Matusi kwa Lowassa yanaletwa na sababu zipi?!

BEHOLD

JF-Expert Member
Nov 17, 2013
5,057
10,715
Najiuliza sana kuhusu matusi na kejeli vinavyoelekezwa kwa Lowassa toka CCM.

Hivi kosa la Lowassa ni nini?,

- Kaomba ridhaa ya kugombea na akateuliwa kwa kukidhi vigezo na matakwa ya kisheria,

- Kapitishwa kugombea wananchi kwa mamilioni, Wanawake kwa Waume, Vijana kwa Wazee wamemkubali kwa roho zao na wanamuunga mkono na hakika Edward Lowassa ndiye atakayekuwa Raisi kwa mujibu wa sheria na demokrasia.

Sasa matusi ambayo CCM wanamtukana yanatoka wapi?.

Nadhani anayepaswa kutukana hapa na SHERIA iliyompitisha Lowassa kwa kukidhi vigezo vyake, na WANANCHI waliomuamini na kumtumaini kuwa hakuna mwingine zaidi ya Lowassa.

CCM acheni dhambi mtaliangamiza taifa.
 
Mkuu umeisha wahi kuachwa na demu kwa mbwembwe,halafu ukapata kifaa zaidi yake??????.

the same situation.
 
Mungu Kawatumia Pepo La Matusi Ili Kuwapoteza Kabisa Na Wazidi Kujichimbia Kaburi Kwa Midomo Yao Michafu.
 
Najiuliza sana kuhusu matusi na kejeli vinavyoelekezwa kwa Lowassa toka CCM.

Hivi kosa la Lowassa ni nini?,

- Kaomba ridhaa ya kugombea na akateuliwa kwa kukidhi vigezo na matakwa ya kisheria,

- Kapitishwa kugombea wananchi kwa mamilioni, Wanawake kwa Waume, Vijana kwa Wazee wamemkubali kwa roho zao na wanamuunga mkono na hakika Edward Lowassa ndiye atakayekuwa Raisi kwa mujibu wa sheria na demokrasia.

Sasa matusi ambayo CCM wanamtukana yanatoka wapi?.

Nadhani anayepaswa kutukana hapa na SHERIA iliyompitisha Lowassa kwa kukidhi vigezo vyake, na WANANCHI waliomuamini na kumtumaini kuwa hakuna mwingine zaidi ya Lowassa.

CCM acheni dhambi mtaliangamiza taifa.
Kkutwa fisadi ni tusi? Unayajua matusi wewe
 
Kkutwa fisadi ni tusi? Unayajua matusi wewe

Watu mlishajaa viburi, vya madaraka , ujinga nao ukatamalaki, mkapumbaa ! hamwezi kuuona ukweli, hata ikitokea mkauona hamtaki kuelewa makusudi !

Matusi kwenu ndiyo hekima, na hekima ni matusi. Kweli madaraka hupumbaza, hulevya na kupofusha macho !

Lakini kumbukeni kila kitu kina mwisho, mwisho wenu utafika, ndipo mtakapo adhibiwa na Mungu kwa maneno na matendo yenu.

Kwa matendo haya nadhani hamjuwi hata uwepo wa Mungu. Lakini haitawasaidia mtahukumiwa tu, pasipo sheria.
 
Daaah amenisikitisha sana bwana mshairi ameongea matusi tu hizi siasa za chuki zitatuvurugia nchi sijui kwanini ccm haikemei hawa watu wanavuruga chama,ni wahuni tu washapiga viroba pale akija jukwaani anatukana tu,huku wananchi wanapima tu, kumbe ccm vijana wadogo hawana adabu wanatukana watu wazima hadharani na viongozi wakubwa wapo wanashabikia na kupiga makofi it's a shame, bwana mshairi aliongea neno paka magufuli mwenyewe akashika mdomo ivi ni kweli ametamka hadi hilo. ...lakini anocho nifurahisha eddo hajibu mtu, ananipa somo zuri sana la kujifunza
 
Back
Top Bottom