Maudhui ya shairi la wanafunzi yamchefua DC

Maudhui ya shairi la wanafunzi yamchefua DC

Zak Malang

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2008
Posts
5,404
Reaction score
242
Maudhui ya shairi la wanafunzi yamchefua DC

Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Henry Clemens, juzi aligeuka mbogo baada ya kukasirishwa na shairi lililoimbwa na wahitimu watarajiwa wa Kidato cha Nne katika Shule ya sekondari ya Kata ya Kiparanganda.

Maudhui ya shairi yalikuwa yanaeleza manunguniko yao dhidi ya serikali kutokana na matatizo kibao yanayozikabili shule za kata ikiwemo ukosefu wa walimu huku wakidai kwamba walengwa wa shule hizo ni watoto wa walalahoi.

Wahitimu hao katika mashairi yao walidai kuwa matatizo mengi yanayozikabili shule za kata yanachangia wengi wao kufeli na kujikuta wakiishia mitaani wakikosa kazi za kufanya huku watoto wa vigogo wakiendelea kuneemeka na elimu bora wanayoipata kutokana na wazazi wao kuwa na uwezo.

Baadhi ya maneno yaliyopo kwnye mashairi hayo yanasema :shule za kata wamejengewa masikini, watoto wa wakubwa hawaonekani, maisha mitaani magumu, wanafunzi wanafeli, nyumba za kupanga, wengi wanakatisha masomo yao, wazazi wengi masikini, hakuna walimu tabu nyingi wanapata mitaani, wazazi hawana uwezo wanategemea mashamba. Serikali itupe suluhisho la matatizo haya.

Baada ya wanafunzi hao kumaliza mashairi yao, Mkuu wa huyo wa Wilaya aliwageukia wazazi wao na kuwaonya kutohusisha ujenzi wa shule hizo na masuala ya kisiasa.

Pia aliwataka waache tabia ya kukumbatia umasikini wakati wana uwezo wa kuwasomesha watoto wao.

kuna matatizo ya hapa na pale lakini motto akianza kutembea anatambaa ndiyo hatua ya kwanza. Jitihada za serikali kujenga shule za sekondari Mkuranga ni tofauti na maeneo mengine hapa nchini kulikuwa na shule za sekondari nne lakini hadi sasa zipo 22, ni sawa na ongezeko la asilimia 450, maeneo mengine hayana asilimia hiyo licha ya halmashauyri nyingine kuwa na umri wa miaka 100, tusiulize serikali iko wapi, tuseme serikali ijitahidi kuongeza ubiora wa shule, alisema Mkuu wa Wilaya..

Aliongeza: Serikali ipo na kama isingekuwepo msingepata nguvu za kusema maneno hayo.

Alisema hakubaliani na waliosoma mashairi hayo na kuwataka wanafunzi hao wasome na kwenda kuwasaidia wazazi wao..

Mimi mbona nilisoma shule za kimasikini na hadi sasa nina digrii zangu mbili na nataka nikaongeze nyingine, na wale wanaotaka kuwa na watoto wa wakubwa nitawapeleka Masaki mkakae nao, msikae kuukumbatia umasikini, shule za kata zimejengwa kwa ajili ya wananchi wote na siyo kuwalenga watoito wa kimasikini, umasikini ni wa kujitakia hata ukiwa tajiri huwezi kukamilika kwa kila kitu. Shida yenu ni kupata elimu au kusoma na watoto wa wakubwa? alisema na kuhoji na kuwataka waachane na mambo ya siasa kwa kuwa hayana mwisho.


Chanzo: Nipashe
 
Kwanza niwapongeze sana hao watoto kwa shairi makini. Inapendeza kuona kwamba vijana wa kidato cha nne tayari wameshajanjaruka na wapo tayari kutetea haki zao za msingi. Na pili nimpe pole huyo mkuu wa wilaya kwa kuwa imemuuma kuambiwa ukweli. Siku zote ukweli unauma. Na huo ndo ukweli kwamba shule za kata ni kwa ajili ya masikini. Kama aliona kwamba shairi hilo ni la uongo basi angeeleza mtoto wake anasoma wapi? Mkuu wa wilaya pia hakujibu hoja ya upungufu wa walimu na ukosefu wa hostel na kupelekea watoto kupanga mitaani.

Hakuna mtu hata mmoja mwenye uwezo wake atakayekubali kupeleka mtoto kwenye shule ya kata ili hali anajua kwamba uwezekano wa kupata elimu ya maana ni mdogo. Lakini iwe na itakavyokuwa, ujumbe umefika.
 
Watoto wanataka madawati,walimu na maabara nzuri..sio takwimu zisizo na mpango..!
 
Nilihudhuria mahafali kama hiyo pale Eagles Bagamoyo wao wanachoomba ni standby generator umeme wa TANESCO ukikatika wasipate shida, computer nyingi na mtandao wa internet wa uhakika, maabara za kisasa zaidi,.... ndani ya Tanzania hii moja!
 
Kazi yao kuchakachua tu mambo muhimu wakiambiwa ukweli wanakimbilia kusema ni siasa. Mbona huyo DC hatumii baiskeli? Gari yake inazidi thamani ya shule aibu.
 
