Mauaji ya Kisiasa Zanzibar

Mauaji ya Kisiasa Zanzibar

Mauaji ya Kisiasa Zanzibar
==========================

Mwandishi wetu aliyewahoji waadhiriwa katika mauaji ya kisiasa Zanzibar, anakuletea ripoti yenye majonzi na huzuni tele.

Tunaanzia nyumbani kwa mjane Bi Mwajuma Omari. Ukiingia tu kwenye nyumba yao ya chumba kimoja na sebule utaona picha kubwa ukutani ambayo wanadai ilikuwa ya Bwana Omari ambaye aliuawa kinyama na askari wa CCM.

Akisimulia kuhusu kisa hicho, Bi Mwajuma alisema." Ilikuwa kama saa saba usiku, na tayari tulikuwa tumeshalala kwani kulingana na hofu iliyokuwa imetanda Zanzibar kila mtu aliwahi kujifungia ndani hasa kwa kuogopa askari waliokuwa wametanda kila mahali. Pamoja na kukosa usingizi siku hiyo, tuliamshwa na kishindo kikubwa mlangoni pamoja na sauti za ukali zilizotutaka tufungue mlango."

"Binti zetu watatu walikuwa sebuleni na walikuja haraka kugonga mlango wa chumbani kwetu. Mume wangu alifungua mlango haraka na kutoka kuelekea sebuleni wakati binti zetu waliingia haraka chumbani kwa hofu ya wale waliokuwa wakigonga nje."

"Nilimsikia mume wangu akiwauliza walikuwa wakitaka nini usiku huo, lakini walisisitiza tufungue au waanze kumimina risasi ndani ya nyumba." "Baada ya mlango kufunguliwa, waliingia watu zaidi ya kumi na kumwamuru mume wangu akae chini."Walianza kupekua kila mahali na kubeba kila walichokiona kinawafaa, kuanzia vito vya dhahabu pamoja na pesa kidogo tulizokuwa nazo. Katika kipindi chote hicho binti zetu walikuwa wameingia uvunguni mwa kitanda chetu."

Tulipowaliza walikuwa wakitafuta nini, walijibu kuwa wanawatafuta waliohusika na maandamano, na mume wangu alikuwa mmoja wao. Jitiada za mume wangu kujaribu kuwaeleza kuwa yeye hakuusika na maandamano hazikuweza kufua dafu." "Walipomaliza kupekua mmoja wao aliwaona binti zangu uvunguni na kuwaamuru watoke na waandamane nao. Nilijaribu kuwaomba wawaache binti zangu ,lakini
walisisitiza kwamba lazima waende nao. Mume wangu alionekana kuchukizwa na kitendo cha mmoja wa askari hao kumpapasa mmoja wa binti zetu mbele yetu. Aliwaambia kuwa haiwezekani kuwanyanyasa kijinsia binti zake mbele yake. Aliwaambia heri wamuue kuliko wafanye hayo mbele yake. Alimshika askari aliyekuwa anamvua nguo binti yetu na kuanza kungangana naye. Katika harakati hizo askari alifyatua risasi mbili na mume wangu alianguka chini, huku akivuja damu nyingi sana."

"Haraka haraka waliwatoa binti zangu nje na kuniacha mimi na mume wangu ndani. Hawakwenda mbali, kwani niliwasikia wakisemezana hapo nje. baada ya muda
kidogo niliwasikia binti zangu wakilia kwa sauti na wakiniita mama mama. Sikuweza kutoka kwani nilikuwa nikijaribu kumsaidia mume wangu ambaye kwa wakati wote
huo alikuwa anavuja damu nyingi sana lakini alikuwa hajafa. Nilitumia mashuka kujaribu kuzuia damu lakini wapi. Alikuwa anavuja damu kama maji ya bomba."

Nayakumbuka maneno ya mume wangu kabla hajapoteza fahamu. alisema: " Wako wapi wanangu?" Nikamwambia wale askari wameenda nao. Akasema CCM waliiba kura na sasa wamewaiba binti zangu. hata kama nitakufa leo lakini uchungu ninaousikia waambie waislamu wote duniani ili walipize kisasi hata kama ni baada ya miaka mia moja. Waambie binti zangu kama watarudi wakiwa hai kwamba ninawapenda kama baba yao, na nimejitahidi kuwazuia askari wa CCM wasiwadhuru na yaliyonipata waliyaona. Mungu ambaye hapokei rushwa atamhukumu Mkapa na serikali yake ya mabavu ambayo inawatendea wananchi wasio na hatia madhambi ya jinsi hii."

