Mauaji ya Mzee Karume: Acha sasa tuhoji yasiyohojika! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mauaji ya Mzee Karume: Acha sasa tuhoji yasiyohojika!

Discussion in 'Jukwaa la Historia' started by KAMBOTA, Apr 7, 2011.

 1. K

  KAMBOTA Senior Member

  #1
  Apr 7, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 176
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  ………the stong man in the world is the one with the best information……..

  Hii ni kauli ya waziri mkuu wa zamani wa Uingereza Benjamin Disarel ambaye aliwahi kutawala kipindi nchi hiyo wakati wa vuguvugu la vyama vya wafanyakazi mwaka 1967, tofauti na watangulizi wake Disarel yeye aliwataka makundi yote ya waingereza wanyonge waliokuwa wanapambana kwa ajili ya maslahi yao kuwa na taarifa sahihi kwa wakati mwafaka hakika haya ni maneno mazito sana.

  Naam! Leo tunapoadhimisha Karume Day kuna haja ya kuwa na taarifa sahihi kuhusu kifo cha Mzee Karume ambaye anatajwa kuwa mwasisi wa mapinduzi ya Zanzibar ya januari 12 , 1964. Nalisema hili kwa jinsi mambo yanavyofichwa nabashiri kuna uwezekano mkubwa huko mbele tuendako wazungu wakaja kutusaidia kufanya utafiti wa kifo cha shujaa huyo, ili kuelewa nayoyasema rudia makala za mwandishi nguli wa Raia Mwema Bw Joseph Mihangwa au nenda visiwani Zanzibar halafu uliza wakazi wa visiwa hivyo vya karafuu wakwambia sababu za mzee huyo kupigwa risasi mnamo mwaka tarehe7 mwezi wa 4 mwaka 1972? Kisha kwa wingi na mkanganyiko wa majibu ndio utakubaliana nami umefika wakati tuhoji yasiyohojika.

  Kwanza swali rahisi hivi ni kweli serikali zetu hizi za Zanzibar na ya Muungano hazifahamu sababu za kifo cha mzee huyo? Hivi ni kweli kabisa mpaka leo tumeshindwa kuweka wazi swala hili? Kwanini? Imefika sehemu tumeruhusu mapambano na malumbano ya wanahistoria kutafiti chanzo cha mauaji hayo ilihali tumeukalia ukweli? Tunaogopa nini? kwa maana tunapojadili mauaji hayo kuna maswali na mtiririko wa kimantiki unaotushawishi kuwa mzizi haswa wa mauaji hayo ni siasa za chuki na kama tunakubaliana katika hili ni lazima twende mbele tujihoji je tumezimaliza hizo siasa za chuki? Au bado zipo?

  Hoja ya kwanza katika mtiririko huu ni kuwa kwanza Karume hakuuawa kwa bahati mbaya la hasha! Ilikuwa ni mipango ya watu Fulani na ndio maana ttunasikia matokeo yake ni kuwa baada ya kifo hiko watoto wa mzee huyo walianza kunyimwa fursa zza kimaendeleo kama vile walinyimwa ajira na baadhi yao walifukuzwa kazi haya kayasema mke wa marehemu Karume mama Fatuma Karume akiongea kupitia TBC1 mapema leo, hii ina maana kuwa baada ya kifo hiko chuki haikuisha ikahamia kwa watoto na mke wake ambaye anaweka bayana kuwa ni Nyerere tu aliyewahi kumfariji mama huyo wengine wote walimtoa kwenye kumbukumbu zao hakika hii ni chuki kubwa!

