Maumivu katika magoti | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maumivu katika magoti

Discussion in 'JF Doctor' started by vicent tibaijuka, May 7, 2012.

 1. vicent tibaijuka

  vicent tibaijuka JF-Expert Member

  #1
  May 7, 2012
  Joined: Mar 22, 2012
  Messages: 276
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Nimamua kuandika mada hii kwani nafikiri yaweza kuwa na manufaa kwa watu wengi. Maumivu ya magoti ni( Osteoarthritis) matatizo makubwa kwa watu wengi hasa wazee, wanawake na watu watu wanene. Magonjwa haya husababisha uchumi wa mtu binafisi kuwa mgumu kutokana na kushindwa kufanya kazi kawaida kama ipaswavyo.

  Osteoarthritis ina maana magonjwa ya viungo vya mwili kiujumla, lakini hasa hushambulia magoti na kiuno. Ni ugonjwa wa muda mrefu na kusababisha uharibifu wa cartilage articular (minofu migumu mieupe katka magoti). Ugonjwa huu umekuwa wa kawaida katika watu wengi, lakini katika nchi yetu ni vigumu kusema ni kiasi gani watu wanaathirika, kwani wengi huugua bila dalili na inapofikia hali kuwa ngumu ndo huenda mahospitalini, mabapo pia wataalm ni wachache au vitendea kazi havipo au ni duni hivyo inagua vigumu kungundulika.

  Lakini njia rahisi ya kuugundua ni kupiga x-ray. Sababu kubwa za ugonjwa huu bado hazijulikani, ila ina semakana kuwa ni uzee, wanawake, magonjwa ya kurithi, matokeo ya majeraha ya zamani katika magoti, mabadiliko ya hormoni za estrojen ,unene, uzaifu wa misuli na uchovu uliokithiri hasa kwa wanamichezo, kazi ngumu, hasa za kusimama au kunyanyua vitu vizito.nk. Michezo ya kawaida, kwa kulinganisha, hakuna hatari, ni nzuri sana kwa ajili ya viungo.

  Dalili na uchunguzi
  Utambuzi wa ugonjwa huu hufanywa kwa kuangalia dalili na uchunguzi. Wengi hupenda angalia dalili kwani matokeo ya X-ray hayatosherezi kinaganaga, Maumivu makali yatokanayo na kuzidiwa kwa uzito katika magoti (mafano wakati wa kuismama au kutembea), ndo huwa dalili za mwanzo.

  Hii hutokana na kupungua kwa misuli mieupo iliyopo katika goti, na kufanya nafasi au mwanya kati ya goti kupungua au hata kuwa inasuguana hivyo kusababisha maumivu makali .

  Ukarabati:

  Kwa sasa hakuna tiba kwa ajili ya osteoarthritis, lakini njia kadhaa za kupunguza dalili na kuchelewesha mchakato wa kuendela kukua kwa ugonjwa huu zaweza tumika. Hapo awali watu walitumia madawa ya kupunguza maumivu, lakini leo hii tiba ya msingi ya kufanya mazoezi, na kupunguza uzito. Hii ni kwa kuwa imeonekana kufanya kazi vizuri zaidi ya kutmia vidonge vya kupunguza maumivu, ambayo wengi huwaletema matatizo ya tumbo kama vile vidonda vya tumbo n.k. Mazoezi hunapunguza maumivu, ihuboresha kazi na kuongeza ubora wa maisha katika osteoarthritis, na uchunguzi umeonyesha hakuna athari juu ya mazoezi.

  Mazoezi hayapaswi kuchanganywa na aina yoyote ya shughuli za kimwili, isipokuwa ma zoezi ni vizuri yawe ya kulenga uimara wa viungo vya mwili hasa katika magoti.

  Na vizuri yasiwe ya nguvu kiasi cha kukufanya ukaumia zaidi. Na mara nyingi inachukua muda wa wiki 6-8 wa mazoezi kwa uboreshaji kukuwezesha kuanza kujisikia vizuri. Maumivu yasiwe kikwazo cha kukufanya uache mazoezi bali iwe kichochezi.

  Kumbumbuka mazoezi yasiwe ya nguvu kiasi cha kukufanya ushindwe tembea . mazoezi mazuri ni kuogelea, kuendesha baiskeli, au kukaa ukawa unanyonga miguu kama vile mwendesha baiskeli.

  Kila la kheri.
   
