Maulid Kitenge wa E-Fm huo uufanyao sasa siyo Utangazaji bali ni uswahili!

wewe huwa una chuki binafsi..

Yawezekana hata siku nyingine kwa mfano ikitokea pengine namsema " Mamaako " humu utasema labda " natembea " nae. You're very FOOLISH. Halafu acha kutumia ID zenye majina ya Watani zangu ninaoheshimiana nao WAHAYA kwani kwa WAHAYA ninaowajua Mimi hawana " JUHA " wa aina yako.
 
mkuu hata kama umeandika unafiki kwa jinsi ulivyopangilia kazi yako unastahili pongezi, nimejaribu kuirudia kwa burudani kabisa ia naona yete yanaweza kufupishwa kuwa sentesi labda tatu


" labda nikuambie tu Wewe una KIPAJI kitu ambacho wenzako wengi hawana na hao wenzio wengi wana ELIMU tu hivyo kwa hicho kipaji ulichonacho ukienda kupata elimu bora ya utangazaji nakuhakikishia " utawaburuza " hawa Watangazaji wenzio hadi waombe " po " kwako."

au nusu sentensi kwa kusema +++ kitenge wewe ni qilaza+++

Haya maoni yako ungeyaanzishia UZI ningekuona GREAT THINKER ila sasa NIMEKUDHARAU KUNAKOTUKUKA.
 
Mkuu acheni kuandama watu Watanzania tuna mambo ya msingi ya kufuatilia lakini muda huo wa kusema watu na kuanzisha thread mnautoa wapi? Au ww ni mtangazaji mwenzie kwenye Redio ya Jirani pale
Acheni hizo habari

Kwahiyo kwako Wewe kuufuatilia mwenendo wa KIUTANGAZAJI wa Maulid Kitenge siyo jambo la msingi? Kwahiyo kwako Wewe jambo la msingi labda ni kwenda msalani kutoa " haja kubwa " yako au? Kuna Watu wengine huwa MNANILAZIMISHA NIWADHARAU kwa ujengaji wa HOJA zenu ambazo ni za " hovyo hovyo " kama mlivyo.

Hivi unajua IMPACT ya utangazaji wake kwa AUDIENCE bila kusahau Watu wanaotaka kuwa kama yeye? Hivi unajua kuwa huu muda nilioupoteza " kumfunda " hapa nimemjenga kiasi gani kama akifuata ushauri ukosoaji na ushauri wangu kwake?

Aliyekuambia kuwa eti ukiwa unamkosoa Mtu basi ni lazima uwe unafanya Kazi kama yake au una Wivu nae ni nani? Kwahiyo kwa mfano Watu tunavyomkosoa Rais wetu inamaanisha sisi wote huwa tunautaka huo Urais wake au tuna Wivu nae?

Namshukuru Mwenyezi Mungu sikuzaliwa " mbumbumbu " kama ulivyo Wewe na labda ni nikushauri kuwa siku nyingine ukiiona ID hii halafu unataka kujibizana nayo basi hakikisha kwanza " upstairs " umekamilika vilivyo kutokana kwamba majibu ya kuwajibu " wapuuzi " wa aina yako huwa hayako mbali.
 
Siku hizi nitajitahidi kuwa makini na thread zako manake nimegundua zingine unazileta ama kuwapa watu promo au kuchimbachimba kwa mambo yako binafsi! Si ni wewe ambae uliwahi kuleta thread kuulizia kuhusu Tunu Hassan?! Au ulitaka watu wafunguke kwa mapana na marefu; kwamba anamegwa na fulani ili halafu ukaanzishe mtiti endapo huyo fulani sio wewe?!

Nashukuru kujua kuwa kumbe na Wewe ni mmoja wa " FOLLOWERS " wangu waliotukuka humu JF safi sana Mkuu na endelea kunifuatilia kwani hapa ndiyo kwenye KISIMA cha kila kitu unachokitaka.
 
Ungeweka basi na ushahidi hata wa voice clip ya hayo makosa yake

Intellectually kuna njia mbili za kuthibitisha kitu au jambo fulani ambapo unaweza ukaweka uthibitisho wa kimaandishi wa makosa au ukaweka ya sauti na Mimi nimechagua kuweka madhaifu yake kimaandishi ambayo yapo hapo katika UZI wangu sasa nashangaa tena kusikia unaniambia nikuwekee ushahidi wa sauti kitu ambacho kimenifanya nishtuke kidogo kama aliyeandika hii kitu ni graduate kabisa au mtarajiwa wa kumaliza standard seven baadae mwaka huu.
 
