Mauaji ya Kimbari ni nini hasa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mauaji ya Kimbari ni nini hasa?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Remote, Jun 1, 2011.

 1. Remote

  Remote JF-Expert Member

  #1
  Jun 1, 2011
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 14,875
  Likes Received: 1,561
  Trophy Points: 280
  Wadau naomba msaada wenu kuhusu mauaji ya kimbari "kimbari" inamaansha eneo/mahali huko Rwanda au ni mauaji ya aina ile ambayo yaliuwa watu wengi?
   
 2. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #2
  Jun 1, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Hapana. Kimbari ni neno la Kiswahili lenye kumaanisha "genocide." Badala ya kusema mauaji ya halaiki, kama ambavyo baadhi ya radio zimekuwa zinatumia, kimbari inamaanisha genocide.
   
 3. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #3
  Jun 1, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Kuna neno tunasema "mbari" yaani "ukoo au famili". Kwa wanaosoma maandiko wanakuta na kile tunachokiita "mbari ya Daudi" yaani familia au ukoo wa Daudi. Katika upana wake inamaanisha zaidi watu wa familia moja. Sasa wanaposema mauaji ya ki-mbari maana yake watu wa jamii moja wanalengwa kuuawa na hapa ndipo neno "genocide" linapokaribiana sana na Kimbari kuliko neno "halaiki".  Neno Geno-cide linaunganisha maneno mawili ya Kigiriki na Kilatini (genos - ambalo humaanisha uzao, jamii ya watu wa asili moja, vinavyofanana n.k). Unakutana na neno hilo unapotumia "genome", "geneology" na tunapata kwenye "genus" ya Biolojia ambavyo vyote vinahusiana na "vinavyofanana au vyenye asili moja". La Kilatini ni hilo 'cidius' ambayo inahusiana na "kukata au kuua" na ndio tunaliona kwenye insecticides, infanticides, genocides. Hivyo, genocide - ni kuua watu wenye asili moja lakini sasa hivi linatumika kuonesha mauaji ya makusudi ya jamii ya watu wenye asili moja katika wingi wao ikiwa na lengo la kuondoa na kufutilia mbali jamii hiyo ya watu. Na neno hilo lina maana hata ya kisheria sasa na hutumiwa kwa uangalifu siyo kila mauaji ya halaiki (mass murder) ni ya kimbari.  Kama alivyosema Jasusi hapo juu radio nyingi zimekuwa zikielezea mauaji ya Rwanda kuwa ni ya "halaiki"; japo ni kweli kwa sababu watu wengi waliuawa kwa wakati mmoja mauaji yale yalikuwa ni ya kujaribu kufutilia mbali jamii fulani ya watu na hivyo yanaingia kwenye level ya mauaji ya kimbari.  Hivyo, "kimbari" si mahali ambapo mauaji ya Rwanda yalitokea bali ni aina ya mauaji ya Rwanda yaliyotokea.

  MM
   
 4. kipindupindu

  kipindupindu JF-Expert Member

  #4
  Jun 1, 2011
  Joined: Dec 16, 2010
  Messages: 1,051
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  ubarikiwe mkuu!nakuheshimu sana.
   
 5. babukijana

  babukijana JF-Expert Member

  #5
  Jun 1, 2011
  Joined: Jul 21, 2009
  Messages: 4,811
  Likes Received: 1,146
  Trophy Points: 280
  asante sana lakini mimi nimeipenda hii chini

  HTML:
  [COLOR="blue"]Ikawa Ahabu alipomwona Eliya, Ahabu akamwambia, Je! Ni wewe, Ewe mtaabishaji (troublemaker) wa Israeli? Naye akajibu, Si mimi niliyewataabisha Israeli bali ni wewe (speaking truth to power), na nyumba ya baba yako (Bila kuuma maneno), kwa kuwa mmeziacha amri za BWANA (mafundisho ya msingi ya taifa); nawe umewafuata mabaali (a.k.a mafisadi unaowaabudia). 1 Wafalme 18:17 Fikiria[/COLOR]
  .

