UZUSHI Mauaji mapya Kibiti: Serikali iweke hadharani idadi ya askari na raia waliouawa mpaka sasa

Baada ya tathmini, tumebaini kuwa taarifa hii ni ya uzushi
Kwa taarifa za uhakika ni kuwa tangu January hadi sasa sio chini ya askari 20 walikwisha uwawa ila serkali Inafanya siri hata sisi hatukuruhusiwa kufika KIBITI kwa kuambiwa kuwa mkuu wa wilaya na kamati yake ya ulinzi na usalama hawaruhu Kwa kuwa eneo ni hatari sana.

IMG_8260.jpeg

Kwa taarifa za uhakika ni kuwa wale magaidi wa kipindi cha magufuli wamerudi Kwa kasi wana silaha nzito za moto huku idadi ya askari ikiwa ndogo baada ya eneo kuonekana shwali baada ya operation ya kipindi cha magufuli

Nitoe wito kwa serikali iweke wazi ili raia wajue nini kiaendelea rufiji kwa umma isifanye Siri huku hali ikizidi kuwa mbaya.

USSR
 
Tunachokijua
Jeshi la polisi nchini kupitia akaunti yake rasmi inayopatikana kwenye Mtandao wa X (zamani Twitter) limekanusha ujumbe unaosambaa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii na kusema kuwa hakuna matukio kama hayo, Kibiti ni shwari na salama.

Limewataka wananchi kupuuza ujumbe huu pamoja na wote wasioitakia mema nchi yetu.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopo mauaji yanayojumuisha eneo la Mkuranga, Kibiti na Rufiji (MKIRU) yalianza mapema Januari 2015 yakihusishwa na vikundi vya vijana wanaopata mafunzo kutoka kwenye kundi la al-Shabaab nchini Somalia.

Kwa mujibu wa Gazeti la Jamhuri, Kwa miaka minne hadi mitano hadi kuanza kwa mauaji haya, vijana kadhaa kutoka maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Rufiji, hasa Ikwiriri, wamekuwa wakisajiliwa na kundi hilo la kigaidi, huku wazazi wao wakiambulia ujira wa dola 3,000 za Marekani (zaidi ya Sh milioni 6).

Akizungumza na JAMHURI, mmoja wa wakazi wa Ikwiriri ambaye hakupenda kutajwa jina lake gazetini kwa sababu za kiusalama, alisema kumekuwa na wimbi la vijana wenye umri wa miaka 16-25 kupelekwa kwenye mafunzo huko Somalia.

“Hapa Ikwiriri katika kipindi cha miaka kama mitano iliyopita kumekuwa na wimbi la vijana wadogo kupelekwa Somalia. Inasemekana wanakwenda kujiunga na kikundi cha al-Shabaab, lakini vijana hao wamekuwa wanapatikana kupitia kwa mawakala kadhaa kwenye misikiti.

Si kweli kwamba polisi hapa Ikwiriri hawajui, maana hata ukifuatilia wale viongozi wa vijiji ambao wamekuwa wakitoa taarifa za vijana hao wamekuwa wakiuawa kwa staili inayofanana… sasa hapo unaweza kuona namna zoezi (kazi) linavyokuwa gumu,”
alisema.
Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya ndani wakati ule, Mwigulu Nchemba, yeye kwa upande wake aliwahi kunukuliwa akidai "mauaji hayo yana harufu ya kisiasa," na kuhoji "Ujambazi gani huo wa Wana CCM tu? Hako kamchezo tumeshakagundua. Dhahiri, huo ni ushamba wa vyama vingi.”

Waziri Mwigulu alikwenda mbali zaidi na kudai kuwa chanzo cha mauaji hayo ni chuki za vyama vya upinzani dhidi ya CCM.

Aidha, aliyekuwa Rais wa awamu ya 5 Hayati Magufuli aliwahi kuagiza Jeshi la Polisi kuhakikisha linakomesha mauaji haya ya raia wasio na hatia.

Mei 4, 2018, Zitto Kabwe akiwa Mbunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Kiongozi wa Chama, ACT Wazalendo alitoa hotuba Bungeni akibainisha kuwa zaidi ya Watanzania 380 walikuwa wamepotea huko MKIRU.
Soma MWANANCHI

USSR
Wanapenda sana sehemu zenye uwekezaji walianza wakati wa SGR na sasa wakati wa Bandari.

Kule msumbiji wako kwenye muradi ya Gesi na huko Central Africa wako kwenye Uraniam na dhahabu.

Ni kama watu wanatengenezwa makusudi kufukuza Wananchi kiaina.

Tunaamini vyombo vyetu vya ulinzi viko imara na vitashinda tena swala hili.
 
Huwa kuna jambo linaandaliwa,huenda kuna watu wanaviziwa kukamatwa na kupewa kesi za ugaidi ama sirikali inatafuta sababu ya kupiga marufuku mikutano ya kisiasa kwa kisingizio cha usalama!!

Masheikh kabla ya kukamatwa enzi za Kikwete yalimea mambo ya ugaidi.

Jana IGP karindima kuna watu wanataka kupindua Samia!!
 
Watu wameuwa family nzima wewe ualeta story za kusadikika.

Ile kauli ya GP kwa watu makini haikuwa ndogo. Mpake leo natetemeka.
 
Huwa kuna jambo linaandaliwa,huenda kuna watu wanaviziwa kukamatwa na kupewa kesi za ugaidi ama sirikali inatafuta sababu ya kupiga marufuku mikutano ya kisiasa kwa kisingizio cha usalama!!

Masheikh kabla ya kukamatwa enzi za Kikwete yalimea mambo ya ugaidi.

Jana IGP karindima kuna watu wanataka kupindua Samia!!
Huna akili... Ungezika ndugu zako ungeacha propaganda za kishenzi.
 
Huwa kuna jambo linaandaliwa,huenda kuna watu wanaviziwa kukamatwa na kupewa kesi za ugaidi ama sirikali inatafuta sababu ya kupiga marufuku mikutano ya kisiasa kwa kisingizio cha usalama!!

Masheikh kabla ya kukamatwa enzi za Kikwete yalimea mambo ya ugaidi.

Jana IGP karindima kuna watu wanataka kupindua Samia!!
Watu wameuwa family nzima wewe ualeta story za kusadikika.

USSR
 
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom