Mauaji ya Bi. harusi Anni, nchini Afrika Kusini

Mauaji ya Bi. harusi Anni, nchini Afrika Kusini

RUCCI

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2011
Posts
1,702
Reaction score
1,716
_68918892_dewani.jpg
Shrien Dewani Na Marehemu mke wake Anni siku ya harusi yao

BAADA ya kutua katika uwanja wa kimataifa wa Cape Town nchini Afrika Kusini, Novemba 7, mwaka 2010, wanandoa Shrien Dewani na Anni Dewani walipanda ndege ndogo kuelekea mbuga ya wanyama ya Kruger.

Wanandoa hao walikwenda nchini humo kwa ajili ya fungate baada ya kufunga ndoa ya kimila ya kihindu, Oktoba 29 mwaka 2010 huko Mumbai nchini India.

Walikaa katika mbuga hiyo ya wanyama ya Kruger kwa siku tano na Novemba 12 mwaka 2010, walirudi jijini Cape Town na waliposhuka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Cape Town, walipanda teksi aina ya VW Sharan, iliyokuwa ikiendeshwa na dereva aliyejitambulisha kwao kwa jina la Zola Robert Tongo hadi katika hoteli ya kimataifa ya nyota tano ya Cape Grace.

Ilipofika jioni wanandoa hao waliondoka na yule dereva aliyewaleta hotelini hapo, Zola Tongo hadi katika mji wa Gugulethu uliopo kilomita 15 kutoka Jiji la Cape Town ambako kuna mghahawa maarufu kwa nyama choma, unaoitwa Mzoli ambao ni kivutio kwa watalii wengi wanaotembelea Cape Town. Waliufahamu mghahawa huo kupitia jarida la mpishi maarufu nchini Uingereza, Jamie Oliver.

Baada ya kupata nyama choma walisafiri hadi eneo la ufukwe la Strand kiasi cha kilomita 50 kusini mashariki mwa Cape Town, kwa ajili ya kupata mlo wa jioni. Walipomaliza kupata mlo wa jioni waliondoka katika eneo hilo na kuzunguka katika viunga vya ‘uswahilini' ili kuona mazingira ya uswahilini katika nchi hiyo ya Afrika Kusini.

Ni wakati walipokuwa katika viunga hivyo vya uswahilini ndipo taxi yao ilipotekwa nyara na wanaume wawili waliokuwa na bastola.

Majambazi hao walimtupa chini dereva wa gari hilo na kisha wakaondoka na wanandoa hao huku wakiwa wamewaelekezea bastola nakuanza kuzunguka nao katika viunga hivyo vya uswahilini. Waliwaambia kwamba, hawana nia ya kuwadhuru bali wanahitaji hilo gari. Baada ya kama dakika 20, wakiwa wametembea umbali wa kilomita 18 kutoka katika eneo walilotekwa, majambazi hayo yakiwa yamemuelekezea bastola Shrien, walimrusha kupitia kioo cha nyuma na kumtupa nje ya gari hilo huku gari hilo likiwa katika mwendo.

Shrien aliwasiliana na polisi na kuwaeleza kuhusu tukio hilo na haraka sana polisi wa nchi hiyo walianza kutafuta gari hilo kwa helikopta.

Novemba 14, saa 1:50 asubuhi, polisi walikuta teksi aina ya VW Sharan ikiwa imetelekezwa umbali wa kilomita 3.2, nje ya mji wa Khayetisha. Ndani ya teksi hiyo walikuta Anni Dewani akiwa amekwishauawa. Mwili wake ulikutwa na michubuko kuashiria kwamba alipigwa, kabla ya kuuawa kwa kupigwa risasi moja shingoni. Silaha iliyotumika kufanya mauaji hayo ni bastola ya MM 9, aina ya Caliber.

Baadaye polisi walibainisha kwamba saa ya mkononi aliyokuwa ameivaa Anni Dewani aina ya Giogio Armani, vito vya thamani alivyokuwa amevaa, mkoba wake na simu ya mkononi aina ya Blackberry vilikuwa vimetoweka na iliaminika kwamba vitu vyote hivyo vilikuwa vimeibwa.

Je, huyu Anni Dewani ni nani?

Labda, kabla sijaendelea na mkasa huu, unaweza kujiuliza je, huyu Anni Dewani ni nani na ni kwa nini mauaji yake yalivuta hisia za watu wengi si nchini Afrika Kusini tu, bali pia vyombo vingi vya habari vya mataifa mbalimbali.

Historia ya wazazi wa binti huyu ilianzia kule nchini Uganda. Familia ya Hindocha kutoka katika kabila la Kihindu ilikuwa ikiishi nchini Uganda hadi mwanzoni mwa miaka ya 1970 walipolazimishwa kuondoka nchini humo na utawala wa kidikteta wa nduli Iddi Amini Dada, ambaye aliamuru raia wote wenye asili ya Asia waondoke nchini humo kwa kile alichodai kwamba ni wanyonyaji wakubwa na wameingiza nchi hiyo katika lindi la umasikini.

Familia hiyo ilipata hifadhi nchini Sweden na waliishi katika mji wa Mariestad, ambako ndipo binti yao huyo, Anni alipozaliwa hapo Machi 12, mwaka 1982.

Anni Hindocha kama alivyojulikana hapo awali kabla hajafunga ndoa na Shrien Dewani alikua kwa umri na kimo, alisoma na kuhitimu katika fani ya uhandisi na aliajiriwa katika Kampuni ya Ericsson.

Kwa upande wa mumewe, Shrien Dewani, naye kama Anni ametokea katika kabila la Kihindu. Alizaliwa katika kitongoji cha Westbury on Trym kilichopo katika mji wa Bristol, mwaka 1980. Alipata elimu yake katika Shule ya Bristol Grammar hadi kidato cha sita ndipo akajiunga na Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia kilichopo mji wa Manchester (University of Manchester Institute of Science and Technology (UMIST) nchini Uingereza. Alisomea taaluma ya uhasibu na kufaulu na kuajiriwa katika kampuni ya ukaguzi wa hesabu na ushauri ya Deloitte na kupangiwa kufanya kazi katika Jiji la London.

