Mauaji ya Kisiasa Zanzibar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mauaji ya Kisiasa Zanzibar

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Gavana, Oct 15, 2009.

 1. Gavana

  Gavana JF-Expert Member

  #1
  Oct 15, 2009
  Joined: Jul 19, 2008
  Messages: 17,989
  Likes Received: 1,558
  Trophy Points: 280
  Mauaji ya Kisiasa Zanzibar
  ==========================

  Mwandishi wetu aliyewahoji waadhiriwa katika mauaji ya kisiasa Zanzibar, anakuletea ripoti yenye majonzi na huzuni tele.

  Tunaanzia nyumbani kwa mjane Bi Mwajuma Omari. Ukiingia tu kwenye nyumba yao ya chumba kimoja na sebule utaona picha kubwa ukutani ambayo wanadai ilikuwa ya Bwana Omari ambaye aliuawa kinyama na askari wa CCM.

  Akisimulia kuhusu kisa hicho, Bi Mwajuma alisema." Ilikuwa kama saa saba usiku, na tayari tulikuwa tumeshalala kwani kulingana na hofu iliyokuwa imetanda Zanzibar kila mtu aliwahi kujifungia ndani hasa kwa kuogopa askari waliokuwa wametanda kila mahali. Pamoja na kukosa usingizi siku hiyo, tuliamshwa na kishindo kikubwa mlangoni pamoja na sauti za ukali zilizotutaka tufungue mlango."

  "Binti zetu watatu walikuwa sebuleni na walikuja haraka kugonga mlango wa chumbani kwetu. Mume wangu alifungua mlango haraka na kutoka kuelekea sebuleni wakati binti zetu waliingia haraka chumbani kwa hofu ya wale waliokuwa wakigonga nje."

  "Nilimsikia mume wangu akiwauliza walikuwa wakitaka nini usiku huo, lakini walisisitiza tufungue au waanze kumimina risasi ndani ya nyumba." "Baada ya mlango kufunguliwa, waliingia watu zaidi ya kumi na kumwamuru mume wangu akae chini."Walianza kupekua kila mahali na kubeba kila walichokiona kinawafaa, kuanzia vito vya dhahabu pamoja na pesa kidogo tulizokuwa nazo. Katika kipindi chote hicho binti zetu walikuwa wameingia uvunguni mwa kitanda chetu."

  Tulipowaliza walikuwa wakitafuta nini, walijibu kuwa wanawatafuta waliohusika na maandamano, na mume wangu alikuwa mmoja wao. Jitiada za mume wangu kujaribu kuwaeleza kuwa yeye hakuusika na maandamano hazikuweza kufua dafu." "Walipomaliza kupekua mmoja wao aliwaona binti zangu uvunguni na kuwaamuru watoke na waandamane nao. Nilijaribu kuwaomba wawaache binti zangu ,lakini
  walisisitiza kwamba lazima waende nao. Mume wangu alionekana kuchukizwa na kitendo cha mmoja wa askari hao kumpapasa mmoja wa binti zetu mbele yetu. Aliwaambia kuwa haiwezekani kuwanyanyasa kijinsia binti zake mbele yake. Aliwaambia heri wamuue kuliko wafanye hayo mbele yake. Alimshika askari aliyekuwa anamvua nguo binti yetu na kuanza kungangana naye. Katika harakati hizo askari alifyatua risasi mbili na mume wangu alianguka chini, huku akivuja damu nyingi sana."

  "Haraka haraka waliwatoa binti zangu nje na kuniacha mimi na mume wangu ndani. Hawakwenda mbali, kwani niliwasikia wakisemezana hapo nje. baada ya muda
  kidogo niliwasikia binti zangu wakilia kwa sauti na wakiniita mama mama. Sikuweza kutoka kwani nilikuwa nikijaribu kumsaidia mume wangu ambaye kwa wakati wote
  huo alikuwa anavuja damu nyingi sana lakini alikuwa hajafa. Nilitumia mashuka kujaribu kuzuia damu lakini wapi. Alikuwa anavuja damu kama maji ya bomba."

  Nayakumbuka maneno ya mume wangu kabla hajapoteza fahamu. alisema: " Wako wapi wanangu?" Nikamwambia wale askari wameenda nao. Akasema CCM waliiba kura na sasa wamewaiba binti zangu. hata kama nitakufa leo lakini uchungu ninaousikia waambie waislamu wote duniani ili walipize kisasi hata kama ni baada ya miaka mia moja. Waambie binti zangu kama watarudi wakiwa hai kwamba ninawapenda kama baba yao, na nimejitahidi kuwazuia askari wa CCM wasiwadhuru na yaliyonipata waliyaona. Mungu ambaye hapokei rushwa atamhukumu Mkapa na serikali yake ya mabavu ambayo inawatendea wananchi wasio na hatia madhambi ya jinsi hii."

  Alipomaliza maneno hayo, alipoteza fahamu na hakupata tena fahamu mpaka tulipomzika.

