My Son drink water
JF-Expert Member
- Nov 30, 2016
- 4,932
- 13,283
Baada ya kupewa Taarifa hii niliamua kwenda mwenyewe kushuhudia hao wajane walioachwa baada ya waume zao kuuawa kikatili kwa kosa la kufanya uvuvi haramu .
Hakuna chombo Chochote cha Habari chenye uwezo wa kuripoti hili Tukio na kikabaki salama, hakuna, na ndio maana watu hawajui ukatili unaotendwa kwenye mkoa tarajiwa kanda ya ziwa.
Karibia na Ziwa kuna mbuga ya wanyama (iliyozinduliwa na wanyama kibao, wakiwemo Twiga na Simba kupelekwa huko).
Wale wavuvi wakisha kurupushwa ziwani na askari pori huwa wanakimbilia msituni ili kujiokoa wasikamatwe kwa sababu hawana access ya kutorokea zaidi ya msituni, lengo la wale askari ni kuwafanya wakimbilie msituni ili waliwe na Simba na ndicho ambacho hutokea.
Wanaokamatwa hupigwa risasi baada ya kutundikwa msalabani Kama Yesu kwa mateso makali.
Ananieleza X mvuvi aliyenusurika nikiwa nyumbani kwake pamoja mjane aliyekuwa akilia muda wote wa simulizi hii ya kweli, na ya kutisha.
Maelezo yote nime record, na kwa sababu za kiusalama siwezi kuyaweka hapa kwa sababu sauti yangu itasikika ikiwahoji, sitaki kumfuata Azory Gwanda.
Nilipata Taarifa hizi nikiwa Kisumu Kenya na kwa kuwa nilipanga kula Christmas Tanzania nikaamua niende kupiga kambi eneo hilo lenye majasusi wengi wa Serikali, nilitumia mbinu exceptional kupata hizi Taarifa.
Najua hii inaweza isidumu humu kwa sababu ya Udikteta wa Habari uliopo Tanzania, lakini kabla ya kuifuta naiomba Management ya JamiiForums itume kikosi kazi cha siri ili kwenda huko kupata Taarifa hizi, watumie ujasusi kuzipata wahakikishe hawajulikani kwa sababu adhabu ni kupotezwa kama Azory Gwanda.
Nilifikia Guest House yenye hadhi duni sana na mwonekano wangu nilivyojiweka haikuwa rahisi kunistukia lengo langu.
Wanawake wamebakia wajane, watoto wanateseka na njaa.
Mungu iponye Tanzania
Sent using Jamii Forums mobile app
=====

No research no right to speak, awali nilihofu kwamba pengine hii mada ingefutwa humu haraka sana baada ya kuiona bado inapumua naendelea na Part -2 ya Mauaji ya kikatili wanayofanyiwa wavuvi kanda ya ziwa, eneo la Chato Mganza kwenye kisiwa cha Rubondo.
Nina ushahidi 100% na Tayari hii Habari naiandaa ili kuifikisha kwenye vyombo vya Habari vya kimataifa ili Dunia ijue Tanzania ilikofikia kwa sasa.
Mandela aliwahi kuwaambia makaburu kuwa, "Huwezi kuua sauti zote, kila sauti moja unayoiua zinafufuka sauti elfu moja zaidi ".
Simulizi ya X inaliza na kuumiza mno, anadai kuwa wauaji wale si askari wa wanyama pori bali ni wanajeshi anaodai wana nasaba na taifa la Rwanda.
"Tumekamatwa mara nyingi mno na Watanzania wenzetu askari pori lakini walikuwa wakituachia na kutueleza kuwa tusirudie tena, lakini tulipokamatwa na wale wanajeshi, tulipelekwa sehemu zenye maiti nyingi na kisha tukaambiwa kuwa Hao ndio wenzetu waliopotea, kwa sababu mimi sijaoa Niliambiwa sina hasara kwa hiyo nishuhudie kwanza mauaji ya wenzangu ".
"Moto ulikokwa chini na wenzangu wakaambiwa wanabanikwa Kama jinsi ambavyo wao wamekuwa wakibanika Samaki, waliuawa huku naona kwa macho yangu, kisha nikaambiwa nenda kasimulie wenzako "
X anadai aliambiwa magereza yamejaa hivyo kuna maagizo toka juu wamalizwe kila wanapokamatwa.
Analia akidai Kama watu hawaamini basi waende wakachunguze na kubaini ukweli.
Habari hizi zimetapakaa pote lakini hakuna Chombo chochote cha Habari chenye uthubu wa kuandika.
Kwa sababu Damu ya mtu haipotei bure ni lazima Dunia ijue,na Mungu atajitwalia kisasi mwenyewe.
Hivi kosa la kuvua Samaki bila kibari adhabu yake ni kifo cha kikatili kiasi hicho?
Eeeh Mungu, sema na Tanzania.
Sent using Jamii Forums mobile app