Matunda ya ziara ya Wang Yi barani Afrika

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,008
1,030
vcbcxvbc.png


Na Ronald Mutie

Kenya, Eritrea na visiwa vya Comoro ndio nchi tatu ambazo waziri wa mambo ya nje wa China alitembelea mwaka huu.

Ziara ya Wang Yi kwenye nchi hizo imeendeleza desturi ya China kwamba safari ya kwanza ya waziri wa mambo ya nje wa China itakuwa Afrika.

Kila ziara huwa na mawasiliano mapya kati ya China na nchi husika na mipango mipya ya ushirikiano hutiwa saini.

Nchini Kenya waziri Wang Ying na mwenzake Raychelle Omamo walitia saini mikataba sita ya kibiashara na kuahidi kuunda kikundi kazi cha pamoja kitakachoshughulikia vikwazo vya kibiashara kati ya nchi hizo mbili na pia kuongeza mauzo ya nje ya Kenya kwenda China.

Katika mazungumzo ya pande hizo mbili Wang Yi, alieleza matumaini kuwa makubaliano hayo yataongeza mauzo ya bidhaa za Kenya kwenda China na kuboresha uchumi wa watu wake.

Kulingana na mkataba huo mpya, katika kilimo, Kenya itasafirisha maparachichi na samaki nchini China.

Katika Wizara ya Ubunifu wa teknolojia ya Habari na Mawasiliamo na Masuala ya Vijana, Kenya iliingia katika makubaliano na Wizara ya Biashara ya China, ambayo yanalenga kutambua uchumi wa kidijitali kama kichocheo muhimu cha ukuaji wa uchumi duniani.

Makubaliano hayo yataruhusu nchi zote mbili kuchunguza maeneo ya ushirikiano wa uwekezaji katika uchumi wa kidijitali unaowiana na dira ya Kenya ya 2030.

Sekta nyingine zitakazonufaika na mpango huo ni usindikaji wa mazao ya kilimo, nguo, usindikaji wa ngozi, viatu, samani, ujenzi miongoni mwa sekta nyinginezo.

Waziri Raychelle Omamo alisema mikataba hiyo sita iliyotiwa saini Alhamisi kati ya Kenya na China itaboresha na kuimarisha mahusiano na ushirikiano kati ya nchi hizo mbili.

“Katika eneo la ushirikiano na afya, China imekubali kutoa mchango wa dozi milioni 10 za chanjo ya Covid-19, chini ya mpango wa dozi bilioni 10 zaidi za chanjo ya Corona kwa nchi za bara la Afrika. Tunawashukuru sana. Pia tumekubaliana kuhusu jinsi ya kusaidia mchango huu kwa kutoa vifaa vya kuhifadhia chanjo na miradi ya pamoja ya uzalishaji wa chanjo na kujenga uwezo wa wafanyakazi wa matibabu”

Aidha Waziri Omamo alisema kuwa ili kupunguza pengo la biashara kati ya nchi hizo mbili, wamekubaliana kuwa Kenya itaongeza mauzo ya bidhaa zake nchini China kama vile maparachichi na samaki.

“Pande zote zinakiri kuongezeka kwa kasi ya biashara baina ya nchi zote mbili na kukiri uwezekano mkubwa wa kuongeza kiwango cha biashara ya nje na thamani kupitia kushughulikia ushuru wa biashara na vikwazo vya biashara ili kukabiliana na nakisi ya biashara ambayo sasa inaipendelea China”

Waziri wa mambo ya nje wa China, Wang Yi alisema kuwa China itaendelea kuiunga mkono Kenya katika kufanikisha ukuaji wa viwanda na uboreshaji wa kisasa kwa kasi ya haraka.

Aidha aliongeza kuwa China itazisaidia nchi za Afrika kukabiliana na changamoto zake ikiwamo umaskini na maendeleo duni.

