Mauaji ya kutisha bugalika, mwanza!!!!

Mauaji ya kutisha bugalika, mwanza!!!!

LIKUD

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Posts
19,987
Reaction score
37,892

Chacha Mwikwabe mzaliwa wa wilaya ya Tarime mkoani Mara, aliwasili mkoani Mwanza, mnamo mwaka 1985 kwa ajili ya kuanza kazi kama askari Polisi kwenye kituo kidogo cha Polisi cha Igogo.Wakati huo alikuwa ni kijana mwenye umri wa miaka 23 . Mwaka 1989 akiwa ameenda kuhudhuria mahafali ya dada yake mdogo, kuhitimu shule ya msingi katika Shule ya Msingi Mlimani, alifanikiwa kukutana na binti aliye itwa Ummy Chende ambaye naye pia alikuwa anahitimu darasa la saba mwaka huo. Chacha Mwikwabwe alitokea kuvutiwa na binti huyu wa kirangi katika namna isiyoweza kuelezeka kwa urahisi. Afande Chacha akaanza urafiki na huyu binti wa kirangi aliye jaaliwa urembo usio kuwa wa kawaida japo alitoka kwenye familia masikini sana ( JAPO SIKUWAHI KUMUONA, ILA UZURI WAKE NAUFANANISHA NA MAUA , DEMU WA BON KOLO NA KANDILI MAULANA KWENYE PESA ZAKO ZINANUKA )...

Baada ya Afande Chacha kuonekana yupo seious, Ummy akamwambia yeye hayupo tayari kuwa na mwanaume hadi ndoa, Afande Chacha akasema yupo tayari kwa ndoa . Basi Afande Chacha akaenda kutambulishwa kwa wazazi wa UMMY. Baada ya kumuhoji, wazazi wa UMMY wakampa Afande Chacha masharti yafuatayo :

1. Abadilishe dini awe muislamu.

2. Amsomeshe Ummy hadi kidato cha nne, halafu ampeleke kwenye chuo cha ualimu, baada ya hapo, wataruhusu amuoe binti yao.

Chacha alikubali kwa mikono yote miwili. Wiki tatu baadaye, Chacha alianza kuhudhuria Madrasa na alibadili jina na kujiita Yaseen.

Matokeo ya darasa la saba yalipotoka Ummy hakuwa amechaguliwa, lakini kwa kuwa Chacha alisha ahidi kumsomesha Ummy, alimlipia ada kwenye shule binafsi ya sekondari iitwayo LAKE SECONDARY. Chacha alimwambia UMMY kuwa hatomjua kimwili hadi watakapo funga ndoa. Mwaka 1993 Ummy alimaliza kidato cha nne na kupata Division 4 ya point 26. Katika kipindi chote alicho kuwa anasoma, Chacha ndio alikuwa anamsomesha na kuitunza familia ya wazazi wa Ummy.. Mwaka uliofuata Ummy alifanikiwa kupata nafasi ya kusoma uhazili kwenye chuo cha uhazili Tabora. Mwezi mmoja kabla ya kwenda kujiunga na Chuo , Ummy alikutana na kijana mmoja, msomi, tajiri na anaye toka kwenye familia ya kitajiri pia. Familia ya kijana huyu ilikuwa ikiishi Capripoint jijini Mwanza. Kwanza alimshauri asiende kusomea uhazili, lakini pili alimuahidi kumpeleka Arusha kusomea uhasibu. Vilevile kijana huyu aliahidi kuwasomesha wadogo zake Ummy pamoja na kuwajengea nyumba na kuwafungulia biashara wakwe zake hao.

Posa ya huyu jamaa ilikubaliwa ,na haraka haraka ikaanza kufanyika mipango ya ndoa. Wakati yote haya yanafanyika Chacha alikuwa hajui chochote kinacho endelea hadi msamaria mmoja kwa kumuonea huruma kijana wa watu akaenda kumtonya….. Chacha alihamaki sana na hakuamini alicho ambiwa, lakini baada ya kufanya upelelezi wake alifanikiwa kugundua kuwa, jumamosi ya tarehe 18 JUNI 1994 kungekuwa na harusi nyumbani kwa kina Ummy lakini hakuwa na uhakika ni nani angeolewa. Kwa kuwa aliwaamini na kuwaheshimu sana wazazi wa Ummy hakutaka kwenda kuwauliza , isipokuwa alimua yeye mwenyewe kwenda kushuhudia kwa macho yake siku ya tukio.
Siku ya tukio, Chacha alifika nyumbani kwa akina Ummy na kukuta Ummy anaolewa. Alicho kifanya Afande Chacha, aliwapiga risasi wazazi wa Ummy, akampiga risasi Ummy na yeye mwenyewe akajipiga risasi. Mauaji haya yalilitikisa jiji la Mwanza na vitongoji vyake na kutoa funzo kwa kubwa kwa watu wote.
Baada ya tukio hilo, wadogo zake na Ummy walichukuliwa na ndugu zao.. Wawili walichukuliwa na shangazi yao aliye ishi, Ngarenaro ARUSHA ,wawili akiwemo msimuliaji wa kisa hiki walichukuliwa na ndugu zao wanaoishi hapa DSM na mmoja aliyekuwa mdogo kuliko wote alichukuliwa na bibi/babu zake aliye ishi Kondoa.

