Stara Thomas, mwimbaji wa zouk akiwa amevalia vazi murua kabisa!
Picha: hisani ya haki-hakingowi blog.
Vazi hili ndio nasikia lilichaguliwa kuwa vazi la taifa (la kike) hapa Tanzania. Sijui naota?
Stara Thomas, mwimbaji wa zouk akiwa amevalia vazi murua kabisa!
Picha: hisani ya haki-hakingowi blog.
Vazi hili ndio nasikia lilichaguliwa kuwa vazi la taifa (la kike) hapa Tanzania. Sijui naota?
Mama, lililochaguliwa kuwa vazi la taifa nafikiri liko hapo juu kidogo.. naomba ucheck tena.
BTW mama, je ni hizo rangi rangi za bendera ndizo zimekufanya ulipende na kusema hivyo au ni mishono?!
ooh kumbe, hilo limefanana kinijeria fulani hivi.
Vazi hili ndio haswaa liko distinct, kwani maana ya vazi la taifa ni nini hasa, labda hapo ndipo ninapokosea.
Nimevutiwa na vyote mwanangu mpendwa,
Rangi imekubaliana na dhana ya utaifa..though sio lazima tuvae hizo Rangi.
Mshono bwana, huu hauchagui umbile.
Hivi elegent maana yake nini?
Baada ya wewe kulizungumzia, limenivutia. Ambacho hakikunivutia ni hili linalofanana na dizini ya kinijeria. (Imekuwa bahati mbaya sipendezwi na vazi la kinaijeria).
Hilo alilotaja mama naona kama tuna husiana nalo kinamna flani hivi katika historia. Wamasai? Watu wa Pwani? Waislam? Southern of Sahara?
.