“Tunavyozungumza hivi sasa, mahitaji katika bara hili yanapanuka. Tumeona mahitaji ya chanjo za covid-19, na mahitaji ya maendeleo bora ya mfumo wa huduma ya afya na matibabu, uchumi wa kidijitali, ubunifu, na miundombinu. Tumepanua ushirikiano na nchi za Afrika kutoka miundombinu hadi maeneo mengine. Lengo letu ni kufikia maendeleo na mafanikio ya pamoja kati ya China na Afrika”

Wang Yi alisema China ingependa kushirikiana na nchi nyingine ambazo ni rafiki kwa nchi za Afrika ili kuondoa umaskini, ukosefu wa maendeleo na kuchangia juhudi za Afrika za kujiletea maendeleo huru na endelevu.

Katika ziara ya Waziri wa mambo ya nje wa China, Wang Yi pia aliandamana na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kukagua maendeleo ya Kituo cha Mafuta cha Kipevu kilicho katika Bandari ya Mombasa kinachotarajiwa kuanza kufanya kazi kufikia Aprili 2022.

Kituo hicho kinajengwa na kampuni ya ujenzi ya China ya CCCC.

Mradi huo ulianza Februari 2019 na kwa sasa umekamilika kwa asilimia 96 ukiwa na gati nne ambazo zitaiwezesha kubeba meli tatu kwa wakati mmoja zenye uwezo wa kubeba tani 200,000 kila moja.

Nchini Eritrea Wang Yi alikutana na Rais Isaias Afwerki na pande hizo mbili kubadilishana mawazo kuhusu hali ya Pembe ya Afrika.

Isaias alisema, Eritrea inapinga vikali kuundwa kwa migawanyiko ya kijamii na migogoro ya kikabila katika eneo hilo na vikosi vya nje. Alisema anatarajia China itachukua nafasi kubwa zaidi katika mchakato wa amani na maendeleo ya Afrika.

Aidha Isaias alipinga usemi unaoitwa "mtego wa madeni" wa China, akisisitiza kwamba China haijawahi kuingilia masuala ya ndani ya nchi nyingine na ni mshirika wa kweli wa maendeleo wa Afrika.

Wang Yi alisema, katika miaka ya hivi karibuni, baadhi ya nchi kubwa nje ya eneo hilo zimetumia Pembe ya Afrika kama uwanja wa michezo ya kisiasa ya kijiografia, na kusababisha machafuko - na migogoro ya mara kwa mara, kudhoofisha kwa kiasi kikubwa amani na utulivu wa kikanda, na kupunguza kasi ya maendeleo.

Na kwenye visiwa vya Comoro Waziri Wang Yi alikutana na Rais Azali Assoumani.

Alisema kuwa China iko tayari kuwa mshirika wa kutegemewa wa muda mrefu wa Comoro, na kuwa nchi yake iko tayari kusaidia Comoro kufikia malengo matatu, ambayo ni kufikisha chanjo kwa wote ndani ya mwaka huu, kutokomeza kabisa ugonjwa wa Malaria ifikapo 2025 na kuunga mkono Mpango wa Comoro wa mwaka 2030 ambao ni mkakati wa maendeleo.

Vile vile aliangazia jukumu la urafiki kati ya China na Comoro, Baraza la Ushirikiano kati ya China na nchi za Kiarabu na Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika, katika kutoa msukumo zaidi katika maendeleo na maendeleo ya Comoro.

Rais Azali alipongeza mpango mkuu wa ushirikiano na Afrika uliotangazwa na Rais wa China Xi Jinping na kuishukuru China kwa kuziunga mkono nchi za Afrika katika kulinda haki na maslahi yao halali katika Umoja wa Mataifa.
 
Kama tunadhani China ni rafiki wa kweli wa Africa basi tunapaswa kupimwa akili zetu kama ziko sawa ama la...! Ya Kenya Uganda na Zambia nj tahadhari tosha kabisa ya huru rafiki usoni, adui moyoni
 
Back
Top Bottom