Ni bahati mbaya sana viongozi wengi wa serikali hutumia mamlaka na madaraka kujibu maswali magumu badala ya kujenga hoja! Amenikumbusha yule mgombea ubunge wa jimbo la Ubungo ambaye alitishia kumpeleka mtu mahakamani kisa kaulizwa swali lililomkera!
 
Yeye yuko mkuranga watoto wake wanasoma wapi?....hapo Kiparang'anda?...sidhani...ndio maana kaudhika...hataki watoto wake wachanganyike na wa wengine...MIMI NIMESOMA NA ROSEMARY NYERERE....
 
UKWELI UNAUMA. HATA YEYE MWENYEWE (MKUU WA WILAYA) ANAJUA HAYO APUNGUFU. ANACHOFANYA NI KUYAFUMBIA MACHO.
WANAFUNZI WAMESEMA "Serikali itupe suluhisho la matatizo haya". Yeye anajibu " kuwaonya kutohusisha ujenzi wa shule hizo na masuala ya kisiasa".

HAO (CCM) WAMEISHIWA SERA
 
kutoka shule 4 hadi 22! ongezeko la 450% na walimu wameongezwa %ngapi? si ni siasa hizo!
 
kutoka shule 4 hadi 22! ongezeko la 450% na walimu wameongezwa %ngapi? si ni siasa hizo!

Walimu nao wanakimbia kufundisha mwalimu anapangiwa shule mshahara anapata kwa mbinde eti jina halijaingia kwenye computer wanaamua kukacha kufundisha.
 
kutoka shule 4 hadi 22! ongezeko la 450% na walimu wameongezwa %ngapi? si ni siasa hizo!

Kuna mtu anataka kkuwa mwalimu sku hizi?, enzi za Mwalimu kuwa mwalimu ilikuwa kazi ya maana sana ktk jamii. lakini ss hv mwalimu ni mtu wa kudharauliwa sana, mwanao akishindwa mipango yote ndy unampeleka ualimu! wanasiasa wanashinda kutukana taaluma za wenzao!!!! Kaaz kwelikweli!
 
:clap2::clap2: bravoooo bravoooooooooo wametunga shairi zuri sana yaani hii in INDIRECT KICK :A S thumbs_up:
 
Tangu siku ya kwanza nilipoingia form I, Chemistry, Physics na Biology nilikuwa nikisoma nikiwa Labaratory. Huwa najiuliza, hivi nikialikwa nikatoe mada ya Chemistry kwenye shule hizi nitafanyaje? Sana sana najua nitaishia kuitwa mbabaishaji, kwa sababu nitashindwa 'kubabaisha' kwa kukosa vitendeakazi!.......
 
kutoka shule 4 hadi 22! ongezeko la 450% na walimu wameongezwa %ngapi? si ni siasa hizo!

Katika zote nimeipenda hii, halafu akaongeza hiyo asilimia ni rekodi, kuna halmashauri zina miaka 100 hazijafikia hapo. Hivi huyu DC mzima kweli?
 
Nakumbuka kuna mtoto mmoja wa shule alimuuliza swali waziri mkuu(wakati huo Lowasa) "kwanini viongozi wanarundikiwa vyeo? huyo huyo mkuu wa mkoa, huyo huyo mbunge..."
Lowasa alichukia sana.
Nchi hii ukitaka kukorofishana na viongozi basi zungumza ukweli tu.
 
Kazi yao kuchakachua tu mambo muhimu wakiambiwa ukweli wanakimbilia kusema ni siasa. Mbona huyo DC hatumii baiskeli? Gari yake inazidi thamani ya shule aibu.

Watoto wamenena na CCM na Serikali hawana njia bali kuhakikisha Shule hizi za kata zinakuwa na ubora unaohitajika. Hili linawezekana bila tatizo na liko ndani ya uwezo wetu kama nchi. Tuwe wakweli.
 
Mimi ni mtoto wa masikini lakini secondary nimesoma na mtoto wa Aboud Jumbe akiwa rais Zanzibar na watoto wa mawaziri kadhaa ENZI hizo kama Kuhanga,Mgonja,Maswanya nk.Hebu ajitokeze mlala hoi anayesoma hizi shule za yeboyebo na watoto kama hao kwa sasa.Tunataka Tanzania moja elimu moja
 
Kazi yao kuchakachua tu mambo muhimu wakiambiwa ukweli wanakimbilia kusema ni siasa. Mbona huyo DC hatumii baiskeli? Gari yake inazidi thamani ya shule aibu.

Hivyo DC ni kifupisho cha nini???? Drunk Clown au????
 
Ni bahati mbaya sana viongozi wengi wa serikali hutumia mamlaka na madaraka kujibu maswali magumu badala ya kujenga hoja! Amenikumbusha yule mgombea ubunge wa jimbo la Ubungo ambaye alitishia kumpeleka mtu mahakamani kisa kaulizwa swali lililomkera!

Mkuu, mimi ninasikia tu kuhusu huyu mgombea kukasirishwa na swali aliloulizwa. Hivi aliulizwa nini na kujibu nini? siku hiyo mi sikuweza kuangalia hicho kipindi.
 
Back
Top Bottom