  Kutokana na hali hii tunapaswa tujihoji kina nani walihusika na mauaji haya? Na nini kiliwasukuma? Na kwanini chuki hiyo ilifika kwa watoto wake? Je ikiwa bado watoto wa karume wako hai tutaaminije kuwa chuki hiyo imekwisha? Nini mzee karume alifanya mpaka ikatokea hiyo chuki? Lakini tusiishie hapa kwenye mauaji haya kuna jingine , inadaiwa kuwa mzee Karume aliuwawa na mwanajeshi, je kama mwanajeshi ndiye alimwua je hayo siyo mapinduzi ya kijeshi? Kwanini? Lakini pia ingawaje Karume aliuwawa na mwanajeshi cha ajabu ni kuwa uongozi wan chi haukutwaliwa na jeshi bali alipewa mwanasiasa tu Aboud Jumbe!, haya ni maajabu mengine sasa, hivi huyo Hamid aliyemwua mzee karume alitumwa na wanasiasa? Au? Na kama hajatumwa kwanini baada ya mauaji hayo yaliyofanywa na mwanajeshi tunaambiwa kuwa jeshi lilitaka limpe madaraka kanali Seif Bakari hata hivyo baadaye tunaambiwa liliachana na mpango huo, je nini kiliwasukuma kuacha mpango huo? Na nani aliwakataza kufanya hivyo? Hatuoni kuwa iwapo jeshi lingempa uongozi kanali Seif Bakari ambaye pia ni mwanajeshi hatuoni kuwa hayo yangekuwa ni mapinduzi ya kijeshi au uasi wa jeshi? Kwanini jeshi limfanye hivo mzee karume? Aliwakosea nini wapiganaji wake hawa?

  Kwa maswali mengi kama haya yasiyo na majibu ndiyo inaibuka haja ya kufahamu je nini sababu za mauaji hayo? Nani alikuwa nyuma ya mauaji hayo? Ni wanajeshi au wanasiasa kwa mgongo wa jeshi? Kina nani hao? Na kwanini? Je chuki zilizopelekea mauaji hayo zilikoma au zingalipo hadi leo? Tukiyajua haya itatuweka huru kwa maana ukweli pekee ndio utatuweka huru vinginevyo tunaficha historia yetu kwa hasara yetu wenyewe! Naam ! wakati ni huu watanzania acha sasa tuhoji yasiyohojika!

  ...Tafakari!


  Kitendawili si deni ukishindwa nipe mji,
  Kwa wanataaluma kutofautiana kimawazo si kosa bali ni dalili ya jamii iliyo hai,
  Nova Kambota,
  Tanzania, East Africa,
  Alhamisi 7 April, 2011


  ==========
  April 2012
   
 2. a

  allydou JF-Expert Member

  #2
  Apr 7, 2011
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 1,485
  Likes Received: 572
  Trophy Points: 280
  nikichambnua kwa haraka tu kutoka kwenye makala yako, na nikiongeza yale machache niliyowahi kuyasikia na yakakubaliana na akili yangu kwamba yanaweza kuwa sawa, naweza kusema kama ifuatavyo, kwa ufupi tu:-

  1) karume aliuliwa na wanasiasa/mwanasiasa aliyekuwa na nguvu ya kutosha ya ushawishi na utawala enzi hizo. na huyo mtu ndie aliyepanga mkakati wa kuisotesha familia yake makusudi( kuna sababu ya hili na mpango mzuri kwa familia baadae kuwapoteza wasiweze kuhisi kwa urahisi kama ni yeye) , na ndie aliyeaamrisha urais asipewe kanali bakari ila apewe jumbe. waliotaka kumpa kanali bakari ni wale amabao hawakujua kama mauaji yalikuwa planned, na ndio maana pamoja na kwamba mauaji yalifanywa na mwanajeshi kama unavyosema lakini jeshi halikuchukua nchi kwa sababu jeshi kama jeshi halikuwa na hiyo plan, kutaka kumpa kanali bakari ni kwa sababu hawakuwa na plan ya mapinduzi ya kijeshi ila ilikuwa ni maamuzi ya ghafla kwa tukio la ghafla.

  2) aliyefanya mauaji hakuwa na shida na urais wa zanzibar, na ndio maana hakuna aliyeclaim urais huo bada ya mauaji wala hakukuwa na movement nyingine yeyote ya kutaka kufanya mapinduzi wala mauaji bada ya hapo.

  3) aliyepanga mauji hayo alikuwa anataka kile kilichotokea na kinachoendelea leo ambacho wengi hawakitaki. kingetokea pia bila ya mauji lakini kungeweza kuleta shida kidogo baadae kidogo kama jamaa angekuwepo, kutokuwepo kwake ilikuwa ni much green lighter.

  bahati mbaya muda haunitoshi, ningetoa ufafanuzi zaidi, lakini angalu mwenye akili zake anaweza kuunganisha dots, akaweza hisi kile ninachokiona mimi.
   
