Maumivu makali ya mgongo (back pain) na tiba yake

Nina miaka takribani miwili sasa huwa nasikia miguu yote kuanzia kiunoni, mapajani na miundi maumivu ya kuungua moto na saa nyingine kama radiating sensation.

Kwa siku za karibu maumivu kama hayo nayasikia pia kwenye pingili za chini ya uti wa mgongo. Maumivu haya hayaumi muda wote na huwa inafikia hatua yanapotea yenyewe tu lakini hurudi tena baada ya muda fulani.

Nlienda kwa daktari wa AGA KHANI wa viungo hapa MWANZA akanipiga X-ray 3 kwenye uti wa mgongo lakini hakuona chochote na akaamua tu kunifanyia mazoezi ya mgongo lakini sikupata badiliko lolote la msingi.

Naomba kusaidiwa kufahamu tatizo ni nini na tiba yake ni ipi

Asanteni
FAHAMU SABABU ZA MAUMIVU YA MGONGO NA TIBA YAKE ASILI HAPA

mgongo.jpeg



Hali ya maumivu ya mgongo huwatesa watu wengi hasa wale wenye umri miubwa jambo ambalo husababisha awatu hao kutojisikia vizuri au kawaida katika misuli au mifupa ya mgongo wako.
Moja ya sababu za maumivu ya mgongo ni aina ya kazi unayofanya. Kazi inayohitaji muda mwingi katika kukaa/kusimama au unaifanya ukiwa katika mkao wa kuinama huchangia sana maumivu ya mgongo.

Sababu nyingine ni ubebaji wa mizigo mizito usiozingatia afya ya mgongo na hata kulalia matandiko (magodoro) laini wakati wa kulala.
Uzito wa kupita kiasi (ujauzito, kitambi) huweza kusababisha maumivu ya mgongo, ila akina mama wajawazito wanafahamu! Kinachotokea huwa ni kubadilika kwa mfumo mzima wa maumbile ya mgongo na hivyo kusababisha baadhi ya misuli/mifupa kubeba uzito wakati wa kukaa au kusimama.

Sababu nyingine ni pamoja na magonjwa yanayoathiri mifupa (pingili) za mgongo kama vile TB ya mifupa ya mgongo, lakini pia kuvunjika au kuhama kwa mifupa ya mgogo kutoka nafasi yake ya hapo awali kutokana na sababu mbali mbali ikiwemo ajali huweza kuwa sababu pia ya maumivu ya mgongo.

Mbali na sababu hizo pia umri wa uzeeni ni mojawapo ya sababu ya maumivu ya mgongo, kadri mtu anavyozidi kuukaribia uzee ndivyo kunavyozidi kutokea mabadiliko katika mifumo yote ya mwili ikiwemo ile ya mifupa na misuli hivyo kuleta matatizo mengine ya kimfumo yakiwemo maumivu ya mgongo na mengineyo.

Sasa baada ya kufahamu sababu hizo ambazo huchangia maumivu ya mgongo ni vyema ikafahamika kwamba kuna baadhi ya vitu asili huweza kutumika kutibu matatizo haya ya maumivu ya mgongo.

Hapa napenda kukwambia kwamba kitunguu swaumu huweza kutuliza maumivu ya mgongo ambapo utahitajika kusaga punje za kitunguu swaumu kisha tumia lojo lojo yake kuchua ile sehemu yenye maumivu. Fanya zoezi hilo asubuhi na jioni kila siku kwa muda wa wiki mbili na utaona mabadiliko.

UKIHITAJI TIBA YA MGONGO UNAWEZA KUNITAFUTA KWA
Mawasiliano MziziMkavu Email barua ya pepe. fewgoodman@hotmail.com What's App na Viber +905344508169
 
Wakuu natumai hamjambo. Nina sumbuliwa na maumivu ambyo huanzia kwenye uti wa mgongo juu kidogo ya kiuno na kusambaa kwenye misuli ya tumbo pande zote. Maumivu haya hutokea kama "electric shocks" na makali hasa wakati wa kusimama. Baada ya muda hutulia na hutokea wakati wa kukaa au kulala. Kuna wakati inabidi kushikilia kitu kilicho jirani ili kuepuka kuanguka. Nawaombeni msaada wa tiba au ushauri. Natanguliza shukurani.
 