Hicho kiredio hakifiki huku kwetu, wanasikiliza wanaume wa dar tu
Kama mnaoishi huko Dar es Salaam ni aibu kuleta hoja kama hii hapa jukwaani.
Mnatusakama tunaoishi Dar, lakini cha ajabu ni kwamba mkifika tu huku mnaanza kuwatafuta akina Kitenge mpige nao picha, au majengo wanayofanyia kazi msimame mpige picha
 
Hii thread ni ya kupuzwaa ipo kwa ajili ya kupotosha jamii

Hakuna ninachokileta humu kisipokelewe au kupendwa au kukubalika na Members Mkuu. NYOTA niliyonayo ni JAHA ambayo huwezi kuuzima muda na wakati wowote ule sana sana kila siku utabaki tu kunichukia humu au kunionea Wivu lakini mwenzako nazidi tu " kupaa ". Njoo nikupe maujuzi ya Wewe pia kukubalika na kung'aa kwani yawezekana una NYOTA ya BUNDI ambayo kila saa inakufanya uwe hapo hapo huku CHUKI na WIVU ukikujaa tu kwa Watu ambao tulishabarikiwa na Mwenyezi Mungu tokea tuko " tumboni ".
 
Nasikitika sana kuwa mpaka sasa hivi hakuna Chombo " maalum " cha kuwasimamia na kuchunguza maadili ya hawa Watangazaji wetu wa redio na luninga hapa nchini Tanzania kwani ama hakika kwa tunachokishuhudia sasa ni " ujinga " kama siyo " upumbavu " hasa katika utangazaji.

Sijui ni SIFA zimeshamlevya au ni UTOTO unamsumbua au ni USHAMBA umemzidi au ni MASHAUZI yaliyopitiliza kwani kusema ukweli ukimsikiliza Maulid Kitenge wa sasa aliyepo E fm unaweza usiamini kuwa ni yule yule Maulid Kitenge ambaye alikuwepo Radio One / ITV miaka ya nyuma.

Maulid Kitenge kwanza tambua kuwa audince wako ni very segmented hivyo basi unatakiwa nawe kuwa neutral hasa katika aina yako ya Utangazaji ili uweze kuwabeba wote lakini nisikufiche " Kijana " kwa jinsi unavyotangaza sasa ninaamini kuna kundi fulani la Watu ambalo kweli ni Wapenzi wa Michezo lakini unawaondoa.

Mapungufu yako makuu ni haya:

  1. Umezidisha mzaha uwapo hewani.
  2. Unaleta uhuni huni wa mtaani redioni.
  3. Unaanzisha mizozo ya kipuuzi isiyo na tija hasa kiueledi.
  4. Kuna muda sauti yako au kauli zako uzitoazo tena hewani ni kama za wale ambao RC Makonda anawatafuta kwa " udi na uvumba " kuwakamata hapa mjini.
  5. Huyo Mtangazaji wa Kike Tunu Hassana Shemkome ambaye namfahamu kimaadili tokea akiwa Radio Uhuru tokea atue hapo umemfanya nae akuige Wewe kwa hayo madhaifu yako na sasa huyu Binti nae amekuwa " mswahili " hadi kila Mtu ameshikwa na " butwaa ".
  6. Uko very biased hasa katika Habari zako ambazo zina upendeleo ulio wazi kitu ambacho professionally ni hatari sana.
  7. Una UNAFIKI wa KITAALUMA.
Naomba nikushauri tu kuwa unaweza kwa sasa labda ukaona umeshamaliza kila kitu ila kwa kukusaidia tu naomba kama hutojali hebu rudi tena Shule ukapikwe zaidi kwani nina uhakika wa kiushahidi kabisa huna ELIMU stahili ya Journalism and Broadscasting zaidi tu ya " ujanja ujanja " wa hapa na pale na kule kunolewa kwano na Mentors wako akina Abdallah Majura na Charles Hillary na kama umesoma sana basi una Basic Certificate tu ya hiyo FANI na UZOEFU ndiyo unakubeba ila kielimu najua hata huyo Bibie Tunu Hassan Shemkome amekuzidi kwani yeye sasa ana ADVANCE DIPLOMA YA JOURNALISM ya Dar es Salaam School of Journalism ( DSJ ).

Tambua kuwa nia yangu siyo KUKUCHAFUA au KUKUUMBUA bali ni jambo baya sana kama Mtu ambaye ni MWELEDI wa FANI husika na UMETUKUKA nayo halafu unaona UDHAIFU fulani unafanywa kila kukicha na Mtu ambaye unamuheshimu na unamkubali halafu unanyamaza na humkosoi ili kumjenga zaidi.

