Mauaji ya kikatili kanda ya Ziwa

Mkuu,
Kubakia kimya hakumaanishi kuwa tuko salama. Dawa si kunyamaza, dawa ni kupigania uhuru wa watu.
Mimi ninaekueleza haya nakueleza kwa uzoefu nilioupata!
Ngoja niwape siri, kati ya walioathirika kwenye yale maandamano ya Pemba na sisi tumo. Pamoja na kwamba mzee wetu (baba) alikuwa moga sana kwa sababu alikuwa ni mstaafu wa cheo fulani serikalini kikubwa serikalini. wakati watu wanahamisisha kuandamana, mzee wetu alitukataza tusishiriki, akatukemea sana, akatuambia hakuna ruhusa mtu yoyote kutoka kwa kuhofia kwamba watakaotoka ndio wataumizwa.
Ukweli ni kwamba tulitii amri ile na kujifungia ndani wakati wenzetu wengine wakiandamana nje. Nyumba zetu ziko barabarani, tuliskia ghasia na milio ya risasi nje, lakini hatukuthubutu hata kuchungulia dirishani!
Hata hivyo hatukusalimika! walikujua askari wakavunja milango ya nyumba zetu, kitu cha mwanzo walichofanya walimchukuwa mzee wetu! yule yule alietukataza tusitoke kuungana na wenzetu. Walimuweka ndani mzee mpaka walipomuachia hakuunga tena! Mzee wetu leo hafiki hata msikitini!
Fundisho ni kwamba ukimya haukupi guarantee ya kinga mkuu!
 
Hahaha kuandika hivyo kila mtu anaweza, kila kitu siri, sasa ukweli wa habari hii uko wapi, eneo X, muongeaji X, Muandishi X, Ushahidi wote X.

Ungeweka hata picha ya eneo husika, au ushahidi wa hata mjane mmoja, au Jima hata moja la victim athibitike aliuwawa kwa njia hiyo, ithibitishwe iko hivyo, eneo hilo ili kuwe na chembe hata ndogo ya ukweli.

Lakini hivi, ni sawa na kusema watu kanda ya ziwa hufa kila siku, bila kusema ni kwa ajali, kipindupindu au HIV.

Muandishi mchunguzi, tupe hata punje yaukweli mengine tuthibitishe wenyewe.

Wewe huko unaweza kuwa umekwenda kwa siri, siku moja. Wapo humu wanaishi huko, wangeweza ku prove unachokisema kwa kupata japo hint tu, hata jina moja kati ya hao wajane,au jina moja tu kati ya waliouwawa.

Bila hivyo sioni kwanini ulete habari hii hapa?! Lengo lako tupate habari au kutuficha habari?!

Mwaga vitu acha woga ubapoleta Jabari. Usitupe audio, tupe hata picha.

Siri mwanzo hadi mwisho, ulitaka tuelewe nini?!
 
Tuambie Azory Gwanda yuko wapi na Ben Saanane na Kwanini serikali inaogopa kuleta wachunguzi huru, iko siku yenu nyie wauaji

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu naona unakuja na black propaganda kuichafua serikali ya Magufuli na vyombo vya ulinzi kwa kuvipaka matope ya mauaji..

Kama umeshindwa kuleta hiyo audio na unathibitisha kuituma kwenye vyombo vya habari vya nje huoni kuwa wewe ni muongo?

Kuna utofouti gani ukiweka hiyo audio hapa ndani kuthibitisha maandishi uliyoandika na kuituma katika vyombo vya habari...

Jaribu kuwa na hofu ya Mungu ndani mwako, kwa maelezo yako inaonesha ni kwa jinsi gani ulivyo muongo...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii habari haina chanzo cha uhakika. Lakini nawashangaa vijana mnavyotiririka. Inasikitisha. Mtu anaandika jambo ww bila kuwa na uhakika nalo unaandika kwa chuki na ghadhabu bila kufikiri mara mbili. Lini mtakuwa vijana. ? Kwanza toka lini Tanzania tuna majasusi? Polisi wanyama pori ni majasusi? Je jasusi ni nani? Unataka kusema jasusi huwa anatumwa kwa wananchi choka mbaya?