 2. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #2
  May 7, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,134
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Kaka Vicent nashukuru sana kwa mada hii kuhusiana na magonjwa haya yanayotupata hususani wazee wetu, nimeisoma na kuilewa vizuri, ni leo tu nimetoka kuongea na mama yangu mzazi kuhusiana na matatizo haya ambayo yameanza kumnyemelea sasa hivi ni mwezi mmoja tokea aanze kupatwa na matatizo haya, na yeye ni mfanyakazi wa serikalini, kwake yeye ni miguu na vidole kuvimba na kuuma lakini akishatumia dawa kama Diclopa uvimbe hupungua na maumivu kupungua, umesema matatizo haya husababishwa na kusimama muda mrefu, ni kweli kazi yake yeye ni mwalimu natumaini kazi za ualimu unazijua ni kusimama ubaoni kwa muda mrefu, je hizi dawa zinaweza kua na madhara anapozitumia? nimeiprint hii kopy nikampe ili azingatie japo mazoezi. Asante.
   
 3. Kipilipili

  Kipilipili JF-Expert Member

  #3
  May 7, 2012
  Joined: May 25, 2010
  Messages: 2,209
  Likes Received: 483
  Trophy Points: 180
  kaka uzi ni mzuri na naamini kuwa utakuwa umewasaidia wengi. je tatizo hili linatofautianaje na ugonjwa unaoitwa RHEUMATOID ARTHRITIS??? kama unajua tujuze na kama wapo weledi wengine wanaofahamu tujuze kwa ajili ya kujielimisha ili tutakapofika uzeeni tuweze kuyaepuka au kama yatatupata tujuwe namna ya kukabiliana nayo
   
 4. vicent tibaijuka

  vicent tibaijuka JF-Expert Member

  #4
  May 7, 2012
  Joined: Mar 22, 2012
  Messages: 276
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Asante bwana Ndallo.kwa maelezo yako nimekuelewa ,kuwa huvimba miguu na vidole, je ni miguuni tu au hata vidole vya mikononi? kuhusu diclopa ni dawa ya kupunguza uvimbe na maumivu hila aiponyi. na inabidi ainywe baada ya chakula, kwa inaweza kusababisha vidonda vya tumbo au hata kuanza kutoa damu tumboni. ukinielezea kwa zaidi jinsi anavyo umwa na ni wakati gani hasa anapata maumivu naweza kupata jibu la karibu zaidi. vizuri akaangaliwe hosp. mfano wamtoe maji katika hizo joints na kuyaangalia watapata jibu zuri na dwa ya kufaa. mazoezi ni muhimu ili isije ikafikia hatua akashindwa tembea.
   
 5. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #5
  May 7, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  mkuu nimekusoma kazi njema, elimu imeshafika sawasawa
   
 6. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #6
  May 7, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,134
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Vicent asante tena kwaushauri wako! Kuvimba kwake ni miguu pamoja na vidole vya mikononi. Ni ushauri mzuri wacha nimpelekee hayo ya mwanzo uliyoleta hapa,alishakwenda hospital akacheki Presha na magonjwa mengine lakini hawakuona kitu na damu yake ni safi, lakini cha kushangaza mama aliona mpaka watoto wadogo nao wanamatatizo kama yake kweli nimeshtuka sana sijui ni upepo gani umepita, au ni hivi vyakula tunavyokula hususani nyama za ng'ombe nazo sio nzuri sana, kwakua amesema tena akila nyama ya Ng'ombe ndio maumivu yanazidi! Hili la kwenda kutoa maji kwenye joints nalo nitalizingatia.
   
 7. vicent tibaijuka

  vicent tibaijuka JF-Expert Member

  #7
  May 7, 2012
  Joined: Mar 22, 2012
  Messages: 276
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  kama unasema akila nyama ndo yanaongezeka, yawezekana anaugonjwa uitwao gout. sijui huenda hosp za aina gani. na kama watoto pia wanayo inawezekana kwani ugonjwa huu pia ni wa kurithi. lakini pia pia lazima aangalie arthritis. check damu kwa ajiri ya kuangalia gout hasa uric acid. watoto pia wachekiwe kama wana bacterial infection, hata swabs katika makoo lazima watolewe. then jibu litapatikana. aache nyama, wine, pombe kwani kama ni gout hivyo vitu huzidisha. na kama asubuhi akiamuka anaona vidole vimeganda (vimekufa ganzi) ni vizuri kuchunguzwa rheumatism.
   
 8. vicent tibaijuka

  vicent tibaijuka JF-Expert Member

  #8
  May 7, 2012
  Joined: Mar 22, 2012
  Messages: 276
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Rheumatoid arthritis ni tofauti, kwani watu wenye rheumatism mara nyingi hupata maumivu wakati wa baridi na subuhi, hasa wanapoamka. mara nyingi vidole vyao huwa vinakufa ganzi kwa muda wa saa au zaidi ya saa moja. ugonjwa huu husababishwa na autoimmune process. mara nyingi maumivu ni makali katia vidole (metacarpal pharangeal joints), na kama mtu kaugua kwa muda mrefu utaona hata joints zake zimebadilika, zinakuwa na vitu vimevimba kama nundu hivi (nodules). ugonjwa huu wa rheumatism huwaez kusababisha mazra mengine pia kama vile magonjwa ya moyo, mapafu figo na mengineneyo. hivyo ukiwa na mgonjwa heli umpeleke hospital kwa uchunguzi zaidi.
   