Napenda mno bidii yako KIUTANGAZAJI ila tumia huu UZI wangu kama sehemu yako ya KUJISAHIHISHA ila nikiri kwako na nisiwe MNAFIKI au mchoyo wa SHUKRANI au hizi SIFA kwako kuwa hadi hivi sasa hapa Tanzania bado sijaona MTANGAZAJI WA MICHEZO anayekushinda au hata tu kukufikia na labda nikuambie tu Wewe una KIPAJI kitu ambacho wenzako wengi hawana na hao wenzio wengi wana ELIMU tu hivyo kwa hicho kipaji ulichonacho ukienda kupata elimu bora ya utangazaji nakuhakikishia " utawaburuza " hawa Watangazaji wenzio hadi waombe " po " kwako.

Natumai utayapokea haya na hutaninunia au kuiona ID hii ni " chungu " kwako. Akhsante.
Ungemsaidia zaidi kama hii kitu ungemtupia kwa 'PM'
 
mkuu usiwe mkali shida nini! kitenge anakuburuza kwenye fani, msubiri chini faza yule pumzi itakata.
wakati unamsubiri nenda tot ukaimbe taarab tar 23.

Niliyoyafanyia nchi hii hadi sasa hasa katika nafasi nilizopitia na majukumu niliyoyafanya ni makubwa ambapo sidhani hata kama huyo Kitenge ameyafikia au atathubutu kuyafikia. Halafu sidhani pia kama hata CV yangu tu inatosha kunifanya Mimi nipeane nae mikono na ndiyo maana umeona nimeamua tu kumfunda huku ili WASHIRIKA wake kama Wewe mumfikishie hii taarifa.

Laiti ungeniambia kuwa nawaonea WIVU Watu kama hawa wafuatao kweli ningekukubalia wazi wazi:

  1. Dr. Ayub Rioba
  2. Dr. Hamza Mponda
  3. Professor Fr. White
  4. Dr. Bishop Bernadin Mfumbusa
  5. Dr. Fr. Charles Kitima
Hao nadhani ndiyo kila siku nawaone WIVU nijitahidi ili niweze kuwafikia kwani napenda mno UWEZO WAO MKUBWA wa KUFIKIRI ambao nakiri bado sijawafikia ila kuniambia namuonea " gere " Maulid Kitenge nadhani utakuwa unanikosea kwa kiwango kikubwa mno.
 
Mnatusakama tunaoishi Dar, lakini cha ajabu ni kwamba mkifika tu huku mnaanza kuwatafuta akina Kitenge mpige nao picha, au majengo wanayofanyia kazi msimame mpige picha
Kama wanaopiga picha serengeti au mikumi wakiwa na wanyamapori, si ndio eh!
 
Duu nilijisahau kwasababu mimi nina ID Yake nikahisi nawewe unayo, ebana ngoja tuishie hapahapa maadamu umemwaga choo hadharani nayeye amesoma tayali

Hata Mimi naona Mkuu bora tu tuishie hapa hapa kwani huko mbele nadhani " tungenuniana " tu bure kupitia ID zetu japo hatujuani kwa " minyago " yetu halisi.
 
Niliyoyafanyia nchi hii hadi sasa hasa katika nafasi nilizopitia na majukumu niliyoyafanya ni makubwa ambapo sidhani hata kama huyo Kitenge ameyafikia au atathubutu kuyafikia. Halafu sidhani pia kama hata CV yangu tu inatosha kunifanya Mimi nipeane nae mikono na ndiyo maana umeona nimeamua tu kumfunda huku ili WASHIRIKA wake kama Wewe mumfikishie hii taarifa.

Laiti ungeniambia kuwa nawaonea WIVU Watu kama hawa wafuatao kweli ningekukubalia wazi wazi:

  1. Dr. Ayub Rioba
  2. Dr. Hamza Mponda
  3. Professor Fr. White
  4. Dr. Bishop Bernadin Mfumbusa
  5. Dr. Fr. Charles Kitima
Hao nadhani ndiyo kila siku nawaone WIVU nijitahidi ili niweze kuwafikia kwani napenda mno UWEZO WAO MKUBWA wa KUFIKIRI ambao nakiri bado sijawafikia ila kuniambia namuonea " gere " Maulid Kitenge nadhani utakuwa unanikosea kwa kiwango kikubwa mno.
mkuu hata unavyoandika unaonekana umepita uwezo wetu wakawaida wa kufikiri natumaini utafika unapolenga, siku moja
 
Nakumbuka ilipoanzishwa Radio One wakti ule na Maulid Kitenge alianza kunipa wasiwasi kwenye kipindi cha michezo alipokishika.

Nafikiri kulikuwa na "kushikwa mguu" sana kwa huyu jamaa mbona wenzake alioanza nao wapo mbali sana?
 