  "Binti zangu walirudi karibu kunapambazuka, na waliyonielezea ni aibu hata kuyasema hapa. Sasa hivi ninavyozungumza binti zangu wawili wamepimwa na kukutwa na virusi vya ukimwi. Sijui kama wanaweza kuwasamehe askari waliowabaka kwa zamu, na mbaya zaidi sijui kama wanaweza kuisamehe serikali ya CCM inayoongozwa na Mkapa." Alimaliza mama huyo aliyekuwa anatoa machozi wakati wote wa mahojiano.


  -----
  Mwandishi wa habari BBC
   
 2. J

  Joyceline JF-Expert Member

  #2
  Oct 15, 2009
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 1,010
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Acha udini wewe? uko st. nyerere ni wapi?
   
 3. Gavana

  Gavana JF-Expert Member

  #3
  Oct 15, 2009
  Joined: Jul 19, 2008
  Messages: 17,989
  Likes Received: 1,558
  Trophy Points: 280

  nakubali mimi nina udini , yaelekea wewe hujasoma thread ya hao wanaotaka kumfanya nyerere saint kwani sikuona mchango wako au kufanywa nyerere saint sio udini

  samahani ikiwa nimekugusa pabaya
   
 4. babukijana

  babukijana JF-Expert Member

  #4
  Oct 15, 2009
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 4,816
  Likes Received: 1,155
  Trophy Points: 280
  kha!nyerere anahusika vipi hapa we mtu?huu ni upuuuz wa mwisho
   
 5. Gavana

  Gavana JF-Expert Member

  #5
  Oct 15, 2009
  Joined: Jul 19, 2008
  Messages: 17,989
  Likes Received: 1,558
  Trophy Points: 280

  ama kweli vijana mmenyeshwa maji ya bendera na damu ya yesuuuu?????

  Hivi huelewi kuwa 1995 aliyekwenda zanzibar kumweka salmini amuri ni nani?????

  Hii ccm iliundwa na nani?????

  Mkapa aliwekwa na nani?????


  Hili jeshi aliyeliunda na kuliimarisha ni nani?????


  Biblia inasema by their fruits you will recognise them

  haya ndiyo matunda yaliyopandwa na saint au baba au father nyerere ndiyo tunayashuhudia
   
 6. M

  Msindima JF-Expert Member

  #6
  Oct 15, 2009
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,018
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Gavana chonde chonde,

  Hivi kichwa cha habari wenzangu mmekielewa? habari iliyopo ndani tofauti na kichwa cha habari,nini lengo la hicho kichwa cha habari hii?

  Hiyo nilio-highlight na red ina uhusiano gani na hii habari? unaanza kashfa? Damu ya Yesu imekujaje hapa,naona kuna ambalo unalitafuta,pole pole na mada zako unazozianzisha hapa.

  maswali yako yote uliyouliza hapa hayana mantiki yoyote,na yanadhihirisha jinsi ulivyokuwa na uwezo mdogo sana wa kuelewa mambo.
   
 7. m

  mchajikobe JF-Expert Member

  #7
  Oct 15, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 2,402
  Likes Received: 684
  Trophy Points: 280
  Sasa wewe mwenzetu mbona hueleweki,kuna uhusiano gani na mtakatifu Nyerere?au umeandika tuu ili upate watu wa kuperuzi hii thread yako, mi naona lengo lako lilikuwa ni kutuletea matabaka ya kidini tuu,Jiheshimu uheshimiwe!!
   
 8. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #8
  Oct 15, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  Upupu tupu!!
   
 9. Gavana

  Gavana JF-Expert Member

  #9
  Oct 15, 2009
  Joined: Jul 19, 2008
  Messages: 17,989
  Likes Received: 1,558
  Trophy Points: 280

  nyinyi ni vijana wapya hivi hili jeshi na polisi na ccm tanzania vilianzishwa na nani????????

  Hivi hujui kuwa nyerere ndiye alimweka salmini zanzibar kwa nguvu???????


  Mbona mnakuja juu mnashindwa kufikiri,,,,,,
   
 10. Gavana

  Gavana JF-Expert Member

  #10
  Oct 15, 2009
  Joined: Jul 19, 2008
  Messages: 17,989
  Likes Received: 1,558
  Trophy Points: 280

  upupu kwani waliokufa na wanaoendelea kuumia hawajakuhusu
   
 11. Gavana

  Gavana JF-Expert Member

  #11
  Oct 15, 2009
  Joined: Jul 19, 2008
  Messages: 17,989
  Likes Received: 1,558
  Trophy Points: 280
  mimi sishindwi kuandika tabaka la dini , naona mnapayukwa hovyo tu kwa kumtaja baba yenu au hivyo vyeo mnavyotaka kumpa vya usaint , si mpeni tu vyeo vyovyote kwani niliwakataza?????
   