Alipomaliza maneno hayo, alipoteza fahamu na hakupata tena fahamu mpaka tulipomzika.

"Binti zangu walirudi karibu kunapambazuka, na waliyonielezea ni aibu hata kuyasema hapa. Sasa hivi ninavyozungumza binti zangu wawili wamepimwa na kukutwa na virusi vya ukimwi. Sijui kama wanaweza kuwasamehe askari waliowabaka kwa zamu, na mbaya zaidi sijui kama wanaweza kuisamehe serikali ya CCM inayoongozwa na Mkapa." Alimaliza mama huyo aliyekuwa anatoa machozi wakati wote wa mahojiano.


-----
Mwandishi wa habari BBC
Nashindwa kuelewa kabisa na sitoelewa maishani kuona mtanzania anashabikia mambo haya aliyoyafanya Mkapa. Uwe Muislam au Mkristo, atheist au materialist lakini kama Mungu amekupa akili huwezi hata kidogo kushabikia unyama huu.

Ninamuelewa muandishi wa Thread hii alipokuwa na machungu na Nyerere, na kubandika kichwa cha habari "Unyama wa askari wa st Nyerere". Kwasababu, Mkapa alisukumizwa mbele na Nyerere, pamoja na wengi akiwemo katibu wa CCM wa wakati huo Gama kumnyima fomu. Hii ni kwa vile walielewa uwezo mdogo sana wa Mkapa kushika nafasi hiyo. Na kwa taarifa ninazozisikia, kuwa kama Nyerere angefariki miezi sita baada ya Mkapa kuchaguliwa basi nchi ingekuwa katika vita mpaka leo hii.

Kama Nyerere hakujilaumu baadaye kwa uamuzi wake huo, basi hata mimi nakubaliana na kichwa cha habari hii. Kwa vile kusema Nyerere hakuhusika kama wengi wasemavyo, ni kumtetea Nyerere bila sababu. Hakika nawaambia, bila Nyerere, Mkapa hata uwaziri mkuu asingepata. Hata mke wake hakuamini kusikia kuwa Mkapa eti Rais Wa Tanzania.

Yaliyotokea yametokea, lakini kinachonisikitisha mimi ni kuona kuwa pindi mtu akileta habari hizi hunyamazishwa kwa kuitwa mdini. Na mbaya zaidi toka yatokee mauaji hayo, Zaidi ya vyombo vya kiislam hakuna chombo kingine chochote kile kilicholaani ktiendo hicho. Nilitegemea wapenda haki za binaadam kama kkkt, kanisa katoliki na jumuiya nyingine zingelaani mauaji hayo. Lakini yaliyotokea baada ya hapo ni kinyume, eti kumuona Mkapa kama kiongozi shujaa asiyechezewa. Kweli hili halitaweza kusameheka.

Ni katika mambo kama haya ndio yanayogawa nchi. Kulalama kuwa Tanzania hakuna Udini hakutasaidia ikiwa matendo yana mwelekeo mwingine. Ni jukumu la kila mmoja kujiuliza ni nini tumefanya kuungana na wenzetu waliofanyiwa Unyama huko Pemba. Kama kweli wewe unaamini kuwa Pemba ni sehemu ya Tanzania basi haYO YATAKUGUSA KAMA VILE YAMETOKEA KIJIJINI KWAKO.
 
Dada Zawadi calm down. Mara nyingi michango yako huwa katika lugha nzuri lakini naona hapa leo umechemka kweli kweli, kwanini? Sisi Wakristo BWANA YESU anatwambia "........wapendeni adui zenu...." (Mathayo 5:43-44). Pia mtumishi wa MUNGU mtume Paulo anasema "Ushindeni ubaya kwa mema wala msilipize kisasi maana kisasi ni cha MUNGU peke yake (Warumi 12:19-21), "wabarikini wanaowaudhi, barikini wala msilaani" (warumi 12:14).
Tena nashukuru kwa kutoa hiyo mistari. Kinachoniudhi na kunifanya nihamaki ni kuona kwa macho yangu, katika luninge ya Taifa, Huyu Mkapa akishika BIBLIA kubwa na kuapa kwa utulivu na unyenyekevu na kuahidi kulinda katiba ya nchi na wananchi wake.