Mwaka 2005 aliacha kazi katika kampuni hiyo ili kuungana na wazazi wake kuanzisha kampuni inayohusiana na shughuli za uendeshaji wa nyumba za wazee.

Familia ya Hindocha na familia ya Dewani zimekuwa marafiki kwa miaka zaidi ya 40, na urafiki wao ndio chanzo cha watoto wao kuoana. Ni wakati Anni alipomtembelea binamu yake, Sneha aliyekuwa akiishi katika mji wa Luton ulioko Bedfordshire nchini Uingereza, mwaka 2009 ndipo alipokutana na Shrien Dewani, ambaye hata hivyo walikuwa wakiwasiliana kwa njia ya mtandao.

MTOKO wao wa kwanza ulikuwa katika ukumbi wa sanaa za maigizo wa Lyceum uliopo jijini London, Uingereza. Walikwenda katika ukumbi huo kuangalia mchezo wa The Lion King. Baada ya mtoko huo waliendelea kutembeleana mara kwa mara kati ya miji hiyo miwili yaani Bristol nchini Uingereza na Stockholm nchini Sweden, kila mmoja akimtembelea mwenzake kwa wakati wake.

Ilikuwa Juni, mwaka 2010 baada ya kupata ruksa ya wazazi wake, Shrien alimposa rasmi Anni walipokuwa nchini Ufaransa katika Hoteli ya Ritz iliyoko Jiji la Paris walikokwenda kwa mapumziko mafupi. Baada ya kukubaliwa ombi lake la uchumba, Shrien alimvisha Anni pete ya uchumba yenye thamani ya paundi 25,000 iliyokuwa na kito cha almasi kilichochongwa mfano wa uwaridi.

Siku chache baada ya Anni kuvishwa pete ya uchumba, alihamia Uingereza katika mji wa Bristol, kuishi na mpenzi wake Shrien. Akitumia jina la ukoo wa mpenzi wake (Shrean) yaani Dewani, Anni alishiriki katika mashindano ya mitindo ya mavazi katika mji huo wa Bristol na kujizolea umaarufu.

Wapenzi hao walifunga ndoa ya kimila ya kabila la kihindu, katika hoteli moja iliyoko ufukwe wa Ziwa Powai, nje ya mji wa Mumbai nchini India Oktoba 29, mwaka 2010. Wageni 500 walihudhuria sherehe hiyo iliyodumu kwa siku tano. Hata hivyo, walipanga kufanya sherehe nyingine ya kawaida mwaka 2011 nchini Uingereza kwa ajili ya marafiki ambao hawakuhudhuria sherehe ya kimila ya harusi hiyo nchini India.

Kutokana na mauaji yake, Mwili wa Anni Dewani ulipelekwa katika hospitali moja iliyoko Cape Town kwa ajili ya uchunguzi wa kitaalamu. Matokeo ya uchunguzi huo yalionyesha kwamba, alifariki kutokana na kupigwa risasi shingoni iliyojeruhi mshipa wa Artery, lakini hakunajisiwa, isipokuwa alikutwa na michubuko kwenye mapaja.

Uchunguzi zaidi ulionyesha kwamba, kabla ya Anni kupigwa risasi kulikuwa na aina ya purukushani za kujitetea dhidi ya wauaji hao ambapo pia alikutwa na jeraha jingine la risasi katika mkono wake. Ndugu wa Shrein walikwenda nchini Afrika Kusini kuungana naye katika kushughulikia suala hilo la mauaji ya mkewe.

Shrien alihojiwa polisi na akazungumza na waandishi wa habari kuhusu tukio hilo la kutekwa na kuuawa kwa mkewe.

Katika mahojiano yake polisi na pia kwa vyombo vya habari Shrien alidai uamuzi wa wao kwenda maeneo hayo ya uswahilini ambayo inadaiwa ni hatari kwa watalii wanaotembelea mji huo wa Cape Town ni wazo la mkewe, ambaye alitaka kuona mazingira halisi ya Waafrika.

Novemba 17, Serikali ya Afrika Kusini iliruhusu familia ya Shrien ichukue mwili wao kwa ajili ya mazishi baada ya kukamilika kwa uchunguzi. Mwili wa Anni Dewani ulisafirishwa hadi Uingereza kwa ndege ya Shirika la Ndege la Uingereza (British Airways) ukisindikizwa na mumewe. Mwili wa Anni ulichomwa moto jijini London katika sherehe ya mazishi ya mila za Kihindu Novemba 21, mwaka 2010. Baadaye majivu ya mwili wake yalimwagwa katika ziwa lililopo jirani na nyumbani kwao huko Mariestad nchini Sweden.

Watuhumiwa mbaroni


Kesi ya mauaji ya Anni ilijizolea umaarufu nchini Afrika Kusini na kwa sababu hiyo iliteuliwa timu ya wapelelezi wakiongozwa na mpelelezi maarufu Kapteni Paul Hendrikse. Novemba 17, wapelelezi hao walimkamata mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Xolile Mngeni na siku mbili baadaye walikamatwa Mziwamadoda Qwabe na dereva wa taxi iliyowabeba Shrien na mkewe, Anni Dewani, aitwaye Zola Robert Tonga.

Wote watatu walifikishwa mahakamani Novemba 20 na kushitakiwa kwa makosa ya ujambazi, kupiga, utekaji nyara na mauaji ya Anni Dewani.

Siku hiyo hiyo baada ya watuhumiwa hao kufikishwa mahakamani na kusomewa mashitaka, polisi wakiongea na kituo kimoja cha televisheni nchini humo walidai kwamba, mauaji hayo yalikuwa ni ya kupangwa, na walibaini hivyo baada ya kumkamata mtu mwingine aitwaye Monde Mbolombo, mfanyakazi wa mapokezi katika Hoteli ya Protea Colloseum aliyeshiriki katika mpango huo kama mtu wa kati, baina ya Zola Tongo na wale watekaji nyara.

Hata hivyo, Mbolombo alipata bahati ambapo alifanya makubaliano na polisi na kuwa shahidi wa upande wa mashitaka. Mbolombo ndiye aliyemuunganisha Zola Tongo na wauaji na aliacha kazi hapo Protea Hoteli Novemba 30.

