Mauaji ya Mzee Karume: Acha sasa tuhoji yasiyohojika!

Abeid Karume aliuliwa na Wa Zanzibari kwa umoja wao. Ni tukio lilo pangwa na timu kabambe walo choshwa na
Uonevu
Ubakaji yaani raping
Njaa
Ubaguzi
Mauaji
Uchumi mbovu
Ufisadi
Na wizi ndani ya SMZ
Walopangwa kufanya hujuma na sunna hio ni Vidume Vitano
Alikuwepo Mwafrika wa Bara - Ali Khatib Chwaya
Alikuwepo Mwarabu wa asili ya Oman - Lt. Humud Mohamed
Alikuwepo Mshirazi Capt. Ahmada
Alikuwepo Maarabu wa asili ya Yemen
Alikuwepo Mngazija
Majemadari hawa walifanya jambo kubwa kwa manufaa ya Umma wa Zanzibar walijitolea uhai wao.
Baada ya Kifo hiki Zanzibar ilibadilika kidogo kidogo na mpaka sasa mambo ya kuna nafuu ingawa bado haki haija patikana sawa sawa
Picha ni Comandoo Lt. Humud

View attachment 1416474

Sent from my iPad using JamiiForums
 
Wajameni haya mambo ya Zanzibar ni magumu. Ukisikia ya Karume aliyoyafanya kwenye mambo ya haki za binaadam hautashangaa. What goes around, comes around!.

Ethiopia haikuwahi kutawaliwa tangu enzi za Qeen of Sheba mpaka kina Manelik na hatimaye Haile Selasie. Ukisikia aliyoyafanya na kilichomkuta, hutashangaa.

Kwa mliomjua William Tolbert wa Liberia alivyo fanywa na Master Sergent Samuel Doe na kilichomkuta Doe, hutashangaa.

Hata aliyoyafanya Dr. Salmin na kilichomkuta na kinachoendelea kumkuta hadi sasa, hutashangaa.

Sheria ya siri ni miaka 50, hivyo subiri 2021 zitafunguliwa. Kuanzi baada ya Desember 9 mwaka huu, siri za uhuru na serikali ya Tanganyika zitamwagwa hadharani.
Leo ni Karume Day, nami naomba kujiunga na Watanzania wenzetu maadhimisho mema ya Karume Day na kuwatakia mapumziko mema.
RIP Abedi Amani Karume.
Paskali
 
Karume alikuwa muuaji katili, muungano kwake ulikuwa muhimu sana kwake kwani zanzibar alikuwa na maadui wengi sana.Kwa sababu hakushiriki mapinduzi aliishi kwa hofu kubwa ya kupinduliwa.
Yale mauaji yalikuwa ya kisasi ni karma.
 
"The stong man in the world is the one with the best information"

Hii ni kauli ya waziri mkuu wa zamani wa Uingereza Benjamin Disarel ambaye aliwahi kutawala kipindi nchi hiyo wakati wa vuguvugu la vyama vya wafanyakazi mwaka 1967, tofauti na watangulizi wake Disarel yeye aliwataka makundi yote ya waingereza wanyonge waliokuwa wanapambana kwa ajili ya maslahi yao kuwa na taarifa sahihi kwa wakati mwafaka hakika haya ni maneno mazito sana.

Naam! Leo tunapoadhimisha Karume Day kuna haja ya kuwa na taarifa sahihi kuhusu kifo cha Mzee Karume ambaye anatajwa kuwa mwasisi wa mapinduzi ya Zanzibar ya januari 12 , 1964. Nalisema hili kwa jinsi mambo yanavyofichwa nabashiri kuna uwezekano mkubwa huko mbele tuendako wazungu wakaja kutusaidia kufanya utafiti wa kifo cha shujaa huyo, ili kuelewa nayoyasema rudia makala za mwandishi nguli wa Raia Mwema Bw Joseph Mihangwa au nenda visiwani Zanzibar halafu uliza wakazi wa visiwa hivyo vya karafuu wakwambia sababu za mzee huyo kupigwa risasi mnamo mwaka tarehe7 mwezi wa 4 mwaka 1972? Kisha kwa wingi na mkanganyiko wa majibu ndio utakubaliana nami umefika wakati tuhoji yasiyohojika.

Kwanza swali rahisi hivi ni kweli serikali zetu hizi za Zanzibar na ya Muungano hazifahamu sababu za kifo cha mzee huyo? Hivi ni kweli kabisa mpaka leo tumeshindwa kuweka wazi swala hili? Kwanini? Imefika sehemu tumeruhusu mapambano na malumbano ya wanahistoria kutafiti chanzo cha mauaji hayo ilihali tumeukalia ukweli? Tunaogopa nini? kwa maana tunapojadili mauaji hayo kuna maswali na mtiririko wa kimantiki unaotushawishi kuwa mzizi haswa wa mauaji hayo ni siasa za chuki na kama tunakubaliana katika hili ni lazima twende mbele tujihoji je tumezimaliza hizo siasa za chuki? Au bado zipo?