 3. kinja

  kinja Senior Member

  #3
  Apr 7, 2011
  Joined: Oct 10, 2010
  Messages: 199
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mi nashukuru kwa makala yako. Tunasikia yule aliyemuua karume alikuwa luteni leutnunt ambaye baba yake alikamatwa na serikali ya karume katika sakata lile pamoja na akina babu. Baadaye alipotezwa na kujenga chuki kati ya umma party na asp ambao walikuwa pamoja katika mapinduzi ya 64, rejea Dr. Salim A. Salim ktk umri wa miaka 22 kijana wa umma part kuteuliwa kuwa balozi nchini misri
   
 4. Obe

  Obe JF-Expert Member

  #4
  Apr 7, 2011
  Joined: Dec 31, 2007
  Messages: 5,982
  Likes Received: 20,375
  Trophy Points: 280
  Historia hapa inajikanganya sana!:help:
   
 5. M

  Mtwike Senior Member

  #5
  Apr 7, 2011
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 116
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  SIRI YA MTUNGI ............
  PILIPILI USIOILA YAKUWASHIYANI?
  Badala kutueleze Sokoine kafaje au Kolimba kafaje, mwaleta hadithi za Alfu ulela!

  Mwajuwa kuwa huyo Salim ni mmoja wa watuhumiwa? na aliyemlinda ni nani? Sasa aliyemlinda naye ahusika? Fumbo mfumbie .......
   
 6. P

  Percival JF-Expert Member

  #6
  Apr 7, 2011
  Joined: Mar 23, 2010
  Messages: 2,567
  Likes Received: 617
  Trophy Points: 280
  Inasemekana mzee Karume alipouwawa alikua na $ 20 milioni nchi za nje ? hizo ni fedha nyingi sana 1972 ukichukulia wakati huo wazanzibari walikua wanasota sana kimaisha
   
 7. n

  nzom Senior Member

  #7
  Apr 8, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 168
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Umejitahidi ukweli tamimu,hamidu na hamudi ni miongoni mwa vijana makomandoo watatu waliowahi kutokea tanzania wa kwanza akiwa mzaliwa wa tanga mwingine bukoba na huyo tamimu mmoja kati yao alikufa baada ya kushindwa kuluka ukuta wa pepsi siku ya majaribio ya kutaka kumpindua mwl na sister aliebeba bunduki kushindwa mmoja akiwa radi tz mwingine ikulu na baada ya hapo tamimu alirudi zanj baba yake akaletwa kwneye gunia na baadae akaitwa mwana akaambiwa na karume kua nina mzigo huu nataka upige risasi bwana huyo hakujua na baada ya kufungu akakuta kamuaa baba yake mzazi akajiapiza mbele ya karume kua atamua kwa mkono wake siku ya tukio aligawa bunduki na alitoa pin na akamfuata mzee karume na kumwambia siku ile ndio leo na akatimiza malipizo yake mwenyewe je wataka kujua kwa nn karume alimua baba mtu endelea kufuatilia
   
 8. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #8
  Apr 8, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,566
  Likes Received: 18,533
  Trophy Points: 280
  Wajameni haya mambo ya Zanzibar ni magumu. Ukisikia ya Karume aliyoyafanya kwenye mambo ya haki za binaadam hautashangaa. What goes around, comes around!.

  Ethiopia haikuwahi kutawaliwa tangu enzi za Qeen of Sheba mpaka kina Manelik na hatimaye Haile Selasie. Ukisikia aliyoyafanya na kilichomkuta, hutashangaa.

  Kwa mliomjua William Tolbert wa Liberia alivyo fanywa na Master Sergent Samuel Doe na kilichomkuta Doe, hutashangaa.

  Hata aliyoyafanya Dr. Salmin na kilichomkuta na kinachoendelea kumkuta hadi sasa, hutashangaa.