Habari zenu wanajamii forum, nilikuwa naomba msaada wenu hasa kwa mtu anayefahamu tiba ya tatizo la kukaza na kuwaka moto misuli ya mgongo, tatizo hili lilinianza muda mrefu wakati nikiwa mwanafunzi wa sekondari mpaka sasa linaendelea, lilianza na kupata maumivu ya mgongo kuanzia kwenye shingo mpaka katikati ya mgongo na mpaka leo ipo hivyo, Mara nyingi likianza mgongo huwa na maumivu kama moto unawaka, nilienda hospital nikapingwa Ex-wakaniambia tatizo misuli imejikaza sana ndiyo maana unahisi kama moto unawaka, nikapewa dawa na nimetumia mwaka mzima bila mafanikio, nikaenda hospital nyingine mwaka huu wakaniandikia kufanya Kipimo cha MRI na nilifanyiwa hicho kipimo na tatizo likaonekana ni misuli, nikaandikiwa kufanya mazoez ya viungo (Physiotherapy) na dawa lakini naona Hakuna mafanikio, kuna muda huwa mgongo unauma sana na huwa nafanya mazoezi ya viungo mfano wa yoga mpaka ninapoona misuli ina stretch kidogo ndiyo maumivu hupungua na inaweza kutulia kwa muda, tatizo hili linaninyima Amani sana na limekuwa likisababisha hata nisifanye vizuri darasani maana likianza lazima nipumzike nakuwa na joto kali kama la Homa na maumivu yanakuwa kwenye mgongo tuu tena kuanzia kwenye mabega mpaka katikati ya mgongo. Naomba msaada wenu kwa yeyote anayefahamu tiba mbadala anisaidie maana za hospital naona zimedunda.
Nawasilisha
Ahsante
 
Habari za wakati ndugu wapendwa wanaJF!

Yamkini wengi wetu tumekuwa tukisumbuliwa na maumivu ya mgongo pengine kutokana na shughuri mbalimbali za kila siku au pia uchovu kutokana na umri.

Hii itahusika zaidi kwa wale ambao tatizo limekuwa sugu kiasi cha kufanyiwa uchunguzi wa kitabibu na kujiridhisha kuwa hawasumbuliwi na maradhi ambayo pengine huanza kama hali ya kawaida ya kujisikia maumivu ya kiuno na mgongo.

Nashauri kabla hujajihusisha na tiba hii ni bora kufanya uchunguzi kwanza wa maradhi kama tb ya mifupa n.k ikiwa tatizo lako ni kubwa sana.

Nafahamu kuna baadhi watahoji juu ya namna ya utekelezaji wa hii tiba. Ila ninaamini wapo pia watakao ona umuhimu wa kusoma na kuelewa na hatimae kunufaika na kile nitakachoelezea hapa kulingana na hitaji la mtu. Ninasema hivyo kwasababu wengi wetu tuna kasumba ya kubeza kila taarifa hasa hizi zinazohusiana na masuala ya tamaduni.

Hii elimu nilipewa bure ndiyo maana nimepata msukumo wa kuitoa bure kwenu pia kama asante kwa JF kwa mambo mengi niliyonufaika tangu nijiunge.

Hii tiba imegawanyika katika sehemu kuu mbili ambazo zitatekelezwa kwa awamu mbili kama ifuatavyo;
1) Mahitaji; tangawizi mbichi 2, unga wa mizizi ya tulatula(ndulele ndogo) robo kilo, asali mbichi robo lita, kinu na mchi wake pamoja na kiwembe ambacho hakijatumika.

Maandalizi; saga tangawizi kisha changanya na unga wa tulatula kiasi cha angalau vizibo5.
Matumizi/Tiba; Baada ya kupata mchanganyiko sahihi fanya yafuatayo kwa usaidizi wa mtu wako wa karibu:
Nenda kalale katikati ya mlango wakutokea kiuno kibaki ndani ya nyumba huku kiwiliwili na kichwa kikiwa nje.

Huyo msaidizi atakuchanja chale kadhaa kiunoni na kukupaka mchanganyiko wa unga na asali mithiri ya mtu anaechua kwa nguvu kuanzia kiunoni kuelekea mgongoni pote. Kisha atachukua kile kinu na kukisimamisha juu ya kiuno ukiwa umelala atwange mara3 kwa kishindo na mgonjwa utaamka na kutoka nje ya nyumba.

Unaweza kuendelea kujichua hii dawa asbuhi nusu saa hadi saa zima kabla hujaoga na jioni baada ya kazi kwa muda wa siku2 hadi3 ili kujihakikishia matokeo mazuri zaidi.

Sehemu ya pili;
Mahitaji: Tafuta na uchukue Jongoo aliefia njiani na mchanga wa sehemu aliyofia, siafu wawili wanaopisha(dume na jike) n.b utawapata kwenye kundi la siafu maana ni jadi yao kufanyakazi kwa kupishanapishana huku wakitembea. Pia usisahau kuzoa na mchanga wao kiasi kidogo sana tumia kidolegumba na chenzie kama vile uchukuavyo tembe ya dawa.