Baadaye polisi hao walimtaka Shrien aende nchini Afrika Kusini kwa ajili ya gwaride la utambulisho ili kuwabaini wauaji hao.

Siku moja baada ya familia ya Shrien kuajiri msemaji wa familia hiyo, msemaji huyo, Max Clifford, alitoa taarifa kwa vyombo vya habari nchini Uingereza ikimnukuu Shrien akisema: "Nilitafuta pande zote za dunia ili kumpata mwenza atakayenifaa na kujenga familia… kwa nini nitake kumuuwa?" Shrien alikuwa akizungumzia habari zilizoripotiwa na magazeti kadhaa nchini Afrika Kusini kwamba alipanga huo utekaji nyara na mauaji ya mkewe.

Maswali ya kujiuliza


Katika tukio hilo, kuna maswali kadhaa ya kujiuliza au kuzingatia. Mosi, ni dereva na si mkewe aliyetoa wazo la kutembelea maeneo ya uswahilini kama Shrien alivyodai.

Pili, Shrien na mkewe walishikiliwa na watekaji nyara hao ndani ya gari kwa dakika 40 na si 20 kama Shrien alivyodai, kabla hajatupwa nje ya gari hilo.

KWA upande wa familia ya Anni Dewani, msemaji wa familia hiyo, Ashok Hindocha, mjomba wa Anni Dewani, alitoa wito kwa Serikali ya Afrika Kusini kuchunguza zaidi mauaji hayo.

Hata hivyo alimtaka Shrien arudi Afrika Kusini na pia kuwataka polisi wa nchi hiyo kutomtuhumu mtu yeyote kabla ya kufanya uchunguzi makini.

Novemba 25, kaka yake Shrien, Preyen Dewani, alitoa taarifa kwa vyombo vya habari akidai kwamba kaka yake anahofia kuhusishwa na mauaji ya mkewe kimakosa kwa ajili ya kuisitiri Serikali ya Afrika Kusini isikose watalii na kupoteza pato la taifa linalotokana na utalii nchini humo.

Naye msemaji wa familia hiyo ya Shrien, Max Clifford, baadaye alisema Shrien yuko kwenye matibabu ya msongo wa mawazo na yuko chini ya uangalizi wa madaktari.

Aliendelea kusema kwamba, Shrien siyo mtuhumiwa wa mauaji ya mkewe na polisi wa Afrika Kusini hawajamtaka arudi nchini humo.

Kauli hiyo iliungwa mkono na mwendesha mashitaka wa Afrika Kusini ambaye katika mazungumzo yake na vyombo vya habari mwendesha mashitaka huyo alithibitisha kwamba, mpaka wakati huo, Shrien sio mtuhumiwa wa mauaji ya mkewe.

Desemba 3, mwaka 2010, Xolile Mngeni na Mziwamadoda Qwabe kupitia wakili wao walilalamika kwamba aliteswa na polisi. Baadaye wakili wa Shrien, raia wa Afrika Kusini Billy Gundelfinger alijitoa katika kesi hiyo.

Desemba 7, akiwa katika Mahakama Kuu ya Western Cape chini ya makubaliano maalumu aliyofikia na upande wa mashitaka ya kuwa shahidi wa upande wa mashitaka dhidi ya Qwabe na Xolile, Zola Tongo alidai kwamba Anni Dewani aliuawa kwa maelekezo ya mumewe, yaani Shrien Dewani ambaye alimpatia pauni za Uingereza zipatazo 1,300, (sawa na Rand 15,000 za Afrika Kusini) ili amuue mkewe.

Max Clifford msemaji wa familia ya Shrien Dewani, katika taarifa yake kwa vyombo vya habari vya nchini Uingereza kwa niaba ya Shrien Dewani na familia yake, alisema kwamba, madai yaliyotolewa na Zola Tongo hayana ukweli wowote.

Akizungumzia maelezo yaliyotolewa na Zola Tongo kuhusu kuhusika kwa Shrien na mauaji ya mkewe, mwendesha mashitaka Rodney de Kock alimwambia Jaji John Hlope aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo kwamba, waliingia makubaliano maalumu na Zola Tongo awe shahidi wa upande wa mashitaka ili aseme ukweli na ndipo alipowaeleza kwamba, tukio la kutekwa nyara gari lake halikuwa bahati mbaya, bali lilipangwa kama mbinu ya Shrien Dewani na watekaji nyara kutaka kuficha ukweli kuhusu mauaji waliyopanga kuyafanya.

De Kock aliieleza Mahakama hiyo kwamba, Zola Tongo alikuwa amefanya makubaliano na katibu muhtasi wa Shrien tangu wakiwa Uingereza kwamba awapokee wanandoa hao watakapotua katika uwanja wa ndege wa Cape Town wakitokea katika mbuga ya wanyama ya Kruger.

Ijumaa ya Novemba 12, baada ya wanandoa hao kutua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Cape Town, Zola Tongo aliwachukua na kuwapeleka katika hoteli ya kitalii ya nyota tano ya Cape Grace.

De Kock alimnukuu Zola akisema: "Baada ya kuwasili katika hoteli, Shrien Dewani alinifuata nikiwa peke yangu na kuniuliza kama namjua mtu yeyote ambaye anaweza kuondoa ushahidi.

Baada ya kuzungumza naye, nilimuelewa kwamba anataka mwanamke fulani auwawe. Alisema kwamba atalipa kiasi cha Randi 15,000. Hata hivyo Shrien alisema kwamba anazo dola za Marekani na angependa kulipa kwa dola.

Baada ya kuwasiliana na rafiki yangu, tulikubaliana kwamba, gari likishatekwa na wauaji, Shrien Dewani na mimi turuke kwenye hilo gari ili huyo mwanamke auwawe." Mwisho wa kunukuu.

Siku iliyofuata wanandoa hao walitumia siku hiyo kujipumzisha kando ya bwawa la kuogelea hapo hotelini ambapo walipigia familia zao simu kuwaeleza kuhusu maendeleo yao ya fungate hapo nchini Afrika Kusini.

Tongo katika maelezo yake alidai kwamba, ni wakati Anni akiongea kwa simu na ndugu zake nchini Sweden, ndipo walipokutana na Shrien kwa siri ili kukamilisha mpango wao wa utekaji nyara na mauaji waliyopanga yafanyike usiku wa siku hiyo.

