Maumivu: Wanaume tunapitia maumivu mengi sana

Maumivu: Wanaume tunapitia maumivu mengi sana

April26

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2020
Posts
1,405
Reaction score
2,163
Wakuu habari ya weekend. Bila shaka hamjambo, poleni kwa wanao pitia magumu. Amini ipo siku yatakwisha.

Moja kwa moja kwenye mada.

Maumivu.[emoji24]

Baadhi ya wanaume kuna wakati tunajifanya tuna furaha na tabasamu mbele za wapendwa wetu (watoto, wake, wazazi na ndugu zetu) kwa kuigiza furaha ya uongo na kweli hasa tunapokuwa na matatizo katika mambo kadhaa ya maisha ili watu wetu wanao tutegemea wasigundue maana wakijuwa tunayoyawaza na tunayopitia kihisia wataumia sana.

Wakati mwingine tunaonekana hatuko romantic yaani hatuna hisia na upendo kwa wenza, wazazi, ndugu na jamaa zetu, kumbe ni sababu ya magumu tunayo pambana nayo ili tuwafurahishe tunao wapenda.

Ni kwa sababu hawajui ndiyo maana wana furaha [emoji24]

Dhana ya wanaume kufa mapema ni dhahili kabisa kwa sababu tuna ishi na sumu nyingi sana za misongo ya mawazo, migogoro ya nafsi, mioyo iliyochafuka, hisia zilizo kufa, tamaa ya mafanikio, vipindi vigumu tunapitia, matusi kutoka kwa watu tunao wapenda, maadui wanaotaka kutukwamisha, wenye wivu na wengineo!!

Mungu akulinde wewe mwanaume unae pitia hali sumbufu na ngumu. Jipe moyo ipo siku moja utasahau yote??

FB_IMG_16675947061678571.jpg
 
Na awalaani wale wakiamka wanapost uzinzi TU.
Tunawaza kwa kupokezana na maono tofauti.Wakati weye unafikiria ukalime,mwingine anawaza awahi nyumba ya ibada.Wakati weye unawaza kwenda kwenye kazi yako ya ulinzi,kuna mtu anawaza achukue shuka gani ajifunike alale.Wakati weye unaenda kwenye mazishi,kuna mwenzio yupo na mwenzake wanawaza safari hii wapate mtoto wa jinsi gani!Heshimu mawazo ya mtu.Tusipotofautiana kimitazamo hatototofautishwa na wanyama hayawani.
 
Uko sahihi sana nikama mtoa mada anovodhani wanaume wote wanapitia mateso; kuna wanaume wanalelewa huko mijini, kuna kina bob risky kuna watoto wa matajiri sasa hao wanapitia mateso gani dhidi ya raha tu.
 
Hakuna ulichoelewa kutoka kwangu ila unataka ujielewe wewe kupitia mimi which is impossible.
 
Mbona hajaeleza kama yeye yupo okay sana na hana mateso.Kaandika tu si wote.Weye umemtafsiri namna gani?
Nimemuelewa anatumia defensive mechanism asijulikane anapitia magumu, hawa wa hivi simple kuwajuwa. Hana raha zozote huyu hiyo attack inajieleza. Yaani hajaona kilichokusudiwa yeye kakimbilia kujitetea.
 
Basi upo vizuri.Umeweza kusoma mawazo na maisha yake kwa kusoma alichokiandika tu?Anzisha kituo cha "Mind reader/reading"!Utapata wateja wengi.
 
Basi upo vizuri.Umeweza kusoma mawazo na maisha yake kwa kusoma alichokiandika tu?Anzisha kituo cha "Mind reader"!Utapata wateja wengi.
Mimi ni profession kabisa mkuu. Hicho alicho andika ni tabia pia. Kuna tabia ya ndani na nje, hapa hatuwezi ona tabia ya nje direct isipokuwa mawazo yake ndicho anachoweza perform nje pia.
 
Basi upo vizuri.Umeweza kusoma mawazo na maisha yake kwa kusoma alichokiandika tu?Anzisha kituo cha "Mind reader/reading"!Utapata wateja wengi.
Yeye anafosi shida anazopitia yeye au magumu au mateso anayopitia yeye basi kila mtu awe anayapitia. Mfano sio kila mwanaume anasumbuliwa na mapenzi, sio kila mwanaume ana mkwamo wa kiuchumi, pia sio kila mwanaume anayepitia magumu anajikaza au anakaa nayo moyoni kuna wengine hawawezi kukaa nayo na wanayaongea. Na sio kweli wanaume wameumbiwa mateso maana mateso ni kwa jinsi yoyote ile kulingana na namna akili yako inavyotafsiri. Mfano kuna mtu akila ugali maharage anaona ni mateso na kuna mwingine akipanda basi la abiria anaona ni mateso. Ni mindset tu sema mtoa mada anataka kutuaminisha wote tukubaliane na fikra zake kitu ambacho kwangu nakiona tayari ni mateso.
 
Tukubaliane kuto kukubaliana mkuu.

Au unasemaje !?
 
Wakati mwingine tunaonekana hatuko romantic yaani hatuna hisia na upendo kwa wenza, wazazi, ndugu na jamaa zetu, kumbe ni sababu ya magumu tunayo pambana nayo ili tuwafurahishe tunao wapenda.

View attachment 2407184
Kuna jamaa kipindi cha COVID mwaka 2020 taasisi aliyokuwa anafanyia kazi alipunguzwa kazini (redundancy)

Akawa anaogopa kuiambia familia yake yaani mama na watoto ili wasipate mshtuko.

Akawa anatoka asubuhi anajifanya anaenda kazini kumbe anapitia tu kwenye mishe zingine, kukutana na wadau aliosoma nao, aliofanya nao kazi na kuomba kazi sehemu nyingine

Baada ya miezi 3 akapata kazi nyingine akaja kumsimulia mke wake kwa nini kipindi cha miezi 3 mambo yalikuwa yamebadilika kwenye kipato.

Mwanamke alilia sana akasema unisamehe mume wangu kwa maneno na kauli zangu za kipindi cha miezi mitatu iliyopita baada ya kuona kipato kimepungua hapa nyumbani

Naungana na mleta uzi hasa uliposema wakati mwingine wanaume tunapitia magumu lakini tunaficha ili tuwafurahishe tunaowapenda
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom