kido madini
JF-Expert Member
- Oct 13, 2012
- 223
- 144
Mm nijuavyo nyumba yyte ile ya ibada mtu anaruhusiwa kusali/kuswali muda wwte hata kukesha.Waislamu pia wana swala za usiku kama yalivyo baadhi ya makanisa ambao huwa wanamikesha. Sina hakika kama mikesha ya makanisani ni uhuni.
NUKUU:
"Askari walikwenda Chumo msikitini, wakapiga risasi wakachukua watu 10 tumefika damu zimetapakaa, walivyorudi mmoja kafa, mmoja hana jicho, mmoja wakamnyoa ndevu kwa kumchoma moto, mnapotuambia nchi hii ina amani na utulivu mimi siwaelewi" - Suleiman Bungara (Bwege) Mb - Kilwa.
[HASHTAG]#MUHIMU[/HASHTAG]
Haya yaliyoripotiwa na Mhe. Bungara ni machache kati ya mengi ambayo askari wetu wameyafanya na wanaendelea kuyafanya dhidi ya baadhi ya viongozi na waumini wenzetu wa dini ya kiislam katika kile kiitwacho vita dhidi ya ugaidi.
Pamoja na madhira hayo wanayokutana nayo viongozi wetu wa dini na baadhi ya waumini wenzetu wa dini ya kiislam nchini sijawahi kuona jitihada zozote zinazofanywa na taasisi ijulikanayo kama Baraza Kuu la Waislam Tanzania (Bakwata) chini ya kiongozi wake mkuu Ndg. Abubakar Zuber kulaani au kutafuta suluhu ya jambo hilo.
Pamoja na hayo naomba niwakumbushe askari wetu wapendwa na jeshi la Polisi kwa Ujumla wake.
Polisi wetu ninyi mmepewa dhamana kubwa ya kulinda usalama wa raia na mali zao, na mkae mkijua kua raia karibu wote wa Nchi hii tunawategemea sana katika kulinda usalama wa maisha yetu na mali zetu,
hivyo ni vema mkazingatia mafunzo, utaalam na weledi wa hali ya juu kwa mujibu wa kanuni mbalimbali za maswala ya usalama zinavyowataka pindi mnapohisi kuna viashiria vya uvunjifu wa amani katika eneo lolote na si kutumia Miguvu katika sehemu inayohitajika Akili na Maarifa.
Najua Askari wetu wanakabiliana na changamoto mbalimbali za mishahara isiyokidhi mahitaji yao lakini pia kufanya kazi kwa maagizo na mashinikizo kutoka kwa baadhi ya viongozi wa kisiasa, nawaomba sana msivunjike moyo kwa kua taifa na watanzania tunawategemea sana katika kuimarisha usalama wetu na wa mali zetu.
Hivyo muitumie dhamana hiyo vizuri kwa kutenda haki kwa watu wa makundi yote kwa kua ninyi ni binaadam na mkumbuke kua kuna maisha baada ya Dunia ambayo yataamuliwa na matendo yenu hapa Duniani aidha Peponi au Jahannam (Motoni)
[HASHTAG]#Tujitafakari[/HASHTAG]
Mimi pia nimekuwa nikijiuliza mara kwa mara kuwa wanzetu wakristo tumewafanyia nini sisi waislam? Najiuliza swali hili kwasababu tupo nao maofisini, tupo nao katika misiba yao na ya kwetu, tupo nao kwenye shida za kuuguliwa, tunakula nao, tunakunywa nao na baadhi yao tumeoleana nao, tupo nao kwenye masoko tukiuza na kununua bila hata kuuliza dini.watanzania wanaoupinga huu uislamu hata hatuelewi kitu gani kimetokea.mpaka wametokea kuchukiwa na baadhi ya wakiristo kiasi hiki na kama ni huo ugaidi tunajiuliza ni ugaidi upi waislamu wa tanzania walioufanya kwa watanzania wenzao? Au ubaya gani Waislamu wa Tanzania waliofanyia wasio waislamu Tanzania kiasi cha kuchukiwa hivi au ni chuki tu ambazo pengine wamefundishwa na viongozi wao wa dini maanake hatuwaelewi hawa wenzetu. Yaani watu wanasherekea na kuunga mkono manyanyaso na mauaji waliofanyiwa watanzania wenzao hii inasikitisha sanaa. Tunakoelekea ipo siku tutajuta.
exactlyKuwatesa na kuua waumini eti kwakuwa umewakuta msikitini usiku siyo utetezi. Uislsmu una ibada za usiku " KIAMLAILI". Pia misikitini ndipo wanapofikia kulala watu TABLIH. Lakini kama alivyoandika chige, wale wanaodai ni ugaidi waseme juu Ben Saanane na Tundu Lissu nao ni Magaidi?
Tupewe hayo maelezo ya inteligensia yenye ushahidi usiotia shaka. Hata wewe sio rahisi mtoto wako auawe mbele ya macho yako halafu unaambiwa ni mwizi bila uthibitisho halafu utakubal kirahisi rahisi. Tusishabikie tu mambo kwasababu yamewakuta wenzetuPamoja na Polisi kutotumia mbinu rafiki kafika kushughulikia changamoto za uhalifu au viashiria vyake naamini kuna shida katikati ya hao waumini na mashehe. Kuna wawili au watatu wana agenda zao sasa wanaponza wenzao. Haingii kichwani polisi wachukie waumini wa mskiti mmoja pekee kati ya yote iliyopo Kilwa. Tusiwe wepesi wa kulaumu bila kujua taarifa za upande wa pili.
