Mauaji ya Makahaba nchini Rwanda

Kimbori

JF-Expert Member
Feb 21, 2012
5,445
3,201
Kumezuka wimbi la mauaji ya
wasichana Nchini Rwanda. Mpaka
sasa wanaohusika na mauaji hayo
hawajajulikana.

Mauaji hayo yanawalenga wasichana
makahaba. Kwa mwezi huu wa Agosti pekee, wasichana 15
wamekwishauawa kwa njia mbali
mbali ikiwa ni pamoja na kukatwa
katwa kwa vitu vya ncha kali au
kunyongwa.

Jana mchana kuna habari ya kuwa wasichana watatu waliuawa kwa
kunyongwa kwenye nyumba moja
ambayo ipo sehemu ya makazi ya
watu wengi.
CHANZO: Sauti ya Ujerumani - Kiswahili, leo mchana
 
Usikute ni dini mpya ambayo lengo lao namba moja ni kuhakikisha makahaba wote wanatokomezwa
 
Mkuu hilo wimbi la mauaji nahisi linaendeshwa na usalama wa taifa wa Rwanda. Miaka ya nyuma mtu aliyehisiwa kuwa ni jambazi aliuliwa na serikali kwa staili ambayo iliacha maswali yasiyokuwa na majibu. Hivi jiulize intelijensi ya Kagame ilivyo mpaka sasa wamashindwa kuwatambua hao wauaji? Na hali ya usalama ilivyo nchini Rwanda hakuna raia ambao sio members special forces wanaweza kutekeleza wimbi la mauaji kiasi hicho ndani ya nchi ya kagame.
 
Kwa jinsi ilivyokuwa inaelezwa na Sauti ya Ujerumani, hata mimi nahisi ni mipango ya Serikali ya Rwanda, ikizingatiwa ukahaba umepigwa marufuku.
Viongozi wa dini na mashirika ya kutetea haki za binadamu wanashinikiza serikali ifanye uchunguzi ili kujua chanzo.
 
Back
Top Bottom