2.Naombeni mseme ni hifadhi gani hiyo mwanza iliyowekwa na kutengwa kuwa hifadhi ya wanyama pori. Nimekaa mwanza sikumbuki. Labdanum mnaokaa mwanza mtuambie kama kuna mwalo, kisiwa kilicho karibu na hifadhi ambacho kinawavuvi

3.huyu mtu ametokea Kenya kisumu ndipo kaja Tz. Huyu ni mtanzania kweli? Eti alipopata habari akaenda kupiga kambi. ??kwangu mimi huyu si mtanzania. Na watanzania hasa vijana mtachanganywa na kuchochewa na mahawayani kama hawa.

4. Uvuvi haramu iliendeshwa kwa operations nafikiri zaidi ya mbili na zote nilikuwepo Irugwa kisiwani, busekere, upande wa mwanza na kwenye mwalo wamakoko na kisiwa cha Lukuba musoma .Najua wavuvi wanavyoreact kwenye ishu za uvuvi haramu. Hakukuwa na cases za watu kuuliwa tena kipindi kile mambo yalikuwa moto. Sasa hii ni IPI mtoa mada anayotueleza.

Aisee tuweni makini mno. Magufuli atapita lakini Tanzania itabaki. Watu kama hawa ndiyo walichafua Libya na nchi zote zisizotawalika kwa msaada wa westerners. Poor Tanzanian's
 
ikizituma marekani kunatokea nini tanzania,wewe weka hadharani tuzipime kama ni majangiri au watu wameonewa,kumbuka jangiri akimuona askari,askari haponi,ndivyo ilivyo kwa askari akimuona jangiri jangiri haponi ,ikumbukwe DRC ilishindwa kuweka askari kwenye mapori matokeo yake vita na waasi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Report ya hovyo kabisa na uchonganishi. Uandishi kama huu ni hatari sana, sema na wapi ziwa na mbuga vinakutana.
Haswaaa. Hilo ndilo nililiuliza. Mimi nimefanya biashara ya samaki na dagaa nafahamu mialo na visiwa. Aseme hapa ni kisiwa gani kinachopakana na mbuga.
Mimi niwaambie vijana wanaonyakua topic juu kabla haijafika chini wakaitafakari. Watumie basi usomi wao hata ule wa kukariri majawabu kuhoji mambo. Tanzania ya kwetu wote ikiharibika kwa sababu ya wapumbavu kama hawa tumeisha wenyewe watarudi kisumu kutucheka
 
Hii habari haina chanzo cha uhakika. Lakini nawashangaa vijana mnavyotiririka. Inasikitisha. Mtu anaandika jambo ww bila kuwa na uhakika nalo unaandika kwa chuki na ghadhabu bila kufikiri mara mbili. Lini mtakuwa vijana. ? Kwanza toka lini Tanzania tuna majasusi? Polisi wanyama pori ni majasusi? Je jasusi ni nani? Unataka kusema jasusi huwa anatumwa kwa wananchi choka mbaya?
2.Naombeni mseme ni hifadhi gani hiyo mwanza iliyowekwa na kutengwa kuwa hifadhi ya wanyama pori. Nimekaa mwanza sikumbuki. Labdanum mnaokaa mwanza mtuambie kama kuna mwalo, kisiwa kilicho karibu na hifadhi ambacho kinawavuvi
3.huyu mtu ametokea Kenya kisumu ndipo kaja Tz. Huyu ni mtanzania kweli? Eti alipopata habari akaenda kupiga kambi. ??kwangu mimi huyu si mtanzania. Na watanzania hasa vijana mtachanganywa na kuchochewa na mahawayani kama hawa.
4. Uvuvi haramu iliendeshwa kwa operations nafikiri zaidi ya mbili na zote nilikuwepo Irugwa kisiwani, busekere, upande wa mwanza na kwenye mwalo wamakoko na kisiwa cha Lukuba musoma .Najua wavuvi wanavyoreact kwenye ishu za uvuvi haramu. Hakukuwa na cases za watu kuuliwa tena kipindi kile mambo yalikuwa moto. Sasa hii ni IPI mtoa mada anayotueleza.
Aisee tuweni makini mno. Magufuli atapita lakini Tanzania itabaki. Watu kama hawa ndiyo walichafua Libya na nchi zote zisizotawalika kwa msaada wa westerners. Poor Tanzanian's
hifadhi ya Burigi chato