Intelijensia ya ipo kila mahali na usishangae kati ya waliochukuliwa na pengine hatarudishwa ni intelijensia.
Ukweli mnaujua ila mnajificha vichwa kama mbuni mkidhani hamuonekani. hakuna siri duniani. kama hawa polisi wanafanya haya ya kumnyanyasa mtu kwa sababu ya dini yake Mungu atashughulika nao. na nijuavyo mimi kama hivi ndivyo hakuna muumin wa uislam au kiongozi wa uislam anayeweza kuuvumilia unyanyasaji au unyanyapaa wa kiiman hata kwa dakika moja au mbili kama walivyo wakristo. Ila ukimya wa viongozi wa kiislam unaashiria kuwapo kwa jambo jingine linalofanywa na hawa jamaa kwa kivuri cha uislam. Polisi msimuonee mtu kisa dini yake. ila anayepanga uharibifu na aharibiwe yeye.Maneno ya kipumbavu ya kuunga mkono mauaji na manyanyaso wanayofanyiwa hawa waislamu na maiti zote zilizo okotea kwenye maviroba ni waislamu waliouliwa
Halafu tuluvyo wanafiki eti nchi ya amani hakuna amani yoyote nchi hii. Na hao wanaofanyiwa huu umyama ni binadamu wenzenu na ni watanzania lakini tofauti iliyopo ni sio wakanisa. Kwa hii ni jinsi gani nchi hii ilivyo na ubaguzi wa dini.
Mberesero alichokifanya chuo kikuu cha garisa kenya unakijua? waliokamatwa Mozambique makosa yao unayajua? leo kenya kesho mozambique keshokutwa wapi? Endeleeni kujificha kichwa kama mbuni mkidhani kiwiliwili hakionekani.watanzania wanaoupinga huu uislamu hata hatuelewi kitu gani kimetokea.mpaka wametokea kuchukiwa na baadhi ya wakiristo kiasi hiki na kama ni huo ugaidi tunajiuliza ni ugaidi upi waislamu wa tanzania walioufanya kwa watanzania wenzao? Au ubaya gani Waislamu wa Tanzania waliofanyia wasio waislamu Tanzania kiasi cha kuchukiwa hivi au ni chuki tu ambazo pengine wamefundishwa na viongozi wao wa dini maanake hatuwaelewi hawa wenzetu. Yaani watu wanasherekea na kuunga mkono manyanyaso na mauaji waliofanyiwa watanzania wenzao hii inasikitisha sanaa. Tunakoelekea ipo siku tutajuta.
Waingie kwenye nchi ya watu wauwe viongozi wao wauwe wananchi hawana nguvu ya kupambana nao. Wanaamua na wao kulipiza kisasi vile wanavyoweza halafu mnawaita magaidi. Hizo za Kenya na huko kwengineko hazituhusu kabisa hapa kwwtu. Munaanza chokochoko na walio wajinga wakiingia kwenye huu mtego muwamalize ?Mberesero alichokifanya chuo kikuu cha garisa kenya unakijua? waliokamatwa Mozambique makosa yao unayajua? leo kenya kesho mozambique keshokutwa wapi? Endeleeni kujificha kichwa kama mbuni mkidhani kiwiliwili hakionekani.
No please! Usidhani uko salama. Kuna siku utapigwa wewe ndio utaelewa machungu ya maonevu.Na mpigwe tu maana hakuna namna....
Mmezidi kucheza ma-karate misikitini badala ya kuswali.
Imekuwa kawaida kuwafundisha vijana wetu mashuleni judo na karate, kutumia majambia, na siku hizi mpaka meditation mnafanya ndani ya masjidi za mashule.
Mimi narudia kauli ya Pinda aliposema
"Na wapigwe tu"
Kwa hiyo Mberesero katumwa na Waislamu Wote wa Tanzania aue wale Wanafunzi wa Garisa?Mberesero alichokifanya chuo kikuu cha garisa kenya unakijua? waliokamatwa Mozambique makosa yao unayajua? leo kenya kesho mozambique keshokutwa wapi? Endeleeni kujificha kichwa kama mbuni mkidhani kiwiliwili hakionekani.
Siyo waislamu wote ila magaidi fulani ndani yake!Asigwa leo sijapenfezwa na mchango wako hata kidogo.
Mimi ni mkristo tena mkristo kweli lkn siwezi kiwachukia ndg zetu waislam kiasi hicho.
Maelezo yako wapelekee wahusika mi nitakusaidia nini. mi najaribu kutoa angalizo tu kuwa wako watu wanauchafua uislam kwa maslahi ya matumbo yao. huo ni mfano hai.Kwa hiyo Mberesero katumwa na Waislamu Wote wa Tanzania aue wale Wanafunzi wa Garisa?
Hakika Generalization ni tatizo sana. Mtu ambae hana uwezo wa kuona na kuyajua hata yale yaliyo mbali na yeye ndio huwaza kua kila akionacho basi ndio kiko hivyo hivyo kila mahali.
Ngoja nikuulize, wewe hujawahi kusaidiwa na Muislamu yeyote asie Mberesero mpaka unafikia kudhani kua kila Muislam yuko kama Mberesero?
Nawe Hilo angalizo lako si ungewapelekea wahusika pia?Maelezo yako wapelekee wahusika mi nitakusaidia nini. mi najaribu kutoa angalizo tu kuwa wako watu wanauchafua uislam kwa maslahi ya matumbo yao. huo ni mfano hai.