Kiwembe kipya ambacho hakijatumika.

Maandalizi: Vyote kwa pamoja yaani jongoo+siafu+mchanga vikaange kwenye sufuria ya moto(usiunguze sana) kisha usage pamoja viwe unga.

Muombe mtu akuchanje chale kadhaa kiunoni na mgongoni kisha asiginie huo unga kwenye hizo chale mgonjwa ukiwa umesimama wima bila kutingishika wala kuangalia nyuma na utatazama mbele jua linapotokea.

Najua kuna maswali ntaulizwa hapa;

Swali1 kwanini ifanyikie mlangoni?
Jibu; Inafanyika hivyo kama tafasiri ya kuzaliwa upya. Yaani siku ulipokuwa unatoka tumboni mwa mama(makalio na kiuno vikiwa ndani) kuletwa duniani (nje ukiwa umetanguliza kiwiliwili)

swali2 kwanini kinu&mwichi?
Jibu; kuonesha msisitizo kwamba you are now delivered new with all the strengh that God induced within your body as a sign of complete creation.

swali3 kwa nini kuchanjwa chale?
Jibu; ili dawa iingie vizuri na ikumbukwe kuwa siku ya kuzaliwa kwako damu ilimwagika hivyo the whole context in here is like being re-born.

Swali4 Kwa nini jongoo?
Jibu: Kila mtu anamfahamu fika jongoo na madoido yake ya kujikunja licha ya kuwa na mapingili pingili hii inaashiria kwamba yupo very flexible in either way!

Swali5:Kwanini siafu wanaopishana?
Jibu: Siafu dume na jike wanawakilisha mchezo wa KIBABA BABA" na kama ujuavyo wadudu hawa hawachoki wanapiga kazi 24/7 iwe juani, majini,kivulini wao ni full kupishana tuu huku dume likiwa na sura ya kazi muda wote!!!

So sincerely from within my heart i wished to grant this knowledge to all JF members ili mrudishe heshima majumbani kwenye ndoa zenu na kule kazini kwa mkoloni sio kila siku unashindwa kutimiza wajibu kisa maumivu ya mgongo.

NB. Muda huu ni kipindi cha baridi kali, kwa wale wenye matatizo ya PUMU (ASTHMA) tutafutane mpate suruhisho.

Wasalaam,
Kisima aka BABU WA SHAMBA.



Mungu akutunze uendelee kuwapo ...nimehangaika na madawa na mume wangu jaman last week nikahangaika kwa mitandao kutafuta tba mana alikuwa analalamika kama mtt maumiv ,,,,nilifanya tba ya tulatula ubarikiwe sana,, niimchanja,, nikamfanyia massage 5days,na kaila siku tatu asubuh vijiko vinne na usiku vinne...huo huo mchanganyoko....saiv mume wangu anaenda kazin bila shida ...asante sana
 
Mungu akutunze uendelee kuwapo ...nimehangaika na madawa na mume wangu jaman last week nikahangaika kwa mitandao kutafuta tba mana alikuwa analalamika kama mtt maumiv ,,,,nilifanya tba ya tulatula ubarikiwe sana,, niimchanja,, nikamfanyia massage 5days,na kaila siku tatu asubuh vijiko vinne na usiku vinne...huo huo mchanganyoko....saiv mume wangu anaenda kazin bila shida ...asante sana
Wow! nilishasahau kama nilitoa bandiko hili hapa jukwaani!
Hongera kwa uthubutu na hatimae umeokoa na kutetea ndoa yako mkuu.
Iwe msaada kwa wengine pia. Uzuri ipo humu ndani haitafutika kamwe. Naamini vizazi na vizazi watatumia ujuzi huu kuimarisha afya zao.
Asante kwa mrejesho na kuthamini mchango wangu. Nimefarijika sana...!
 
Mbona haiwork kwa ndugu yangu
Pole sana mkuu. Naamini mlifuata utaratibu wa vipimo na tiba nyingine kabla hamjahamia huku. Kuna uwezekano pengine nduguyo ana tatizo jingine kabisa.

Fanyeni uchunguzi wa tb ya mifupa n.k waone wataalam wa SUA kwa uchunguzi wa kina kuhusu tb pale wana kitengo hicho kwa kutumia panya maalum.
 
Habari wadau, Poleni na majukumu ya kila siku.

Wadau baada ya siku mbili nikifanya tendo la ndoa mgongo unaniuma kama unataka kukatika flani hivi. Msaada katika hili nini chanzo na matibabu yake. MziziMkavu Watu8 au yeyeto anayejua tatizo hili tafadhali.

Lyandembela1.
 