 9. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #9
  May 8, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  Dawa ya Maumivu ya Magoti . juici ya Bamia.

  Tayarisha mabamia kama 2 mpaka 4 kwa siku , yakoshe vizuri halafu yakate slice ndogo ndogo. Yatie kwenye jagi na maji safi ambayo Unaweza kupata glass kama tatu za maji kwa muda wa saa hadi masaa mawili. baada ya hapo utapata maji mazito ya urenda uwe unakunywa mara 3 hadi nne kwa siku. tumia hii dawa kisha unipe feedBack. Au tumia Dawa hii

  unapoumwa na kiungo chochote kile: Maji ya moto (sio moto sana ukajiunguza) pamoja na chumvi na taula yako ndogo kujiwekea pale panapouma ikisha ujikaushe maji na utie dawa kama mafuta ya Halzet (Olive Oil) uchanganyishe na

  mafuta ya karafuu kama huna tia hata viksi au dawa zinazotumika za mafupa. kumbuka hujikandi wala hujichui kisha chukua kanga au tambara ujiwekee ili dawa ifanye kazi. Hivi unafanya unapotaka kulala na InshaAllah unaamka maumivu

  yameondoka. Hivi unafanya siku 3 mpaka 7 pindi maumivu yataendelea. Pia kumbuka kwamba kukaa tu husababisha maumivu ya miguu na hata ya mwili kwa hivyo ujitahidi uwe unakwenda kwenda hata kama ndani ya nyumba nenda ukirudi ili upata mazoezi na hii ni dawa kubwa.

  Au tumia hii Dawa Dawa ya viungo inaitwa makerela ambayo yamekaa kama matango lakini kama yana miba miba kwa siku unakula nusu bila kupika, maumivu yote ya viungo yanaondoka. Ni machungu lakini maumivu ya viungo yanaondoka kwa uwezo wake Mwenyeezi Mungu.

  Haya yote husababishwa na ukosefu wa calcium kwa hivyo mwenye kujiona anaumwa sana na magoti, miguu na viungo basi ajitahidi kunywa maziwa, na kula lozi, korosho na kunywa maji kwa wingi na mwenye kuwa hana uwezo wa kupata vitu hivyo basi achemshe mchele na ukiwiva achuje anywe maji yake.


  [​IMG]


  [​IMG]  Tumia hizi dawa kisha unipe feedBack
   
 10. vicent tibaijuka

  vicent tibaijuka JF-Expert Member

  #10
  May 8, 2012
  Joined: Mar 22, 2012
  Messages: 276
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  hiyo bamia ni nzuri kwa kushusha sukari na presuure ya hataua ya kwanzamwilini. kuhusu magoti nitafuatilia. mchango wako mzuri.
   
 11. KakaJambazi

  KakaJambazi JF-Expert Member

  #11
  Jun 21, 2013
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 15,030
  Likes Received: 3,231
  Trophy Points: 280
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 12. D

  Dina JF-Expert Member

  #12
  Jun 21, 2013
  Joined: Sep 18, 2008
  Messages: 2,824
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Nimechelewa sana sana kuiona hii post yako mkuu, lakini bado ni wakati muafaka kwangu. Baada ya kuisoma kwa makini naanza kupata mwanga wa matatizo ya mzee wangu.....nahisi nae anaangukia huku.

  Asante sana mkuu. Kama kumuona daktari anaonwa yeyote au kuna wataalam wake?
   
 13. Sanctus Mtsimbe

  Sanctus Mtsimbe Tanzanite Member

  #13
  Jun 21, 2013
  Joined: Jul 14, 2008
  Messages: 1,815
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Pia kuna hii kama inaweza kusaidia. Ipo Kimombo ila juice au tunda la Apple na Ndimu ndo mpango mzima: Mafanikio Na Afya Njema: Je Una Maumivi Ya Gouts (Viungo)? - Home Remedies for Gout


   
 14. A

  Amantogoyoka Member

  #14
  Aug 4, 2015
  Joined: Jul 9, 2015
  Messages: 31
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 15
  Hello wanajamii,
  Naomba ushauri kama kuna mtu yeyote ambaye amewahi kupata shida kama hii niliyonayo leo, au anyejua dawa, kwa muda wa wiki moja sasa nasikia maumivu makali sana kwenye goti langu la mguu wa kulia kiasi cha kushindwa kuinua mguu ili kutembea siwezi hata kuchuchumaa.
  Hii ni mara ya tatu kupata maumivu kama haya kisha yanapotea baada ya siku 2 bila dawa yoyote lakini sasa ni wiki imekwisha sijapata nafuu yoyote, asanteni sana.
   
