fredrick850
Member
- Nov 21, 2015
- 12
- 2
Karibu sana
Lala kwenye ubao ukilalia kutumia mgongo kwa masaa 2 kila siku kwa muda wa siku 7
Unayo Dawa au unamjuwa anaejuwa kutibia huo Ugonjwa?kama unataka kumshauri, mshauri hata sasa kwa manufaa ya wote!!
Nielekeze mie niende au nipe Contact za huyo Bingwa niongee nae km yupo!Bingwa mwingine wa matizo ya pingili za uti wa mgongo yupo Tanga mjini eneo laitwa kibiboni.
Sharti uwe umepiga x-ray na tatizo kuthibitishwa.
Poleni sana.
Ngoja, waje wataalamu.
Pole sana kaka!Habarini za muda huu wakuu, binafsi mi mzima saana.... ni matumaini yangu pia nyie wenzangu ni wazima.
Kilichofanya niandike uzi huu leo
Ni kuhusu afya ya shemeji/wifi yenu anaesumbuliwa na tatizo la kuumwa mgongo, kisogo na misuli ya shingo kukaza. Tatizo hili humtokea pindi anapokuwa anafanya kazi za kutumia akili kubwa sanasana akiwa anasoma na Limemuanza tokea december ya 2015. Tumeenda hospitali zaidi ya moja kuchukua vipimo.. X-ray.. Sindano kachomwa lakini hadi leo hali inajirudia.
Anateseka kweli kweli na maumivu anayoyapata yananikosesha raha maana mnajua kuuguza mke ni kazi. Hivyo kwa mtu mwenye uelewa na huu ugonjwa naomba msaada.. Pia kwa mwenye kujua tiba naomba msaada wako na. Ushauri wako.
... Nitafurahi saaa kama nitakutana na ushuhuda humuhumu.
Pole sana kaka!
Kama vipimo hivyo vilionesha hakuna tatizo, na maumivu bado yanaendelea,nakushauri usikate tamaa, endelea kufuatilia kwenye hospitali hizi kubwakubwa, waone wataalamu wa neuro/nerve au wataalamu wa mifupa watakupatia ufumbuzi wa tatizo la mwenza wako. Mi wangu alikuwa anasumbuliwa na maumivu ya mgongo kila siku haachi kulalamika, na akifanya kazi ngumu ndo basi kabisaa, tulitembea kwenye hizi hospitali za kawaida hatupati ufumbuzi, X-ray tulipiga lakini hamna tatizo lolote, tukazidi kumwomba Mungu! Baadae tukaenda hospitali moja kubwa tu hapa Tanzania, tukafanya vipimo viwili X-ray na MRI ndipo tatizo lilipoonekana, lakini halikuwa kubwa sana, Daktari akatuandikia dawa na asisitizia juu kufanya mazoezi.
Baada ya pale tukaenda kwa Physiotherapist, akamfanyia mazoezi ya viungo nami pia akanielekeza namna ya kumfanyia,basi nikawa namfanyia mazoezi mimi mwenyewe nyumbani! Sasa hivi yapata miezi miwili tangu tuanze hiyo tiba hajalalamika tena maumivu ya mgongo!
Kitu cha msingi kaka, itabidi uangali wale madaktari bingwa kwenye hizi hospitali kubwa,lakini pia usisahau kumuomba Mungu kwani Yeye Ndiye Muweza wa yote!
MNH kitengo cha mifupa!!Thanks saana mkuu kwa ushauri.. Ingekuwa vizuri kama ungenitajia hiyo hospitali ili niende
MNH kitengo cha mifupa!!
Shukran kWa mawazo yakoBadili godoro
Sawa mkuunenda hospital dr atajua nini afanye kulijua tatizo lako
ukisema mgongo kitaalamu ni pingiri kuanzia shingoni hadi kiunoni
na mgongo unagawanywa sehemu kuu tatu
1cervical spine
2 thoracic spine
3.lumbar spine
so dactor ataangalia wapi achuchunguze kujua tatizo lako
vipimo vya kufanya kama ni mgongo
1.xray
2. ct scan
3.mri
hivi vipimo vitakusaidia kujua tatizo kama ni mgongo