  kama vile ninamuona n kwere akileta longolongo hizo in future
   
 6. f

  furahi JF-Expert Member

  #6
  Jun 1, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 947
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  kwa lugha rahisi:
  Genocide=Mauaji ya kimbari (koo/ kabila/jamii fulani)
  Masacre=Mauaji ya halaiki (Haijalishi kama ni wa koo/jamii/kabila fulani)
   
 7. S

  Senior Bachelor Member

  #7
  Jun 2, 2011
  Joined: Mar 23, 2011
  Messages: 86
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Nakubaliana na Mwanakijiji 100% kwa tafsiri alotoa ya neno "mbari" na pia mauaji ya kimbari. Aidha nakubaliana naye pia kuhusu mkanganyiko katika vyombo vya habari kuhusu mauaji ya Rwanda na genocide kwa ujumla. Pamoja na hayo naomba niongezee haya yafuatayo-kushadidia tu aliyosema mwanakijiji.

  Mauaji yako ya aina nyingi. Yale yanayohusu mauaji ya watu wengi kwa wakati mmoja yanaitwa massacre (mauaji ya halaiki). Yale yanayotokana na sababu za kisiasa huitwa assassination (mauaji ya kisiasa) e.g. yale ya Lumumba etc. Pia kuna murder (kuua kwa kukusudia) manslaughter (kuua bila kukusudia) execution (kuua kama adhabu e.g kutokana na hukumu ya kifo), suicide (kujiua mwenyewe), electrocide (kuua kwa kutumia umeme) etc. Kwa hiyo wanahabari wengi hawajali/hawajui kuhusu hizi tofauti -lkn hilo sio relevant hapa

  Sasa basi: Genocide inafall wapi?

  Kwa matumizi ya sasa neno genocide ni dhana ya kisheria zaidi na lina maana zaidi ya "mauaji ya kimbari". Yaani, mauaji ya kimbari i.e yale yanayolenga watu wa jamii/ukoo fulani i.e ethnic group ni aina moja tu ya genocide.
  Definition ya kisheria (maana genocide kwa sasa ni istilahi ya sheria) ni kuwa genocide ni mauaji yanayofanywa huku muuaji akiwa na "lengo la kuangamiza kabisa au sehemu ya " kundi fulani la watu kwa sababu ya mbari yao, imani yao ya dini, utaifa wao, au rangi yao" i.e "genocide means any of the following acts committed with intent to destroy, in whole or in part, a national, ethnical, racial or religious group".(See Article 6 of the Rome Statute for the International Criminal Court au pia the Genocide Convention (1948)). Hay makundi 4 huitwa "protected groups". Kuestablish lengo la muuaji ( genocidal intent) ni muhimu sana sana. Vinginevyo yatakuwa mauaji tu ya kawaida.

  NB 1:
  Ifahamike kuwa genocide huweza pia kufanyika kwa namna nyingine 4 zaidi ya kuua ili mradi lengo lake ni "to destroy the protected group in whole or in part". Ktk sheria ya jinai ya kimataifa namna hizo nyingine zimebainishwa na kuaainishwa kama (i) kuzuia kwa namna yoyote watu wa kundi moja kati ya hayo 4 hapo juu wasizaliane; (ii) kuwahamisha/kuwatenga watoto wa kundi hilo na kuwapeleka kwenye kundi au mahali pengine (kama Hitler alivyofanya kwa watoto wa Russia na Polland aliokuwa anawapeleka kuishi na familia za Ujerumani) kwa lengo la kuzuia kundi kuongezeka; (iii) kuwa-subject kundi husika ktk hali ngumu kwa makusudi (eg. kuwakatia food supply etc) kwa lengo la kuwafutilia mbali - kama alivyofanya Hitler kwa kuwapa chakula kidogo sana -"modest meal"- wayahudi waloshikiliwa kwenye concentration camps hadi wakafa/dhoofu sana); na (iv) hata tu kusababisha serious bodily and mental harm kwa members wa group hilo.