Nashukuru kujua kuwa kumbe na Wewe ni mmoja wa " FOLLOWERS " wangu waliotukuka humu JF safi sana Mkuu na endelea kunifuatilia kwani hapa ndiyo kwenye KISIMA cha kila kitu unachokitaka.
Sijasema mimi ni FOLLOWER wako!! Watu si huwa mnaanzisha threads hapa jamvini? Na mkianzisha lengo lenu si ni kwamba wengine tusome? Sasa sisi wengine tukisoma huwa hatusahau mada wala jina la mleta mada hata kama muda umepita!
 
Nakumbuka ilipoanzishwa Radio One wakti ule na Maulid Kitenge alianza kunipa wasiwasi kwenye kipindi cha michezo alipokishika.

Nafikiri kulikuwa na "kushikwa mguu" sana kwa huyu jamaa mbona wenzake alioanza nao wapo mbali sana?

Aliokotwa tu pale Uwanja wa Taifa maeneo ya kwa " Mama Chichi " akiwa anabwabwaja bwabwaja tu masuala ya mpira na yule Kijana mwenzie aitwae " Kambarage " ambaye mpaka sasa yupo pale na akifanya tu Kazi za kulinda magari ya Watu wanaokunywa Bia au wanaokuja kuangalia mechi za VPL na za Kimataifa Uwanja wa Taifa ila zamani uhondo wote huu ulikuwa pale Uwanja wa Uhuru a.k.a Shamba la Bibi.

Watu waliomuibua Maulid Kitenge walikuwa ni Watangazaji akina Charles Nkwanga Hillary na mwenzie Abdallah Idrisa Majura ambapo kipindi walipokuwa Watangazaji wa michezo hasa hasa mpira wa Miguu wakiwa na RTD walikuwa wakimwona mno Maulid Kitenge pale Taifa akiwa anabishana na Watu kuhusu mpira huku akionekana ni mjuaji mzuri wa masuala ya " Kandanda " hivyo basi Watangazaji wawili hawa walipoahamia tu Radio One / ITV miaka ya 1993 hadi 1994 wakiwa na akina Mama Faudhiat Abood waliamua kumchukua Maulid Kitenge na kuanza kumpa ujuzi pale pale Radio One huku akiwa bado hajapewa vipindi lakini wakati huo huo Maulid akiwa ndiyo kamaliza Form Four yake ambapo kwa Heshima kubwa niliyo nayo juu yake sipo tayari kusema alipata ALAMA gani na itabaki kuwa SIRI yangu na kwa wale wanayoijua.

Hata hivyo baadae alipoonekana sasa ameiva ndipo Mzee Mzima Charles Hillary akamtambulisha rasmi katika Utangazaji na hapo ndipo nyota ya Maulid Kitenge ikaanza kung'aa hadi alipoanza kuteka mioyo ya Watu na kukubalika hasa kwa aina yake ya Utangazaji na Interviews zake ambazo kiukweli kama hukujiandaa vizuri unaweza ukaomba ardhi ipasuke uzame tu upotee.

Basi baada ya hapo ndipo Kijana wa Watu akazidi kuimarika na kuwa tishio hata kwa wale Watangazaji wasomi huku akipata bahati ya kupendwa na wenye kujua kupenda na mwenzetu sasa kabarikiwa hivyo ana nyumba mbili ambazo zote zina uhakika ( namaanisha hajaoa magubegube kama wengi wetu ) na ambapo amebahatika pia kuwa exposed katika dunia nyingine ambako sasa anaweza kusafiri kwenda " mamtoni " ambako wengi wetu tunaishia tu kupaona katika BBC Habari kila siku Saa 3 usiku huku wengine tukiishia tu kupaota na tukiamka tunajikuta tupo pale pale uwanja wa Fisi.

Hata hivyo yawezekana ubora wake umeongezeka maradufu kutokana na kwamba hata Wake zake alionao nao ni Wana Habari na Watangazaji maarufu hivyo kuna namna nao walivyomjenga hadi baadae Redio ya E fm ilipoanzishwa basi Kijana wa Watu akaonekana na kupewa dili ya maana na hatimaye kuamua kuachana rasmi na Radio One / ITV ambapo sasa ndiyo amekuwa Bosi wa Sports Desk / Department pale E fm.

Ni Kijana ambaye kama akijiendeleza hasa Kimasomo na kimaadili ya Kazi ya Habari na Utangazaji nina uhakika Tanzania ipo siku tutakuja kujivunia na Kazi zake kwani katika Tasnia nzima ya Habari na Utangazaji kuwapata akina Maulid Kitenge kumi ( 10 ) unaweza " ukasota " hata miaka 25 usiwapate kwani ana vitu adimu ambavyo kwa Watangazaji wengine havipo na hata vikiwepo basi ni full artificial.

Naomba niishie hapa tafadhali.
 
Back
Top Bottom