Sasa najiuliza, hivi BIBLIA aliyoishika wakati ule haikuwa na mistari hiyo? Au ndio unafiki tunaousema mara kwa mara. Wakati umefika sasa kutotumia Vitabu vitakatifu kwa viongozi kuapa pindi wanapochaguliwa. Hivi hatuoni kuwa tunajidanganya. Hilo ndilo linaloniudhi zaidi. Tuache kuiga mambo tusiyoyaelewa.

Vyombo vya habari mara kwa mara huandika kuwa Mwinyi ni rais aliyenyonga watanzania wengi kuliko marais wote Tanzania. Wakati umefika sasa wa kuiandika kuwa Mkapa ndiye Rais aliyeua watanzania wengi zaidi kuliko Rais mwingine Yeyote yule.

Si uongo, Mkapa siwezi kumsamehe hata kidogo mpaka atapoomba radhi katika Luninge.
 
cuf cuf, acheni kampeni zenu ndani ya jf haya tuambie mwandishi gani wa bbc maana wale huwa hawaogopi ktk jambo la ukweli


ingia katika website ya bbc uulize????
 
I think you should do all of us a favor and call yourself Mister Gayvagina given all the Muslim/Islamic crap you are so used to serving us all the time...now, isn't that simply craptastic!


your picture speaks more than my words , THAT IS YOU AND YOUR MIND

and what people are doing to you . tusalimie MCHUNGAJI Mhogolo


THANKS A LOT
 
Yasome kwa kina maneno ya mjane huyu niliyoyanukuu hapa chini. Hivi unapata picha gani? Jaribu kufikiri kama hayo yametokea katika familia yako ungekuwa na picha gani kwa wale wanaomtetea Mkapa? Na kwa wle waliyoisfu hatua yake mara tu baada ya kushushwa mabomu huko Pemba. Nakupa nafasi ujadili kwa kina na familia yako kabla ya kujibu.

"Nayakumbuka maneno ya mume wangu kabla hajapoteza fahamu. alisema: " Wako wapi wanangu?" Nikamwambia wale askari wameenda nao. Akasema CCM waliiba kura na sasa wamewaiba binti zangu. hata kama nitakufa leo lakini uchungu ninaousikia waambie waislamu wote duniani ili walipize kisasi hata kama ni baada ya miaka mia moja. Waambie binti zangu kama watarudi wakiwa hai kwamba ninawapenda kama baba yao, na nimejitahidi kuwazuia askari wa CCM wasiwadhuru na yaliyonipata waliyaona. Mungu ambaye hapokei rushwa atamhukumu Mkapa na serikali yake ya mabavu ambayo inawatendea wananchi wasio na hatia madhambi ya jinsi hii"

Moja katika thread zangu huko nyuma niliandika kuwa tofauti kubwa kati ya Mkapa na Kikwete, ni kwamba Mkapa alitumia mabomu kutatua matatizo yanayowakabili wananchi lakni Kikwete anatumia diplomasia. Na huo ndio utawala bora.

Angalia siku hizi watu wakiomba kuandamana, hupewa ruhusa mara moja. Na maandamano huanza kwa amani na kuisha kwa amani. Wakati wa Mkapa ukiomba kibali cha kuandamana hupati, mpaka hayo maandamano yawe ya wafuasi wa CCM wakiomba kuandamana kwa ajili ya kumpongeza yeye na wauaji wenzake.

Kweli, Mkapa alikuwa kiongozi aliyetawala kwa hofu, bila kujiamini. Alielewa fika kuwa akiondoka madarakani ataandamwa ipasavyo. Ashukuru hako kakinga kakumshtaki kalikowekwa na wafuasi wake, vinginevyo angekuwa na mashtaka zaidi ya 100. Ninamaanisha si hayo ya ufisadi tu, bali hata haya ya mauaji ya Pemba na Mwembe chai.

Nikikuacha nakuomba usome kitabu kilichoandikwa na Prof Hamza kiitwacho "The Mwembechai killings and the political future of Tanzania"
 
Grow up men, would you please think kwa kwenda mbele na siyo kurudi nyuma? mtaishia kumlaumu nyerere hadi mchoke na wakati kashakufa, whethr he is the source of the problem or not, he is not here so find a way to deal with the situation and stop whining. do something 4heaven,s sake.
 
Grow up men, would you please think kwa kwenda mbele na siyo kurudi nyuma? mtaishia kumlaumu nyerere hadi mchoke na wakati kashakufa, whethr he is the source of the problem or not, he is not here so find a way to deal with the situation and stop whining. do something 4heaven,s sake.