 12. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #12
  Oct 15, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Gavana,
  Kwa kuwa wewe umezaliwa na baba yako, basi unapolala na mkeo maana yake Baba yako amelala na mkeo?
   
 13. Gavana

  Gavana JF-Expert Member

  #13
  Oct 15, 2009
  Joined: Jul 19, 2008
  Messages: 17,989
  Likes Received: 1,558
  Trophy Points: 280


  BWANA YESU ANASEMA

  mathayo 7:17-18  7:17 Basi, mti mwema huzaa matunda mema, na mti mbaya huzaa matunda mabaya.

  7:18 Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mbaya hauwezi kuzaa matunda mema.  MIMI NIMEWALETEA MATUNDA YA NYERERE BAADA YA KUTUMIA HILO JESHI LAKE KUWAWEKA VIONGOZI WASIOTAKIWA NA WANANCHI KULE ZANZIBAR
   
 14. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #14
  Oct 15, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Wanyamwezi tunasema....
  "Moto huzaa MAJIVU".

  Hata kwenye biblia imeandikwa, Mpanzi alipoenda kupanda mbegu, nyingine ziliangukia kwenye Mwamba zikaliwa na ndege, nyingine zikaangukiwa kwenye magugu na nyingine zikaangukia kwenye udongo mzuri zikazaa...... Sasa Nyerere yeye alipanda tu, na kapanda wengi. Walikoangukia hilo si kosa lake..........

  Narudia tena: Maadamu baba yako kakuza wewe, basi unapolala na mkeo ni kuwa baba yako kalala naye? Baba akija na kutembea na mkeo itakuwa sawa tu kwani wewe na baba ni WAMOJA? Nyerere anaenziwa na Mkapa anasubiriwa apandishwe mahakamani....
   
 15. Gavana

  Gavana JF-Expert Member

  #15
  Oct 15, 2009
  Joined: Jul 19, 2008
  Messages: 17,989
  Likes Received: 1,558
  Trophy Points: 280

  huyu mkapa ndiyo hayo matunda ya nyerere.

  Pia kule zanzibar kulazimisha watu kwa nguvu kumuweka salmini ambaye hakushinda uchaguzi ilikuwa ndiyo chanzo cha ile mbegu , nyerer hakutupa ovyo mbegu maana ilikuwa akubaliane na matokeo halali ya uchaguzi sio kujitia kimbele mbele na matokeo yako mpaka leo wananchi wa zanzibar wanateketea sababu ni mtu huyu na siasa zake .


  HAPA HAKUNA HADISI ZA KINYAMWEZI KUNA WATU KUTEKETEA NA HUU UDHALIMU WA NYERERE
   
 16. M

  Msindima JF-Expert Member

  #16
  Oct 15, 2009
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,018
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135

  Oooooh poor Gavana,
  kama lengo lako lilikua kuanzisha thread inayomhusu Nyerere ungeanzisha tu,nakushangaa sana yaliyopo kwenye thread yako ni tofauti na ambayo unayoandika,uliweka hicho kichwa cha habari ili watu wasome na watoe comments halafu uchomekee issue za udini eeee,akili yako chafu sana,nakuonea huruma,huyo aliekutuma kamwambie hivi wale watu kule nilikopeleka ile thread wamewaona kuwa hamna akili.
   
 17. Gavana

  Gavana JF-Expert Member

  #17
  Oct 15, 2009
  Joined: Jul 19, 2008
  Messages: 17,989
  Likes Received: 1,558
  Trophy Points: 280
  unashangaa kitu gani au kumuandika nyerere saint ndio kitu kinachokustjaabisha wala hukushangaa kuuliwa hawa watu wasio na hatia na wale w3alionajisiwa ama kweli udini umewaingia nyinyi vibaya sana
  akili yangu chafu maana hawa waliouliwa kwako wewe ni ngurue au vipi????
   
 18. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #18
  Oct 15, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Hii Thread haina MPANGO. Kuendelea kuwa hapa ni sawa na kubishana na ...... Watu hawataona tofauti. I'm off.....
   
 19. N

  Natasha Ismail JF-Expert Member

  #19
  Oct 15, 2009
  Joined: Jul 14, 2008
  Messages: 511
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 60
  GAVANA,Wewe una matatizo yoyote ya akili?
   
 20. Gavana

  Gavana JF-Expert Member

  #20
  Oct 15, 2009
  Joined: Jul 19, 2008
  Messages: 17,989
  Likes Received: 1,558
  Trophy Points: 280
  kwa kumuandika baba yenu vitendo vyake alivyovifanya vya kuwaweweka maraisi walioleta na wanaoleta maafa na wasiotakiwa kule zanzibari , pia kunajisiwa watu na wengine kuuliwa ama hapa kwa kweli mimi sina akili


  , mwenye akili ni wewe na hao mnaoona kuuliwa watu wasio hatia na kunajisiwa watu kuwa ni kama kuuwa nguruwe

  hayawaumi
   
Loading...