Tongo alidai alimuendesha Shrien hadi katika duka la kubadilishia fedha za kigeni kwa ajili ya kubadilisha dola za Marekani alizokuwa nazo na kununua randi (fedha ya nchini Afrika Kusini).
KATIKA maelezo yake polisi, Zola Tongo alibainisha kwamba, jioni ya siku hiyo, aliwachukua wanandoa hao kutoka katika hoteli waliyofikia na kuwaendesha kupitia viunga vya Jiji la Cape Town hadi kwenye eneo alilopanga kukutana na marafiki zake watekaji nyara, lakini hakuweza kuwakuta watekaji nyara hao katika eneo hilo walilokubaliana.

Tongo aliendelea kuendesha gari hadi kwenye mgahawa wa Sushi ulioko eneo la Somerset West, ambapo alidai kwamba, Shrien alimkumbusha kupitia ujumbe wa simu yake ya mkononi kwamba mauaji lazima yatekelezwe usiku wa siku hiyo.

Baada ya wanandoa hao kumaliza mlo wao wa usiku katika mgahawa huo wa Sushi, Tongo aliwaendesha hadi kwenye eneo ambalo alikubaliana kukutana na watekaji nyara.

Wakati wakiwa njiani kuelekea kwenye eneo walipokuwa watekaji nyara, Tongo alimtumia Shrien ujumbe kwenye simu yake ya mkononi kumkumbusha kuhusu malipo ya kazi hiyo ya mauaji na Shrien alimjibu kwamba zipo katika bahasha aliyoiweka katika pochi iliyoko nyuma ya kiti cha abiria cha mbele.

Walipofika kwenye eneo walilokubaliana kukutana na wateka nyara, Mngeni na Qwebe walikuwa wamekwishafika eneo la tukio na waliiteka nyara teksi hiyo ya Tongo kama walivyokubaliana na kutekeleza mauaji hayo kwa kumuua Anni Dewani.

Tongo alidai kwamba, ilikuwa alipwe kiasi cha paundi za Uingereza zipatazo 459 na Shrien, lakini aliambulia kiasi cha paundi za uingereza 92 tu.

Hata hivyo, Tongo alikuwa amekwishahukumiwa kifungo cha miaka 18 jela, Desemba 7 mwaka 2010 na anatumikia kifungo hicho katika Gereza la Malmesbury. Lakini pia Zola Tongo alitarajiwa kutoa ushahidi katika kesi ya Mngeni na Qwebe ambayo ilikuwa ianze mwaka unaofuata, yaani 2011.

Kwa mara nyingine tena msemaji wa familia ya Dewani akizungumzia madai hayo ya Tongo aliyaita ni madai ya kipuuzi kwa asilimia 100 na ni juhudi zake za kujitetea na kujisafisha.

Xolile Mngeni na Mzwamadoda Qwebe nao walisomewa mashitaka ya mauaji, kesi yao ilitajwa kwa mara ya kwanza katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Wynberg.

Wakili aliyekuwa akimtetea Mziwamadoda Qwebe alituhumu Mahakama hiyo kwamba haitamtendea haki mteja wake.

"Nimepata taarifa kuwa, ofisa mmoja wa polisi alimtesa sana mteja wangu kwa kutumia kitu kinachofanana na kurunzi. Alipigwa sana katika sehemu mbalimbali za mwili na hata maelezo aliyotia sahihi hayakuwa yake bali yalikuwa ni ya polisi. Hawa (maofisa wa polisi) walishakuwa na maelezo yao yanayomtuhumu mteja wangu kuhusika na mauaji hayo, walichofanya ni kumwambia tu aweke sahihi. Maelezo hayo hatuwezi kuyaita kwamba ni ungamo," alisema Thabo Nogemane, wakili aliyekuwa akimtetea Qwabe.

Naye wakili wa Mngeni, Vusi Tshabalala, alidai kwamba mteja wake alizibwa pumzi na mfuko wa plastiki kabla ya kulazimishwa kutia sahihi katika maelezo yaliyoandaliwa na maofisa wa polisi, yanayoonyesha kwamba alishiriki katika mauaji hayo.

Wakili huyo alidai kwamba, maofisa hao wa polisi walitumia mbinu mbalimbali za mateso ili kulazimisha mteja wake akiri kuhusika katika mauaji hayo kutokana na msukumo kutoka ngazi za juu uliowataka kushughulikia kesi hiyo haraka kwa sababu imekuwa gumzo kwa watu wengi ndani na nje ya nchi hiyo, hususan vyombo vya habari.

Kesi hiyo ilichelewa kuanza kusikilizwa hadi ilipofika Juni 13, mwaka 2011. Kucheleweshwa kwa kesi hiyo kulitokana na mmoja wa washitakiwa, Xolile Mngeni kuonekana ana uvimbe katika ubongo wake ambapo ilibidi afanyiwe upasuaji ili kuondoa uvimbe huo.

Hata hivyo, kesi ya Mziwamadoda Qwebe aliyekuwa na miaka 28 wakati huo iliendelea kusikilizwa na Agosti 8, mwaka 2012 alihukumiwa kifungo cha miaka 25 gerezani.

Miezi minne baadaye, kesi ya Xolile Mngeni aliyekuwa na miaka 24 ilikwishakusikilizwa na Desemba 5, mwaka 2012 alihukumiwa kifungo cha maisha gerezani kwa kosa la mauaji ya Anni Dewani.

Serikali ya Afrika Kusini ilituma maombi nchini Uingereza kutaka Shrien arejeshwe nchini humo kukabiliana na mashitaka ya mauaji.

Ilikuwa Desemba 8, mwaka 2010, baada ya kujisalimisha mwenyewe katika kituo cha polisi cha Bristol, Shrien alikamatwa saa 4:38 usiku na kushikiliwa katika kituo cha polisi cha Metropolitan na askari wa kitengo cha kurejesha watuhumiwa wanaohitajika kujibu mashitaka katika nchi nyingine (Extradition Unit).

