Mauaji ya Dr Mvungi: Mtuhumiwa akiri kushiriki kwa malipo ya Tsh.30,000

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
94,127
164,538
Mshtakiwa Paulo Mdonondo anayetuhumiwa na wenzake 6 kumuua aliyekuwa mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Mpya, Dkt. Sengondo mvungi, anadai alishiriki katika tukio na alilipwa ujira wa Sh 30,000 kwa kazi aliyofanya.

Hayo yalibainika jana katika Mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam wakati Wakili wa Jamhuri, Patrick Mwita aliposoma ushahidi wa mashahidi 30 wanaotarajiwa kutoa ushahidi katika kesi hiyo Mahakama Kuu.

Mwita alidai mshtakiwa Paulo alipohojiwa Polisi, alikiri kushiriki katika tukio hilo na kwamba kazi yake ilikuwa kulinda majirani wasifike kutoa msaada kwa Dkt. Mvungi wakati uvamizi ukifanyika.

Inadaiwa mshtakiwa huyo alikaa nje akiwa na mawe kuzuia majirani, alifanikiwa na akalipwa Sh 30,000 na tukio lilipomalizika alienda kupanda daladala kuelekea katika shughuli zake Kariakoo.

Chanzo: Mtanzania
 
Haya mambo ya sheria hayatabiriki! Si ajabu aliminywa pumbu akaamua kusema hivyo kujiokoa. I am sure atakana statement hiyo mahakamani!

"Where a confession is retracted or repudiated and where there is no evidence to corroborate the confession, the trial court should conduct a trial within a trial (inquiry ) to ascertain the legality of the confession and before it admits that confession in evidence, without doing so the act results in fundamental and incurable irregularity"
 
Well said counsel
 
Nani alimlipa?
 
Hata yule jamaa aliesema alimuona scopion juzi kasema aliambiwa aseme hivo
 
Haya mambo ya sheria hayatabiriki! Si ajabu aliminywa pumbu akaamua kusema hivyo kujiokoa. I am sure atakana statement hiyo mahakamani!

"Where a confession is retracted or repudiated and where there is no evidence to corroborate the confession, the trial court should conduct a trial within a trial (inquiry ) to ascertain the legality of the confession and before it admits that confession in evidence, without doing so the act results in fundamental and incurable irregularity"
100%
 
Sishangai hata,, mbona huko Malaysia kuna mdada kalipwa $100 tu kwa kumuwekea sumu ya mauaji ndugu yake Kim, na ilikuwa kazi hatari kupitiliza. Binadamu wengi wana mapungufu au kutumiwa kimtego bila kujijua unayofanya yana madhara kiasi gani.
.inawezekana ni kweli kabisa kashiriki kwa Tsh.30000/-; wala sitashangaaa..
 
Atakuwa teja huyo!! Unapewaje jukumu la hatari namna hiyo kwa Tsh 30,000? Tanzania ni nchi yenye watu wenye upeo mdogo kupita nchi zote duniani.
waliomuua Mvungi wanajulikana ni wale waliokuwa wanahofu ya misimamo yake juu ya rasimu ya warioba.
 
Atakuwa teja huyo!! Unapewaje jukumu la hatari namna hiyo kwa Tsh 30,000? Tanzania ni nchi yenye watu wenye upeo mdogo kupita nchi zote duniani.
Uko sawa kabisa. Mateja ni tishio la usalama wa raia. Makonda alikuwa sahihi kuyasweka lupango. Teja liko tayari kufanya cho chote ili mradi lipate pesa ya kupata misokoto yake ya madawa.
 
Back
Top Bottom