GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 59,949
- 119,214
Nasikitika sana kuwa mpaka sasa hivi hakuna Chombo " maalum " cha kuwasimamia na kuchunguza maadili ya hawa Watangazaji wetu wa redio na luninga hapa nchini Tanzania kwani ama hakika kwa tunachokishuhudia sasa ni " ujinga " kama siyo " upumbavu " hasa katika utangazaji.
Sijui ni SIFA zimeshamlevya au ni UTOTO unamsumbua au ni USHAMBA umemzidi au ni MASHAUZI yaliyopitiliza kwani kusema ukweli ukimsikiliza Maulid Kitenge wa sasa aliyepo E fm unaweza usiamini kuwa ni yule yule Maulid Kitenge ambaye alikuwepo Radio One / ITV miaka ya nyuma.
Maulid Kitenge kwanza tambua kuwa audince wako ni very segmented hivyo basi unatakiwa nawe kuwa neutral hasa katika aina yako ya Utangazaji ili uweze kuwabeba wote lakini nisikufiche " Kijana " kwa jinsi unavyotangaza sasa ninaamini kuna kundi fulani la Watu ambalo kweli ni Wapenzi wa Michezo lakini unawaondoa.
Mapungufu yako makuu ni haya:
Tambua kuwa nia yangu siyo KUKUCHAFUA au KUKUUMBUA bali ni jambo baya sana kama Mtu ambaye ni MWELEDI wa FANI husika na UMETUKUKA nayo halafu unaona UDHAIFU fulani unafanywa kila kukicha na Mtu ambaye unamuheshimu na unamkubali halafu unanyamaza na humkosoi ili kumjenga zaidi.
Napenda mno bidii yako KIUTANGAZAJI ila tumia huu UZI wangu kama sehemu yako ya KUJISAHIHISHA ila nikiri kwako na nisiwe MNAFIKI au mchoyo wa SHUKRANI au hizi SIFA kwako kuwa hadi hivi sasa hapa Tanzania bado sijaona MTANGAZAJI WA MICHEZO anayekushinda au hata tu kukufikia na labda nikuambie tu Wewe una KIPAJI kitu ambacho wenzako wengi hawana na hao wenzio wengi wana ELIMU tu hivyo kwa hicho kipaji ulichonacho ukienda kupata elimu bora ya utangazaji nakuhakikishia " utawaburuza " hawa Watangazaji wenzio hadi waombe " po " kwako.
Natumai utayapokea haya na hutaninunia au kuiona ID hii ni " chungu " kwako. Akhsante.

- Umezidisha mzaha uwapo hewani.
- Unaleta uhuni huni wa mtaani redioni.
- Unaanzisha mizozo ya kipuuzi isiyo na tija hasa kiueledi.
- Kuna muda sauti yako au kauli zako uzitoazo tena hewani ni kama za wale ambao RC Makonda anawatafuta kwa " udi na uvumba " kuwakamata hapa mjini.
- Huyo Mtangazaji wa Kike Tunu Hassana Shemkome ambaye namfahamu kimaadili tokea akiwa Radio Uhuru tokea atue hapo umemfanya nae akuige Wewe kwa hayo madhaifu yako na sasa huyu Binti nae amekuwa " mswahili " hadi kila Mtu ameshikwa na " butwaa ".
- Uko very biased hasa katika Habari zako ambazo zina upendeleo ulio wazi kitu ambacho professionally ni hatari sana.
- Una UNAFIKI wa KITAALUMA.