Walikuwa wanamshikilia kutokana na amri iliyotolewa kuwa akamatwe baada Serikali ya Uingereza kupokea ushahidi kupitia ubalozi wa Afrika Kusini nchini humo unaodai kuwa, kuna hali ya kutia shaka inayoashiria Shrien alishirikiana na watu wengine kumuua Anni Dewani hapo Novemba13, mwaka 2010.

Asubuhi ya Desemba 9, wakili wa Shrien nchini Uingereza anayeitwa Clare Montgomery akikanusha madai hayo, alisema kwamba, Shien hakuhusika kabisa katika mauaji ya mkewe.

Alipofikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Westminster, Shrien aliiambia Mahakama hiyo kwamba, hastahili kurejeshwa nchini Afrika Kusini kukabiliana na mashitaka ya mauaji ya mkewe.

Wakili wa nchini Uingereza anayeiwakilisha Serikali ya Afrika Kusini, Ben Watson, alisema pale mahakamani kwamba, Shrien alitoa katika kadi yake ya malipo (Mastercard) kiasi cha pauni za Uingereza 1,000 kabla ya kutokea kwa mauaji hayo, kikiwepo kiasi kingine cha pauni za Uingereza 800, jioni ya Novemba 13.

Wakili huyo aliendelea kudai kwamba, Shrien aliwahi kuongea na watekaji nyara hao kuhusu mpango wake wa kutaka kuua kabla ya kwenda kwenye fungate nchini humo, lakini wakili wa Shrien, Clare Montgomery alikanusha madai hayo na kusema kwamba, Shrien hajawahi kwenda nchini Afrika Kusini kabla ya kwenda kwenye fungate.

Wakili huyo alionyesha hati ya kusafiria ya Shrien pale mahakamani iliyotolewa mwaka 2006, ambayo haikuwa na mahali palipoonyesha kwamba Shrien aliwahi kuwa nchini Afrika Kusini kabla ya fungate.

Shrien aliachiwa kwa dhamani ya kiasi cha pauni za Uingereza 250,000 kiasi ambacho kililipwa na familia yake.

Hata hivyo, Mwendesha Mashitaka aliyekuwa akiwakilisha Serikali ya Afrika Kusini alitoa hati ya kukata rufaa dhidi ya dhamana aliyopewa Shrien.

Siku iliyofuata, Desemba 10 katika Mahakama Kuu, wakili wa upande wa mashitaka Ben Watson alimwambia Jaji Ouseley, aliyekuwa akisikiliza maombi hayo ya Serikali ya Afrika Kusini kutaka Shrien arejeshwe nchini humo kujibu mashitaka, kwamba, kamera (CCTV) zilizofungwa katika Hoteli ya Cape Grace, ambayo ndipo walipofikia wanandoa hao ilimuonyesha Shrien.

SIKU iliyofuata, Desemba 10 katika Mahakama Kuu, wakili wa upande wa mashitaka Ben Watson alimwambia Jaji Ouseley, aliyekuwa akisikiliza maombi hayo ya Serikali ya Afrika Kusini kutaka Shrien arejeshwe nchini humo kujibu mashitaka, kwamba, kamera (CCTV) zilizofungwa katika Hoteli ya Cape Grace, ambayo ndipo walipofikia wanandoa hao ilimuonyesha Shrien akikutana na kuzungumza na dereva taxi, Tongo, katika eneo la kuegeshea magari mara mbili siku ya tarehe 12 Novemba usiku kabla ya mauaji, wakati Tongo kwa upande wake alidai kwamba, Shrien alimuomba amtafutie mlenga shabaha atakayemuua mwanamke.

Na katika maelezo ya polisi wa Afrika Kusini ya maombi ya kutaka Shrien arejeshwe nchini humo kujibu mashitaka ya mauaji, maelezo hayo yalidai kwamba, kaka wa Shrien alifanya juhudi kubwa ili kupata mkanda huo uliorekodiwa na kamera (CCTV) za hoteli unaomuonyesha Shrien akikutana na dereva taxi Tongo, mara mbili katika eneo hilo la kuegeshea magari.

Shrien alionekana akikutana na dereva taxi Tongo mara kadhaa bila mkewe ndani ya hoteli hiyo katika saa 24 kabla ya mauaji na alionekana akimkabidhi dereva huyo wa taxi bahasha, Novemba 16, ikiwa ni siku tatu tangu yatokee mauaji hayo.

Kabla ya kumkabidhi Tongo bahasha hiyo, Shrien alionekana akiwa amekaa pembeni ya baba mkwe wake, Vinod Hindocha ambaye alionekana akiomboleza kifo cha binti yake. Baadaye Tongo alionekana akiingia katika mojawapo ya vyoo vya hoteli hiyo ili kuhesabu fedha alizopewa na Shrien.

Wakili huyo aliendelea kusema kwamba, polisi wa Afrika Kusini pia wanayo maelezo yaliyotolewa na muuzaji wa fedha za kigeni kwa magendo nchini humo ambaye alithibitisha kuwatambua Tongo na Shrien walipokwenda kwake ili kubadilisha kiasi cha dola za Marekani 1,500.

Watson alidai kwamba kiasi hicho kilikuwa ni nyongeza baada ya awali kuwalipa pauni za Uingereza 1000, ambazo Shrien alizitoa katika mashine ya kutolea fedha benki, kupitia kadi yake ya malipo (Mastercard).

Hata hivyo, Shrien aliachiwa kwa dhamani na kutakiwa kusalimisha hati yake ya kusafiria. Alipotakiwa atoe maoni yake kuhusiana na kesi hiyo wakati alipokuwa katika ziara ya kikazi katika Jimbo la Limpopo, aliyekuwa Kamanda wa Polisi nchini humo, Bheki Cele alisema: "Kima mmoja alikuja hapa na mkewe kutoka Uingereza ili kumuua. Alidhani sisi Waafrika Kusini ni wapumbavu. Msije kuua watu hapa."

Hata hivyo baadaye Oktoba 2011, kamanda huyo wa polisi Bheki Cele alifukuzwa kazi kutokana na tuhuma za rushwa.

Mwanasheria mmoja akizungumzia kauli hiyo ya Bheki Cele alidai kwamba, kwa kauli hiyo kutoka kwa mtu mwenye dhamana kubwa katika mamlaka ya sheria, hatarajii Shrien kutendewa haki katika shauri hilo.