 15. Cataliyya

  Cataliyya JF-Expert Member

  #15
  Aug 4, 2015
  Joined: Feb 12, 2015
  Messages: 509
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 60
  Kama kuna mtu anaumwa gaut humu ndani dawa ninayo ni ya mitishamba ila ipo in form of capsules inapatikana kwa 80,000. Kama unaitaji nichek kwa namba 0719 252523
   
 16. A

  Amantogoyoka Member

  #16
  Aug 4, 2015
  Joined: Jul 9, 2015
  Messages: 31
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 15
  Asante sana mkuu kwa ushauri ntajitahidi kuufuata lakini kwa sasa nina maumivu makali sana siwezi kuanza kufanya mazoezi mpaka pale ntakapo pata nafuu.
   
 17. Dola Iddy

  Dola Iddy JF-Expert Member

  #17
  Aug 22, 2015
  Joined: Sep 26, 2014
  Messages: 1,734
  Likes Received: 899
  Trophy Points: 280
  Habari za wakati huu ndugu zangu wapendwa!, Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 23 , kazi yangu ni mchezaji wa mpira wa miguu,
  Nakumbuka mnamo mwezi MARCH nilikuwa katika mechi ya kirafiki nikiwa napeleka mashambulizi katika lango la timu pinzani ndipo beki akawa anakuja kublock mbio zangu ile anakuja kuupiga mpira ili utoke nje nikaruka ili kumkwepa asiniumize ile natua chini nikapata mshituko kwenye jointi ya goti na kunipelekea kutolewa nje ya uwanja na kupakwa dawa ya kuchua lakini haikusaidia ,
  Nikakaa toka mwezi MARCH mpaka JULY nikiwa ma maumivu ya goti pindi ninapoanza kucheza mpira ila kama nikitembea au kufanya shughuli yoyote ile sihisi maumivu yoyote,
  Mnamo JULY katikati nikaamua kwenda kwenye duka maarufu sana hapa ushirombo bukombe lijulikanalo kama KADAMA PHARMACY nikamueleza daktari tatizo langu akanipatia dawa ya kuchua na vidonge vya kumeza kwa maelekezo kuwa nitameza kidonge kimoja asubuhi na kidonge kimoja usiku kwa kila dozi na kupaka dawa ya kuchua asubuhi, mchana na usiku,

  Nilitumia dawa kama nilivyoelekezwa nikapata nafuu ila nilipoanza tena mazoezi maumivu yakaanza tena hivyo mpaka sasa hivi sijatumia dawa yoyote ndo nikaona bora nipite humu nipate ushauri wenu ndo nifate taratibu za matibabu. AHSANTENI.
   
 18. Coke Zero

  Coke Zero JF-Expert Member

  #18
  Aug 22, 2015
  Joined: Mar 30, 2015
  Messages: 1,033
  Likes Received: 284
  Trophy Points: 180
  A.Nadhani umeptata kati ya yafuatayo

  1.ligaments sprains

  2.muscles sprains

  3.Mild joint dislocation/Angulation

  4.Rupture of tendons around the knee joint.

  5.A mild fracture ambayo bado haijapona


  B.NAKUSHAURI:

  1.Kapige x-ray au ultrasound utajua tatzo lako pamoja na matibabu yanayotakiwa!

  C.ANGALIZO

  1.Dawa za kuchuwa ni kwaajili ya maumivu hazisaidii kidonda au mfupa kupona
   
 19. Dola Iddy

  Dola Iddy JF-Expert Member

  #19
  Aug 23, 2015
  Joined: Sep 26, 2014
  Messages: 1,734
  Likes Received: 899
  Trophy Points: 280
  mkuu nashukuru sana kwa ushauri wako ila naomba japo uniambie dawa ambayo angalau itanipunguzia maumivu na kulirejesha goti langu katika hali yake ya awali.
   
 20. Woolf Cruse G

  Woolf Cruse G Member

  #20
  Oct 12, 2015
  Joined: Apr 12, 2015
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Nina matatizo kwenye JOINT za miguu, ule uteute umepungua hali inayonipelekea kushindwa hata kuchuchumaa vizuri au kupiga magoti, wakati mwingine miguu huniuma sana pindi napotembea umbali mrefu .

  Naombeni msaada nitumie dawa gani?
   
Loading...