Kumbe na humu pia wewe kichwa? Nilifikiri ni kule kwenye mambo yetu tu. Lol!
 
Tena nashukuru kwa kutoa hiyo mistari. Kinachoniudhi na kunifanya nihamaki ni kuona kwa macho yangu, katika luninge ya Taifa, Huyu Mkapa akishika BIBLIA kubwa na kuapa kwa utulivu na unyenyekevu na kuahidi kulinda katiba ya nchi na wananchi wake.

Sasa najiuliza, hivi BIBLIA aliyoishika wakati ule haikuwa na mistari hiyo? Au ndio unafiki tunaousema mara kwa mara. Wakati umefika sasa kutotumia Vitabu vitakatifu kwa viongozi kuapa pindi wanapochaguliwa. Hivi hatuoni kuwa tunajidanganya. Hilo ndilo linaloniudhi zaidi. Tuache kuiga mambo tusiyoyaelewa.

Vyombo vya habari mara kwa mara huandika kuwa Mwinyi ni rais aliyenyonga watanzania wengi kuliko marais wote Tanzania. Wakati umefika sasa wa kuiandika kuwa Mkapa ndiye Rais aliyeua watanzania wengi zaidi kuliko Rais mwingine Yeyote yule.

Si uongo, Mkapa siwezi kumsamehe hata kidogo mpaka atapoomba radhi katika Luninge.
hizi biblia na quran zinahikwa hata na majambazi, wauaji, watoa mimba, wadhulumaji na kila aina ya wenye dhambi, so inategemea na imani ya mtu na kwa hili ni Mungu mwenyewe ndo atajudge.
 
Kumbe na humu pia wewe kichwa? Nilifikiri ni kule kwenye mambo yetu tu. Lol!
mimi kichwa kwani hujanikubali tu? we chriss kama unataka utani tuhamie kule kwetu, si unajua hapa ni kwa watu walio serious na mambo ya nchi.
 
mimi kichwa kwani hujanikubali tu? we chriss kama unataka utani tuhamie kule kwetu, si unajua hapa ni kwa watu walio serious na mambo ya nchi.

Serious na mambo ya nchi ya kifisadi? I hate politics. Mi Ntagombea ubunge kwa ajili ya kujiongezea kipato na wala si vinginevyo. Bila CCM kutoka madarakani, my friend, utaumiza kichwa chako bure ukijihusisha na maswala ya maendeleo ya taifa.
 
Grow up men, would you please think kwa kwenda mbele na siyo kurudi nyuma? mtaishia kumlaumu nyerere hadi mchoke na wakati kashakufa, whethr he is the source of the problem or not, he is not here so find a way to deal with the situation and stop whining. do something 4heaven,s sake.

Nakubaliana na wewe Nyerere is not there anymore, but Mkapa is still there with Billions of money he accumulated during his term. Kwa hiyo ina maana anaefanya makosa hastahiki kujibu au ndio siasa ya ccm kulindana?. Angalia kwa makini Mkapa wa instruction na mafunzo ya Nyerere amewaaccha watoto wangapi Pempa tu bila ya Baba zao waliouliwa bila ya hatia, Jee serikali inawauliza? Alilofanya ni kuwapandisha vyeo askari walioshiriki kwenye hayo mauaji.
Haya ndio matunda aliotuachia huyo Baba yenu wa Taifa, Nyerere, Mkapa, Mugabe, Kibaki etc,etc They are all in the same bench.
 
Grow up men, would you please think kwa kwenda mbele na siyo kurudi nyuma? mtaishia kumlaumu nyerere hadi mchoke na wakati kashakufa, whethr he is the source of the problem or not, he is not here so find a way to deal with the situation and stop whining. do something 4heaven,s sake.
Hata Starlin na Mao wanasemwa vibaya mpaka leo, japo walikufa miaka mingi iliyopita zaidi ya Nyerere. Elewa matatizo ya leo husababishwa na jana. Usipoikumbuka jana hutatatua matatizo hata siku moja.

Na katika misingi hiyo ndio maana tumebakia hapa tulipo. Kwani watu wanaposema tumuenzi Nyerere wanamaana gani, na itakuwa na madhara gani kufanya hivyo.

Angalia, pamoja na kuelewa matatizo ya muungano hakuna anayethubutu kuyakubali au kuyatafutia ufumbuzi wake. Eti tunataka kumuenzi Nyerere. ujinga ulioje? Ndio akina Mkapa hao!!!!!!
 
Back
Top Bottom