  Sheria ya siri ni miaka 50, hivyo subiri 2021 zitafunguliwa. Kuanzi baada ya Desember 9 mwaka huu, siri za uhuru na serikali ya Tanganyika zitamwagwa hadharani.
   
 9. T

  T.K JF-Expert Member

  #9
  Aug 8, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 345
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Fafanua kidogo hapo mkuu
   
 10. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #10
  Aug 8, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0

  Hii inaweza kuwa adithi ya kusadikika ambayo inatumia characters waliowai kuwepo duniani. Hii ndio shida za nchni maskini polisi hawa chunguzi matukio ya vifo kitaalam na kutoa report kwa Umma badala yake Umma unaishi kwa speculations na mtu akitunga adithi yoyote inaweza ku-fit in ili mradi ajue tu majina ya wahusika na aina ya tukio analolitungia adithi.
   
 11. Sonara

  Sonara JF-Expert Member

  #11
  Aug 8, 2011
  Joined: Oct 2, 2008
  Messages: 730
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  kwa ufahamu wangu nakumbuka wakati ule nikijana mdogo mwenye akili yangu timamu tulikuwa tunangalia kesi ya marehemu karume kupitia TVZ ,kulikuwa na Mtu ambae huwa hatajwi jina isipokuwa hutajwa kama MR X
  Pili tujiulize kwa nini mzee karume mpaka nakata mauti alikuwa hazungumzi na Kambarage (kamnunia )
  Tatu ni nani alisababisha kifo cha Khanga
  Nne ni nani aliyeamrisha kupelekwa zanzibar Bititi na kufanyiwa machafu na mateso ambayo sitoweza au hayastahiki kuandikwa hapa
  Mama karume anasema ni kambarage peke yake aliwahi kumfariji lakini basi tusisahau panya akutafunapo(kungaka) huwa anakupuliza usipate maumivu
  Lamwisho nataka kuchangi kuhusu wanajeshi walipotaka kumpa urais seif Bakari Kambarage akasema haitowezekana kufanya hivyo na akatowa sababu zake na ndipo wanajeshi wakakubaliana nae kwa ushauri huo
  sasa ukiangalia Director
  wa mchezo wote anaeleweka na wla huhitaji (Brain surgery)kulijuwa hilo (kuelewa ) ni nani alikuwa Behind all this
   
 12. V

  Vonix JF-Expert Member

  #12
  Aug 8, 2011
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 1,988
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Uzuri wa jamvi hili kama jambo hulijui vema uliza ueleweshwe,usijaribu kuponda na kuleta kashfa kwa mleta mada vinginevyo na wewe ni mmoja kati ya wale wanapenda siri iendelee kufichwa!'outdated mind'nahata kifo cha sokoine wewe lete maada hapa utaambiwa.mengi tutayasikia lakini mwisho wa siku hayatakuwa siri tena.tusubiri.
   
 13. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #13
  Aug 8, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,246
  Likes Received: 3,831
  Trophy Points: 280
  Acheni kutafuna maneno! Aliyemuua Karume ni JULIUS K NYERERE rais wa kwanza wa Tanganyika na chama chake cha TANU-CCM!
  Si huyo tu ambaye kauawa na serikali ya ccm, orodha ni ndefu sana.

  Tunasubiri 2015 watakapokuwa chama cha upinzani ndipo tutafungua kesi za mauaji hayo maana ushahidi upoo!!
   
 14. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #14
  Aug 8, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Da inahonekana ukusoma RAI enzi zake mdau hakuna matimba hapo huo ndio ukweli.Simulizi zinasema hata Mwalimu hakufurahishwa na mauaji ya komando huyo.
   
 15. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #15
  Aug 8, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Tujuze sababu za Mwalimu kufanya hayo manake umemvisha kitanzi bila kumungunya maneno kuwa ndio muhusika.Tusaidie.
   
 16. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #16
  Aug 8, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  zama na nayakati huwa asifungwi na tunakoelekea ni kutungwa kwa katiba mpya wazungu wanasema Time will tell.Wamarekani huwa wanakaa na sirikuu [TOP SECRET] miaka 25 inakuwa sio siri tena.Ndio maana wanajua na kusema wazi kwanini walitenda jambo fulani.Fuatilia swala la Patrick Lumumba liko wazi ni kwanini walimua na mengineyo mengi yaliyotokea zama hizo.