Naye Helen Zille, Gavana wa Jimbo la Western Cape (Kwa Afrika Kusini cheo cha Gavana hujulikana kama Premier) akizungumzia kesi hiyo alisema ni lazima Shrien arejeshwe Afrika Kusini kujibu mashitaka ya mauaji ya mkewe.

"Siamini kama kuna pepo mbaya kiasi hiki hapa duniani, na pepo huyo anaonekana kuichafua Afrika Kusini…" alisema mama huyo wa kizungu.

Katika sherehe za kukaribisha mwaka mpya wa 2011, marafiki watano wa Anni, waliandika barua ya wazi kwa Shrien kupitia gazeti la nchini Uingereza, The Sun, wakisema: "Unadai kwamba huna hatia kuhusiana na hizi tuhuma, kwa nini usirudi Cape Town nchini Afrika Kusini na kuwathibitishia polisi wa nchini humo kwamba wamekosea..?"

Katika barua hiyo marafiki hao wa Anni walimtaka Shrien aepuke kujiingiza katika malumbano na vyombo vya habari na badala yake azingatie kile kilichotokea Novemba 13 na 14.

Familia ya Dewani walianzisha mfuko wa kumbukumbu ya kifo cha Anni Dewani ambapo fedha zitakazopatikana kupitia mfuko huo walipanga zitumike kujenga shule nchini India kama kumbukumbu ya kifo chake.

Januari 8, mwaka 2011, Ashok Hindocha msemaji wa familia ya Hindocha, alitoa taarifa katika vyombo vya habari akisema kwamba, familia ya Hindocha haikushirikishwa katika mpango huo na kuuelezea mpango huo kama mradi wa kutaka kumsafisha Shrien machoni mwa jamii.

Januari 17, rafiki wa familia ya Dewani, Hashmukh Velji Shah alionekana kwenye kipindi kimoja cha televisheni cha BBC (Shirika la Utangazaji la Uingereza) akisema kwamba, Shrien hawezi kuhukumiwa kurudishwa Afrika Kusini iwapo hatahakikishiwa kupewa dhamani nchini humo.

Hata hivyo katika kipindi hicho hicho cha televisheni cha BBC, Waziri wa Sheria na Katiba wa Afrika Kusini, Jeff Radebe, alisema: "Kwa jinsi ninavyofahamu, iwapo shauri la Shrien Dewani litasikilizwa katika Mahakama ya Afrika Kusini, shauri hilo litaendeshwa kwa haki."

JANUARI 18, aliyekuwa Kamanda wa Polisi Afrika Kusini, Bheki Cele alisema wapelelezi wa shauri hilo wanajua kwa nini Anni aliuawa. Askari mmoja wa upelelezi wa cheo cha juu, Luteni Kanali Mike Barkhuizen alitumwa Uingereza kupeleleza shauri hilo ili kukusanya ushahidi zaidi ambapo ilikuwa pia ahudhurie shauri la maombi ya nchi yake ya kutaka Shrien arejeshwe nchini humo kukabiliana na mashitaka ya mauaji.

Shauri hilo lilikuwa lisikilizwe Januari 20, ambapo askari huyo wa upelelezi ilikuwa atoe vielelezo vya ushahidi dhidi ya Shrien ili Mahakama ikubali ombi la nchi yake la kutaka Shrien arejeshwe nchini humo.

Januari 20, siku ambayo Shrien alitakiwa afike mahakamani kusikiliza shauri lake, lakini hakufika na wakili wake alidai kwamba amelazwa hospitalini akipatiwa matibabu kutokana na kusumbuliwa na msongo wa mawazo.

Kuanzia hapo shauri hilo lilikuwa likiahirishwa mara kwa mara kutokana na hali ya afya ya Shrien kutotengemaa.

Septemba 28 2011, baada ya shauri hilo kuahirishwa kwa taktiban miezi tisa, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uingereza, Theresa May, alisaini hati ya kuamuru Shrien Prakash Dewani apelekwe Afrika Kusini kujibu mashitaka ya mauaji.

Hata hivyo, Shrien alikata rufaa kupinga amri hiyo na Machi 30, mwaka 2012 Mahakama Kuu nchini humo, ilisitisha utekelezaji wa amri hiyo.

Kusitishwa kwa utekelezaji wa amri hiyo kulitokana na hali ya afya ya Shrien ambaye alikuwa bado anasumbuliwa na msongo wa mawazo na hali yake ilikuwa haijatengemaa.

Siku hiyo ya Machi 30, 2012, Jaji wa Mahakama Kuu Uingereza, Sir John Thomas alisema kwamba, haitakuwa vyema kumrudisha Shrien Dewani Afrika Kusini kwa hali aliyokuwa nayo.

Julai 24, mwaka 2013, Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Westminster, Howard Riddle alitoa hukumu ambayo iliridhia mtuhumiwa Shrien Dewani kupelekwa Afrika Kusini kwa ajili ya kukabiliana na mashitaka ya tuhuma za kuhusika na mauaji ya mkewe, Ani Dewani.

Hata hivyo, timu yake ya wanasheria waliokuwa wakimtetea ambayo ilikuwa na siku 14 kisheria za kukata rufaa ilisema kwamba, wataipitia hukumu hiyo kwa makini kabla ya kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo wa Mahakama.

Lakini Machi 2,mwaka huu (2014), Shrien Dewani alifanya jaribio la kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa Mahakama uliomtaka arejeshwe nchini Afrika Kusini ili kukabiliana na mashitaka ya kumuua mkewe, lakini rufaa yake ilitupiliwa mbali na Mahakama na hivyo kupewa siku 28 za kupelekwa nchini Afrika Kusini ili kukabiliana na mashitaka hayo.

Nchini Afrika Kusini vyombo vingi vya habari vilikuwa vikiripoti kesi hii tangu kugundulika kwa mwili wa Anni Dewani. Kesi hiyo ilisababisha kupungua kwa mapato yanayotokana na biashara ya utalii.

Kampuni nyingi za utalii ziliripoti kupungua kwa kiasi kikubwa kwa kupokea wageni. Watalii walipewa tahadhari kuhusu kuongezeka kwa mauaji nchini humo kwa kiwango cha vifo 46 kwa siku.