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waziri wa uvuvi ni mmoja wa watu wakatiri kabisa nchini Tanzania , na mtu wa kanda hiyohiyo , anaitwa Mpina ( kwa kinyakyusa maana yake Yatima )
Hata kwa Kisukuma mkuu maana yake ni hiyo hiyo! Kumbuka mkuu kalisifiwa ma mkulu kwamba ni ka kichaa kama yeye!
 
Haswaaa. Hilo ndilo nililiuliza. Mimi nimefanya biashara ya samaki na dagaa nafahamu mialo na visiwa. Aseme hapa ni kisiwa gani kinachopakana na mbuga.
Mimi niwaambie vijana wanaonyakua topic juu kabla haijafika chini wakaitafakari. Watumie basi usomi wao hata ule wa kukariri majawabu kuhoji mambo. Tanzania ya kwetu wote ikiharibika kwa sababu ya wapumbavu kama hawa tumeisha wenyewe watarudi kisumu kutucheka
Ww ushaitafakari au? maana usikatae wahenga walisema kisemwalo lipo kama halipo laja Kuna mtu kasema yupo maeneo ya Geita na kadai habari hii ni kweli so kila mtu afanya uchunguzu kwa namna yake ili kuondoa ukakasi wa habari hii kama ni kweli au la, kikubwa mleta hoja kaleta habari kutujulisha kwamba Kuna kitu cha namna hii ndani ya Tz

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kikulacho siku zote ki nguoni mwako. Majirani zetu wanatumezea mate mno amini ninachosema. Kenya haina vita vya bunduki lakini wana baguana kwa makabila. Makabila hawana ardhi walishaiuza kwa wachache. Katika ukanda huu wa afrika mashariki tumewaacha mbali wenzetu kwa kila kitu mpaka kuzaana. Sasa wanatamani tupigane tuvurugane. Ila niwahakikishie maharamia hao kwamba matatizo yetu tutayatatua wenyewe . Kama tatizo liko polisi tutasawazisha, kama liko kwa raisi ataweka mambo sawa. Kama vile ambavyo Mbowe alisimama na kutaka maridhiano ya amani ndivyo hivyo hivyo itakavyokuwa. Kwasababu kwa asili yetu sisi watanzania ni watu wenye hekima na tumeishi tukivumiliana na kuchukuliana.
Halafu kwa Tanzania wenye nia ovu watasubiri sanaaaaaaaaa mpaka watachokaaaaa kama ni kuzimezea mate rasilimali zetu mpaka mate yawakauke.....hiyo kitu imeasisiwa.
 
Ww ushaitafakari au? maana usikatae wahenga walisema kisemwalo lipo kama halipo laja Kuna mtu kasema yupo maeneo ya Geita na kadai habari hii ni kweli so kila mtu afanya uchunguzu kwa namna yake ili kuondoa ukakasi wa habari hii kama ni kweli au la, kikubwa mleta hoja kaleta habari kutujulisha kwamba Kuna kitu cha namna hii ndani ya Tz

Sent using Jamii Forums mobile app
Kasema bugiri chato. Sijui kuhusu huko. Kwanini mtoa mada asitupie hicho alichorekodi
 
Back
Top Bottom