  Kuna mdau alisema kwetu Tanzania ni Miaka 50,tena kwangu mimi naona miaka mingi sana hiyo ilitakiwa japo miaka 25 au 30 tu SIRI KUU inawekwa wazi waliohusika kwenye SIRI mioyo yao inapumua na kuiachia jamii kutafakari na kupima umuhimu wa tukio kuwa ulifanyika [Collective or Joint Responsibiliy].

  Manake hizi SIRI KUU zinakuwa na sababu na umuhimu kwa TAIFA.Kwa kuwa pasipo kutendwa hili ama lile madhara ya hiki au kile yatakuwa makubwa kwajamii au Taifa kwa ujumla wake.Tujue Serikali zote duniani toka zilpoanzishwa mpaka Mungu atakapotengua uwepo wa Serikali za kidunia zitaendelea kuwepo na kuendeshwa kwa mipango na mikakati zikiwemo hizo SIRI KUU.

  Muda ya nyakati ndio zinafungua vitabu vya siri kuu na kufanya kizazi kilichopo na kijacho kuona na kujifunza kupitia zilizokuwa SIRIKUU.

  Sio kuwa watu awajui kilichotokea kwa Sokoine watu wengi wanajua lakini wasichojua ni usahihi wa taarifa zao kwa kuwa sio wahusika wa matendo kitakacho kuwa sahihi ni taarifa lasmi toka kwa wahusika na muda ukifika umma utajua kama ni sawa au si sawa na kama aliuwawa au ni ajari kama ajari.[Confession].
   
 17. Remote

  Remote JF-Expert Member

  #17
  Aug 8, 2011
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 14,875
  Likes Received: 1,562
  Trophy Points: 280
  eleza kinaganaga, don't talk as layman
   
 18. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #18
  Aug 8, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Ndio maana yake watoto wa mujini wanasema funguka
   
 19. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #19
  Aug 8, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,246
  Likes Received: 3,831
  Trophy Points: 280
  Sababu kuu ya Mt JK Nyerere kukatisha uhai wa baharia yule ni MUUNGANO!

  Baadhi ya mambo waliyokuwa wamekubaliana ktk muungano huu Mt Nyerere alikuwa hayatekelezi ndipo baharia alipo anzisha harakati za kujiondoa ktk muungano! Mt Nyerere kuona hivyo akaukatisha uhai wa Baharia Karume!

  Wapo wengi waliouawa kwaajili ya kupinga muungano huu!

  Na wapo ambao kila maadhimisho ya muungano huu wao kauli mbiu yao ni "Hatuta sahau siku ambayo Mzanaki alituingiza mjini"
   
 20. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #20
  Aug 8, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Wapi na wapi?kuna mdau katujuza kuwa muuaji wa Mzee karume alikuwa ni mlipizaji wa kisasi wa kifo cha Baba yake [Hoja hii kama ni kweli Mzee Karume alishurutisha mtoto Mtu kumua Baba yake pasipo hiari yake hata kama ilikuwa ni SIRI KUU hapo ilikuwa ni dhambi ambayo mmalipo yake lazima yangerudi] . Yani wenzetu wanasema what goes around comes around.Hoja ya kulipa kisasi asilmia kubwa ina mashiko kwangu kwa kuwa na utamaduni wa watu wa kimazingira siasa za Zanzibar zimezungukwa na visasi kwa hilo naafiki kuna uwezekano.

  Haya mdau Jason wewe unakuja na hoja ya Mwalimu kumua Mzee Karume ambae kwa jukumu alilokuwa nalo tena kwa hiari yake mwenyewe alimfuata Mwalimu ili auende Muungano na si Mwalimu aliyemfuata kuunda Muungano.Hiyo imeakaaje aliayetaka Muungano ndie awe mvunja muungano huo huo?Naomba ufafanuzi ukiziangati hiyo taarifa ya mdau kuhusu ujumbe hapo juu.
   
Loading...