Shauri hili bado halijapatiwa ufumbuzi na hadi leo linazisumbua mamlaka za kisheria za hizi nchi mbili, yaani Afrika Kusini na Uingereza.

Nchini Uingereza inaaminika kwamba pamoja na mambo mengine, sababu ya Shrien Dewani kupanga mauaji ya mkewe, Anni Dewani, ni kutokana na tabia yake ya kupenda wanawake kupita kiasi.

Baada ya hukumu hiyo iliyosababisha rufaa kutupiliwa mbali, siku 36 baadaye Shrien Dewani hatimaye alisafirishwa kwa ndege kupelekwa nchini Afrika Kusini kujibu mashitaka ya kuhusika na mauaji ya mkewe Anni Dewani.

Ilikuwa Jumanne ya Aprili 8, 2014, Shrien Dewani alisafirishwa kwa ndege maalumu ya kukodi ambayo ilikodishwa na Serikali ya Afrika Kusini na aliwasili asubuhi, akisindikizwa na daktari mmoja, nesi mmoja askari mmoja wa Afrika Kusini na askari mwingine wa Interpol.

Akiwa amevalia suti nyeusi na shati jeupe na tai nyeusi, Shrien Dewani mwenye umri wa miaka 34 sasa, alipakiwa kwenye gari dogo jeusi lenye vioo vilivyowekewa vivuli vyeusi (tinted), alipelekwa moja kwa moja hadi Mahakama Kuu ya Cape Town, saa 11:00.

Akiwa amekaa kwa utulivu hapo mahakamani, Jaji John Hlope alimjulisha kwamba atakuwa chini ya ulinzi wakati atakapokuwa katika Hospitali ya Valkenberg kwa uchunguzi wa kiafya. Alipoulizwa na Jaji kama ameelewa alichoambiwa, Shrien Dewani alijibu kwa kifupi tu; "ndiyo".

Waendesha mashitaka katika shauri hilo walikubaliana kuahirishwa kwa kesi yake hadi Mei 12, mwa 2014. Msemaji wa waendesha mashitaka katika kesi hiyo Nathi Mncube akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuahirishwa kwa shauri hilo alisema; "Wakati atakapokuwa akifanyiwa uchunguzi wa kiafya katika hospitali hiyo, tunaamini kwamba madaktari watatupa taarifa kuhusu afya yake na taarifa hiyo ndiyo itakayotusaidia kufanya uamuzi kuhusu kuendelea kwa kesi yake."

Baadaye alipelekwa katika Hospitali ya Valkenberg inayohusika na masuala ya matibabu ya kisaikolojia na msongo wa mawazo ambapo atalazwa hapo akiwa chini ya ulinzi mkali, kwa ajili ya uchunguzi zaidi ili kuthibitisha kama hali yake ya kiafya na kiakili inaruhusu kusimama kizimbani ili kusikiliza kesi yake.

Tangu yalipotokea mauaji ya mkewe nchini Afrika Kusini, Dewani amekuwa akipatiwa matibabu ya kisaikolojia na msongo wa mawazo nchini Uingereza, matibabu ambayo yalisababisha kesi yake ya kutakiwa kurudishwa nchini Afrika Kusini kujibu mashitaka, kuahirishwa mara kadhaa.
 
Habari imekuwa ndefu...ntasoma baadae...
Ila nilishafatilia kuhusu hii case..
Jamaa alikuwa gay...alioa ili kuficha ukweli kuhusu yeye.
Na walipokuwa honeymoon SA camera za hotelini ziliona picha huyu mwanaume anatoa pesa (if am right) kwa wauaji wa mkewe...hivyo aliwalipa wamuue mkewe...na alijua wakienda SA itakuwa rahisi kumuua mkewe kwa sababu ni moja ya nchi mashuhuri kwa wauaji wa kulipwa...

Leo nimeona habari yahoo kuwa jamaa mahakama imemkuta hana hatia...nimeona heading tu sijasoma details...
Mambo ya sheria bana ...unaweza achiwa huru huku ni mkosaji...au ukafungwa bila kosa...kazi sana...
 
ingekuwa ni mimi ningekufia hapo hapo
 
A travesty of justice!

How that faggot can walk scot-free is mind-boggling to me.

Law really is an ass, sometimes.
 
dah nimesoma hadi nimechoka,,atakaeisoma yote anipe summary ya sababu ya jamaa kuagiza mkewe auawe au ni propaganda za wasauzi wasikose watalii
 
Jamaa alikuwa gay, akamuua mke wake.. Familia zote za mke na mume ni mabilonea.. so mwanaume alilazimishwa kuoa ili kutoa aibu but alikuwa hampendi mke wake.
 
Jamaa alikuwa gay, akamuua mke wake.. Familia zote za mke na mume ni mabilonea.. so mwanaume alilazimishwa kuoa ili kutoa aibu but alikuwa hampendi mke wake.

dah! noma sana,,nashkuru kwa ufupisho mkuu
 
Ukiisoma jamaa alikuwa ameshashindwa kesi lakini mwisho wa siku akasafishwa, nna nadharia mbili kuhusu hii kesi. Inawezekana kweli alipanga mauaji, pili inawezekana hakuua lakini stori iliisababishia Afrika kusini madhara makubwa kwenye utalii hivyo kusafisha hali ilibidi walete 'twist' itakayowapunguzia madhara.
 
Dah! Story nzuri japo mambo ya sheria wakati mwingine yanatatanisha
 
Jamaa alikuwa gay, akamuua mke wake.. Familia zote za mke na mume ni mabilonea.. so mwanaume alilazimishwa kuoa ili kutoa aibu but alikuwa hampendi mke wake.

Ndugu mwandishi...
Nimesoma mwanzo mwisho ila hakuna sehemu uliyaondika hauo kuwa alikuwa gay na hakumpenda mkewe...
Naomba imalizie kiasi fulani imenvuta...
 
Jamaa alikuwa gay, akamuua mke wake.. Familia zote za mke na mume ni mabilonea.. so mwanaume alilazimishwa kuoa ili kutoa aibu but alikuwa hampendi mke wake.