CHANZO CHA HABARI : Rafiki yangu IBRAHIM CHENDE, kaka mdogo wa Marehemu Ummy.

N.B: TUKIO HILI LINAWEZA KUJIRUDIA KWA MTU YOYOTE , SEHEMU YOYOTE NA WAKATI WOWOTE. TAKE CARE!
 
Yeah, if you play with someone's HEART and SOUL, this is exactly what will happen to you.
 
^^
Aliyeona pesa akabadili uamuzi na kubadili mfumo mzima wa historia ya ndugu zake.
Yeye ndiye muolewaji
^^

Ila wazazi nao walifanya makosa makubwa sana, bora wangemuita Chacha na kuongea naye, pengine ingeweza kupunguza jazba japo angeumia sana
 
Vipi yule muoaji, je naye alipigwa risasi?
 
dah! Haya ndo matatzo ya kupenda uspopendwa.
 
Nani alaumiwe? Wazazi wa Ummy? Ummy au Chacha?

Kila mtu anastahili lawana tukianzia ummy ni kua alikua unfaithfull....wazazi nao walijali kitu zaid kuliko utu i mean waliendekeza tamaa... chacha yeye tumlaumu kwa kushindwa kutafta njia mbadala ya kulikabidi tatizo.....ijapkua tunaamini kwamba inna swababna maaswaba bil muswiba(kifo hakikosi sababu)
 
Ila wazazi nao walifanya makosa makubwa sana, bora wangemuita Chacha na kuongea naye, pengine ingeweza kupunguza jazba japo angeumia sana

^^
LIKUD
Ni haki kutofautiana maoni..mwanamke ambaye ndiye mwenye kujua nani alimsomesha,,nani alimpenda,,nani alijitoa mhanga kumfikisha alipo hadi akawa mzuri na KUSAHAU ALIKOTOKA huyu ndie kwangu chanzo cha yote..natazama tatizo lilipoanzia sio lilipoishia.
Take note.
Ukigeugeu huu ni wa kawaida kwa sasa,,hususani kwa walioko vyuoni.
Umeweka wazi kuwa kijana aliemuoa ni tajiri..nguvu ya PESA ilimsukuma kubadili mawazo ya binti na familia yote.
Pesa inatawala tamaa ya mwanamke
^^
 
Last edited by a moderator:
^^
LIKUD
Ni haki kutofautiana maoni..mwanamke ambaye ndiye mwenye kujua nani alimsomesha,,nani alimpenda,,nani alijitoa mhanga kumfikisha alipo hadi akawa mzuri na KUSAHAU ALIKOTOKA huyu ndie kwangu chanzo cha yote..natazama tatizo lilipoanzia sio lilipoishia.
Take note.
Ukigeugeu huu ni wa kawaida kwa sasa,,hususani kwa walioko vyuoni.
Umeweka wazi kuwa kijana aliemuoa ni tajiri..nguvu ya PESA ilimsukuma kubadili mawazo ya binti na familia yote.
Pesa inatawala tamaa ya mwanamke
^^

Hapo ndipo ninapokubaliana na falsafa yako ya " Mbele ya pesa...kila goti la mwanamke litapigwa "
 
Kama ni mimi siwezi kukosea kama chacha.

Angewapa ulemavu wa kudumu kwa risasi bila kujulikana aliyefanya tukio hata kwa kutumia watu then anatafuta Mrembo mwingine anaoa.
Siwezi kuacha kuishi kwa ajili ya kiumbe chenye Uke.
 
aisee... sijui pesa imekukosea nini kaka yangu wewe

^^
Hata watu wa chini tunahitaji faraja..
Kwa kuwa wanapigia goti nguvu ya pesa na kutema mate nguvu ya upendo niache niseme huenda nikapata nafuu
^^
 
Back
Top Bottom