Je katika shughuli zako za kutwa huwa unatumia nguvu nyingi kufanya kazi zako za kila siku? Fanya utafiti hivi kaa siku moja bila ya kufanya kazi yoyote ya nguvu na ikifika wakati wa kufanya tendo la ndoa fanya kisha uje utupe mrejesho wako je bado unaumwa na huo mgongo ukifanya tendo la ndoa? kama bado itakuwa unaumwa na huo mgongo itabidi uende hospitali kufanya check up ya Afya yako utakuwa na hitilafu mwilini mwako katika viungo vyako uguwa pole kunywa maji mengi ya Uvuguvugu itakusaidia kukutibu maumivu ya mgongo wako.
 
Jogi Tunaomba Address au Contact number ya kufika Igoma Mwanza kwa huyo Daktari Bingwa wa Uti wa Mgongo nasi akatutibie maana tuna tatizo km lako"!
Utusaidie bila kukosa,tunatanguliza Shukrani kwako"!
 
Mimi nimepona kwa maombi hilo tatizo lilinisumbua miaka mingi hadi nikakata tamaa mwaka 2010 nikaambwa nina disc degenerative disease, 2012 nikaombewa mpaka sasa nimesahau hata kama niliwahi kuumwa pingili. Huu ni ushuhuda wa kweli kabisa, kabla ya hapo nilikuwa siamini kabisa kama mtu anaweza kuombewa na kupona.
 
Mimi nimepona kwa maombi hilo tatizo lilinisumbua miaka mingi hadi nikakata tamaa mwaka 2010 nikaambwa nina disc degenerative disease, 2012 nikaombewa mpaka sasa nimesahau hata kama niliwahi kuumwa pingili. Huu ni ushuhuda wa kweli kabisa, kabla ya hapo nilikuwa siamini kabisa kama mtu anaweza kuombewa na kupona.
Uliombewa wapi mkuu, mi nasumbuliwa na spinal cord injury imenifanya nipooze kabsa mguu mmoj mpk saiv two years
 
Bingwa mwingine wa matizo ya pingili za uti wa mgongo yupo Tanga mjini eneo laitwa kibiboni.

Sharti uwe umepiga x-ray na tatizo kuthibitishwa.
Mkuu tupe msaada wa mawasiliano ya huyo bingwa tumtafute
 
Mkuu tupe msaada wa mawasiliano ya huyo bingwa tumtafute
Bahati mbaya namba ya simu nimeipoteza, lakini kwa umaarufu wa jina la kazi yake na eneo ni anuani tosha.
"mtaalam wa mifupa, kibiboni tanga" unafika bila shaka.
 
Kwa majina naitwa andrew mkazi wa songea, nina miaka 23 nasoma.
"Nina tatizo la maumivu katka pingiri moja juu kidogo ya kiuno ni zaidi ya miaka 5 sasa lakini sijabahatika kupona,
Nimetumia dawa mbalimbali lakini bado hayo maumivu hayajapona, nimeenda hosipitali mbalimbali km PERAMIHO,
lakin sijafanikiwa,nimejitokeza kwenu wana JF ili niweze kupata hata ushauri au tiba kwani hyo maumivu yana
leta uchovu muda wote huwa nachoka, nasahau kwasababu ya hayo maumivu, yaan huwa sitaman kulala maana
nikilala2 ndio ugonjwa unazidi,hosipitali zote nilizoenda wanasema sinatatizo bt mimi mwenyewe nasikia maumivu
ktk pingiri hyo moja. Kipindi nasoma nilikuwa natumia baiskeli kma usafiri wangu wakunifikisha shule kwa miaka yote,
minne(4),nimewaikudondoka nayo mara moja(1) tu kwa miaka yote,tatizo limeanza tu pale nilipo maliza mwaka 2010
wakati nilpoacha kutumia baiskeli lakin vle vle nishawai kujichua sa cjajua nn chanzo cha tatizo kati yahivyo.Naitaji
sana msaada wenu wana JF unaweza kunisaidia"
Ni mimi
andrew@josephina is my mumy!
Nitafute mimi nipate kukutibia upate kupona ukihitaji matibabu yangu
Unaweza kunitafuta kwa Mawasiliano Dr. MziziMkavu Email barua ya pepe. fewgoodman@hotmail.com What's App na Viber +905344508169
 
Mimi nimepona kwa maombi hilo tatizo lilinisumbua miaka mingi hadi nikakata tamaa mwaka 2010 nikaambwa nina disc degenerative disease, 2012 nikaombewa mpaka sasa nimesahau hata kama niliwahi kuumwa pingili. Huu ni ushuhuda wa kweli kabisa, kabla ya hapo nilikuwa siamini kabisa kama mtu anaweza kuombewa na kupona.
mkuu uliombewa wapi? nisaidie aisee
 
Back
Top Bottom