Matumizi ya vyandarua vya mbu (the mosquito-nets uses)

busy bees

JF-Expert Member
Aug 26, 2016
2,249
1,332
Serikali kupitia Wizara ya Afya ya Jamii imekuwa na mkakati wa kupambana na Malaria kwa wananchi wote mijini na vijijini hasa WATOTO na MAMA WAJAWAZITO.

VYANDARUA vingi VYENYE DAWA vimesambazwa bure katika jitihada hizo za kupunguza kama si kuondoa kabisa VIFO vitokanavyo na MALARIA.

Yafuatayo hapa chini ndo MATUMIZI ya VYANDARUA hivyo VILIVYOTIWA DAWA.:.

1)Kujikinga/kujizuia na mbu waenezao Malaria.

2)Kuwazuia/kuwakinga kuku, bata, kanga nk wasiliwe na mwewe/kunguru.

3)Kutumika kama uzio katika bustani ya mboga.

4)Kutumika kama "nets" za kuvulia samaki.

TOA MAONI YAKO
 
Kuna tetesi kwamba hizi net zenye dawa si salama kwa binadamu na zina madhara kwa mtumiaji je kuna ukweli????

Niliitumia siku moja tu baada ya kuskia haya nikaitupa kabisa!!! Na mpaka leo nikinunua net sitaki ngao
 
Kiwazuia kuku nk wasiliwe na kunguru.....Huwa tunatumia NET zilizochakaa kwa kazi hiyo.Ukichuunguza utakuta zina matundu yanayoweza pitisha hata mende kwa ukubwa.Hali kadhalika ktk uzio zitumikazo ni zile chakavu.
 
Net mpya nyingi sana nimeshuhudia zikitumika kwa kazi ya kuzuia vifaranga wa kuku wasiliwe
 
20acres.......Inawezekana labda hizo net zilikuwa ndogo jamaa akabadilisha matumizi.Kwa huku kwetu TZ ni very possible.Tuwaambie wananchi wapatapo net ndogo wasisite kuwapa wenye vitanda vidogo wazitumie au wazipeleke mashuleni.
 
nadhani serikali kupitia wizara ya afya ilipaswa kutoa elimu yakutosha kwa wanainchi kuhusiana na matumizi sahihi ya vyandarua...
 
Kiwazuia kuku nk wasiliwe na kunguru.....Huwa tunatumia NET zilizochakaa kwa kazi hiyo.Ukichuunguza utakuta zina matundu yanayoweza pitisha hata mende kwa ukubwa.Hali kadhalika ktk uzio zitumikazo ni zile chakavu.
Yawezekana kwa maeneo ya kwenu mwatumia hizo zilizochakaa .... but mie niliskia kauli ya mwananch mmoja akisema, ..." ninaamini sasa kuku na kanga wangu sasa watasalimika" ....

Kauli hiyo aliitoa nje kidogo tu ya ofisi ya mtendaji wa kijiji mda mfupi baada ya kukabidhiwa nets zake 3 ..... Lakini pia nimeshudia sehemu tofauti tatu , 2 vyandarua (vipya) vikiwakinga kuku na1 bustani ya mboga
 
Situmiagi hizo net...nikitumia napumua kwa shida na joto jingi mno... nikija kwako kama wewe unatumia chandarua nalala zangu kwenye kochi inatoshaa
 
nadhani serikali kupitia wizara ya afya ilipaswa kutoa elimu yakutosha kwa wanainchi kuhusiana na matumizi sahihi ya vyandarua...
Exactly .... yawezekana ingepunguza hii "misuse" .... by the way kuna "people" zingine vichwa ngumu .... cku zote wanakuwa against na ndo maamuz yanakuw "kuwaponya kuku" huku binadamu wakiangamia

Wakati mwingine "rumors/ hearsays" huwa sababu ... mfano ni hiyo ya vyandarua kuua NGUVU ZA KIUME .......... ni sawa na zile pesa za TASAF zilipotoswa na baadhi ya watu kwa kuambiwa ni pesa ya FREEMASON
 
Net mpya nyingi sana nimeshuhudia zikitumika kwa kazi ya kuzuia vifaranga wa kuku wasiliwe
Exactly mkuu .... maeneo ni mengi sana tu ..... kuku wanapeta but watu wananyong'onyea na malaria
 
Back
Top Bottom