Makubwa sasa kwanini aliamua kumuua mkewe au kuficha aibu ndo mana nilikuwa naona BBC sikuelewa
 
Hivi hii kesi haijasha kumbe? Kweri ukiwa na fedha kila kitu cha wezekana
 
Ndugu mwandishi...
Nimesoma mwanzo mwisho ila hakuna sehemu uliyaondika hauo kuwa alikuwa gay na hakumpenda mkewe...
Naomba imalizie kiasi fulani imenvuta...

ni kweli jamaa alikuwa gay hiyo imesemwa kwenye vyombo vya habari kama ulikuwa unafuatilia hii stori.

Ila jamaa alivyoukwepa mkono wa sheria inashangaza maana kweli wanasheria wanaweza kukupitisha kwenye tundu ya sindano. Au pengine wale mashahidi ambao tayari walishafungwa walipewa mshiko ili kutoa ushahidi usioeleweka. Chief Prosecutor leo amekubali kwamba kushindwa kwao kumechangia kwa kiasi kikubwa kwa kutumia mashahidi wale.

Ila kama amepanga kweli mauaji haya Mungu anamwona na itakuwa kichwani kwake mpaka mwisho wa uhai wake.
 
Mkuu haya ya kuwa gay sithani kama yanaukweli inaweza kuwa spinning tu ila polisi wa SA kwa rushwa ni maisha yao na ndiyo inawezekana wamepanga haya na ushahidi ni huyo mkuu wa polis ailiyefukuzwa kazi.
 
Kweli ukitaka kumficha kitu muafrika muandikie. Mimi nimeona uvivu hata kisoma, labda kesho kwakua ni mapumziko cna kazi ntasoma. Haya wanasheria ndo mahali penu hapo
 
Cape town siijui vema,na ata mauaji huko si mengi kama hapa JOBURG,but now days mambo yamebadirika maana usalama ni mkubwa.
But kuna mitaa kama YEOVILLE,BEREA,ALEXANDRA na HILLBROW,huko ni full mauaji na unyang'anyi,ni kama miezi miwili imepita kuna dogo mmoja ni MTZ ni machinga wa simu anatokea kanda ya ziwa,aliuawa club hapa JOBURG kwa ulimbukeni wake.
Dogo alikua anaingia club kila weekend na around rand 10,000.Siku hiyo jamaa wakamuotea wakamchoma kisu wakabeba mzigo wakatembea.
But maeneo kama BEDFORDVIEW,SANDTON,FOURWAYS,SUNNINGHILL,HYDE PARK,MORNINGSIDE,ROSEBANK,HOUGHTON,WAVERLY,PARKHURST,NORTHGATE huku ni salama sana kuishi.
But nyumba ziko bei juu sana.
So kabla ya kuja huku ni vema ukajiandaa kukabiliana na majanga hayo.
But DARBAN iko poa sana ingawa pesa ngumu kama MORO kwa TZ.
Mambo yote Joburg!!!!
 
Nilibahatika kukutana na wanafunzi wa Stellenbosch kwenye event fulani,...nao wanalalamika uharifu mitaani huko juu...na nadhani hiki chuo kipo Cape Town au karibu na Cape Town...walikuwa wananisimulia kuporwa laptop na kuumizwa mtaani ni kawaida...
Nimekosa hamu na hiyo nchi ...

Cape town siijui vema,na ata mauaji huko si mengi kama hapa JOBURG,but now days mambo yamebadirika maana usalama ni mkubwa.
But kuna mitaa kama YEOVILLE,BEREA,ALEXANDRA na HILLBROW,huko ni full mauaji na unyang'anyi,ni kama miezi miwili imepita kuna dogo mmoja ni MTZ ni machinga wa simu anatokea kanda ya ziwa,aliuawa club hapa JOBURG kwa ulimbukeni wake.
Dogo alikua anaingia club kila weekend na around rand 10,000.Siku hiyo jamaa wakamuotea wakamchoma kisu wakabeba mzigo wakatembea.
But maeneo kama BEDFORDVIEW,SANDTON,FOURWAYS,SUNNINGHILL,HYDE PARK,MORNINGSIDE,ROSEBANK,HOUGHTON,WAVERLY,PARKHURST,NORTHGATE huku ni salama sana kuishi.
But nyumba ziko bei juu sana.
So kabla ya kuja huku ni vema ukajiandaa kukabiliana na majanga hayo.
But DARBAN iko poa sana ingawa pesa ngumu kama MORO kwa TZ.
Mambo yote Joburg!!!!
 
Nilibahatika kukutana na wanafunzi wa Stellenbosch kwenye event fulani,...nao wanalalamika uharifu mitaani huko juu...na nadhani hiki chuo kipo Cape Town au karibu na Cape Town...walikuwa wananisimulia kuporwa laptop na kuumizwa mtaani ni kawaida...Nimekosa hamu na hiyo nchi ...
Ni kweli mkuu,Ukiachana na WESTERN CAPE hicho ni miongoni mwa vyuo vikuu pale CAPE TOWN,kipo kwenye mji mmoja unaitwa STELLENBOSCH.But mkuu hayo maeneo niliyoyataja kua ni salama it is real safety.Becouse even clusets zinakua garded 24hrs.So kama utabahatika next time kufika joburg ebu tembelea maeneo hayo,there are a lot of white peoples from europe and asia who move to joburg for life and job seking na wote wanafikiaga maeneo hayo.Sehemu kama HILLBROW ni shida sana,bcoz kuna wabongo na wakenya pale as well wazimbabwe na wanaigeria wanataabika sana so hawaoni shida kukutoa roho.But nawasifu sana wtz wa huku,bcoz wana ushirikiano mkubwa sana hasa wale wanao ishi maeneo duni,but shida ni hizo biashara mbovu ambazo hawataki kuziacha wakati huku kuna kazi za mashambani ambazo zinalipa.Mwezi sept nilimtembelea girlfriend wa mdogo wangu(shemeji yangu) yupo KWAZULU NATAL akaniambia kampuni yao ya kilimo cha mpunga inatafuta vibarua,nikaja nikawachukua wabongo kama 27 tena kwa kuwalipia nauli yangu but wamefanya kazi mwezi mmoja tu wakaacha isipokua wawili pekee ndio wanaendelea.
 
Back
Top Bottom