakika gani kidhibiti kilikua 100% pasi shaka?

Ulikuwepo tu hata mahakamani mkuu?

Haya tuchukulie basi hakimu katoa hukumu,ni sawa,ila inaweza iwe au isiwe ya haki pia.

Ndio maana sio vizuri kushabikia hukumu za watu.

Ila ni sawa pia,una ruhusiwa kushabikia chochote mkuu!You are entitled !

Wewe unafikiria kwa nini hata Sugu mwenyewe ameishia kukana tu maneno yake? Umeona utetezi wowote wa Sugu? Polisi wana audio yeye Sugu ana nini?
Mwisho na muhimu, kama anaamini alichokuwa anaropoka kwa nini aende kukikana mahakamani.
 
Back
Top Bottom