Hoja ya kwanza katika mtiririko huu ni kuwa kwanza Karume hakuuawa kwa bahati mbaya la hasha! Ilikuwa ni mipango ya watu Fulani na ndio maana ttunasikia matokeo yake ni kuwa baada ya kifo hiko watoto wa mzee huyo walianza kunyimwa fursa zza kimaendeleo kama vile walinyimwa ajira na baadhi yao walifukuzwa kazi haya kayasema mke wa marehemu Karume mama Fatuma Karume akiongea kupitia TBC1 mapema leo, hii ina maana kuwa baada ya kifo hiko chuki haikuisha ikahamia kwa watoto na mke wake ambaye anaweka bayana kuwa ni Nyerere tu aliyewahi kumfariji mama huyo wengine wote walimtoa kwenye kumbukumbu zao hakika hii ni chuki kubwa!

Kutokana na hali hii tunapaswa tujihoji kina nani walihusika na mauaji haya? Na nini kiliwasukuma? Na kwanini chuki hiyo ilifika kwa watoto wake? Je, ikiwa bado watoto wa karume wako hai tutaaminije kuwa chuki hiyo imekwisha? Nini mzee karume alifanya mpaka ikatokea hiyo chuki? Lakini tusiishie hapa kwenye mauaji haya kuna jingine , inadaiwa kuwa mzee Karume aliuwawa na mwanajeshi, je kama mwanajeshi ndiye alimwua je hayo siyo mapinduzi ya kijeshi? Kwanini? Lakini pia ingawaje Karume aliuwawa na mwanajeshi cha ajabu ni kuwa uongozi wan chi haukutwaliwa na jeshi bali alipewa mwanasiasa tu Aboud Jumbe!, haya ni maajabu mengine sasa, hivi huyo Hamid aliyemwua mzee karume alitumwa na wanasiasa? Au? Na kama hajatumwa kwanini baada ya mauaji hayo yaliyofanywa na mwanajeshi tunaambiwa kuwa jeshi lilitaka limpe madaraka kanali Seif Bakari hata hivyo baadaye tunaambiwa liliachana na mpango huo, je nini kiliwasukuma kuacha mpango huo? Na nani aliwakataza kufanya hivyo? Hatuoni kuwa iwapo jeshi lingempa uongozi kanali Seif Bakari ambaye pia ni mwanajeshi hatuoni kuwa hayo yangekuwa ni mapinduzi ya kijeshi au uasi wa jeshi? Kwanini jeshi limfanye hivo mzee karume? Aliwakosea nini wapiganaji wake hawa?

Kwa maswali mengi kama haya yasiyo na majibu ndiyo inaibuka haja ya kufahamu je nini sababu za mauaji hayo? Nani alikuwa nyuma ya mauaji hayo? Ni wanajeshi au wanasiasa kwa mgongo wa jeshi? Kina nani hao? Na kwanini? Je chuki zilizopelekea mauaji hayo zilikoma au zingalipo hadi leo? Tukiyajua haya itatuweka huru kwa maana ukweli pekee ndio utatuweka huru vinginevyo tunaficha historia yetu kwa hasara yetu wenyewe! Naam ! wakati ni huu watanzania acha sasa tuhoji yasiyohojika!

Tafakari!

Kitendawili si deni ukishindwa nipe mji,
Kwa wanataaluma kutofautiana kimawazo si kosa bali ni dalili ya jamii iliyo hai,
Nova Kambota,
Tanzania, East Africa,
Alhamisi 7 April, 2011

==========
April 2012
Karume alikuwa sawa tu na Magu...kuna watu wakiona huyu jamaa anatupanda kichwani wanarekebisha mambo
 
All roads lead to Rome.

Nyerere, Nyerere, Nyerere.

Nini zaidi kinachotakiwa? iweje Nyerere awawachie huru baada ya muda watu waliokula njama za uhaini na mpaka Karume kuuawa? Haiingii akilini.
Itakuwa Nyerere alifanya hivi kwaajili ya dini tu..au unasemaje mama?
 
Maswali Yako mepesi sana hayahitaji tafakuri!
Hivi Kiongozi aliuawa na meanajeshi tayari hayo tuyaite Mapinduzi ya kijeshi!?
Kwa hiyo watoto wa Karune walibaguliwa na bado wakakwea hadi Ikuku na u2qziri,na ubalazi!
Au Kuna watoto WENGINE u awazuznzgumzia sio kina Amani na Ally?
 
Ukizingatia ukweli kwamba Nyerere ndiye aliyekiunda chama cha ASP utajua kuwa Karume alikuwa ni kibaraka wa Nyerere aliyewekwa kuwatawala Wazanzibari. Sasa kiongozi kibaraka akikorofishana na aliyemweka madarakani, kibaraka hawezi kutawala muda mrefu. Atapinduliwa abaki kuwa mkimbizi, au atafungwa au yatampata yaliyompata mzee Karume.

Back
Top Bottom