  Kwa hiyo basi, yale mauaji ya Rwanda yanaitwa ni ya "kimbari "kwa kuwa tu yalihusu mbari/ukoo/kabila fulani. i.e.etnic group. yaani yalilenga kuwamaliza watusi au wahutu. Yangekuwa kwa mfano yanalenga watu wa dini fulani ni dhahiri kuwa neno "kimbari" lisingetumika. Mauaji kama hayo yalifanywa tena kule Yugoslavia ya zamani dhidi ya waSerb ambao ni waislam-naamini unakumbuka kesi za kina Milosevic na huyu Miladic alekamatwa majuzi etc. Kule Ukraine(1910s) yalifanywa dhidi ya Waarmenia etc. Ninachomaanisha ni kuwa "kimbari" ni sehemu tu ya kuielezea genocide.

  NB 2:
  Tujue kuwa kuyaita ya halaiki sio sahihi sana kwa sababu sio lazima wafe watu wengi . Cha msingi ni kuprove ile "genocidal intent" na kwamba hata kama alikufa mtu 1 au 10 au 1000 au 1 million, ni kuwa aliuawa/waliuawa katika context ya "intent to destroy his group in part or in full".
  Hayo ya Kenya ya 2007/2008 kidogo yangeelekea huko kwa sababu yalichukua sura ya kuangamiza watu wa makabila fulani fulani. Lkn bado hayakuweza kuifkia uwezekano wa kuestablish "genocidal intent" ndio maana Ocampo amewashtaki kwa makosa dhidi ya ubinadamu i.e. "crimes against humanity" na sio genocide. Mauaji hayo ya Kenya yalichukua sura ya "ethnic cleansing", ambayo ni dalili kuwa genocide, tena ya aina ya kimbari, ilikuwa njiani kutokea. Fortunately, haikufikia "kiwango"

  Conclusively, genocide inaweza kuwa:
  1)Mauaji/maangamizi ya kimbari (e.g Rwanda)
  2) Maangamizi/mauaji ya kidini (eg yugoslavia) ambayo pia yamechanganyika na kimbari kwa kuwa walengwa ni wa kabila la serb ambao pia ni waislamu)
  3) Mauaji/maangamizi yanayolenga rangi (race) ya mtu
  4) Mauaji/maangamizi yanayolenga utaifa (nationaity) wa mtu.

  Mauaji ya albino sio genocide kwa kuwa albinism sio "race" bali ni biological disorder tu. sickle cell, anaemia etc. Mauaji ya wanachama wa chama fulani cha siasa hayawezi kuitwa genocide kwa kuwa kama nilivyosema awali currently there are only 4 protected groups under the law and a political group is not inclusive.

  Asanteni na samahani kwa jibu refu, tena la kisheria.
   
 8. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #8
  Jun 2, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,688
  Likes Received: 410
  Trophy Points: 180
  asanteni kwa somo hili,mmeeleweka wakuu
   
 9. m

  mwabaluhi JF-Expert Member

  #9
  Jun 2, 2011
  Joined: Oct 16, 2010
  Messages: 561
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nimekuelewa kwa ufasaha. Post nzuri sana
   
 10. T

  Torch JF-Expert Member

  #10
  Nov 14, 2013
  Joined: Aug 11, 2013
  Messages: 536
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 33
  Asanteni hata mimi nilikuwa na changanyikiwa na huo msamiati KIMBARI
   
 11. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #11
  Nov 14, 2013
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Ni mauaji yakiyotokea kijiji cha kimbari
   
 12. WISTON MWINUKA

  WISTON MWINUKA Member

  #12
  Nov 14, 2013
  Joined: Apr 29, 2012
  Messages: 82
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Nimekwenda wakati fulani kwenye makumbusho ya mauaji hayo pale kigali panaitwa KIGALI GENOCIDE MEMORIAL,kwa kweli inahuzunisha ukisimuliwa ilivyokuwa,Tumuombe mungu aitunze amani yetu.AMEN.
   
Loading...