Matumizi ya simu wakati wa mvua yanaweza kuleta madhara endapo radi itapiga?

Tohoa

Member
Sep 13, 2021
28
17
Mkuu wa polisi hapa Arusha katutahadhalisha matumizi ya simu wakati wa mvua yanaweza kusababisha RADI.

Hii kweli inawezekana jamani?

Wenye kujua hili naomba ufafanuzi
 
Kulingana Na Swali Lililopo Kwenye Kichwa Cha Uzi Ni Kweli Matumizi Ya Simu Wakati Mvua Zilizoambatana Na Radi Zikipiga Kunaweza Leta Madhara Makubwa Kwa Mtumiaji Wa Simu.

Tofauti Na Content Ya Uzi Ulivyoandika Kuwa Ukitumia Simu Wakati Wa Mvua Kunaweza Kuleta Radi Hicho Hapana. Matumizi Ya Simu Hayasababishi Kutokea Radi.

Ila Matumizi Yako Ya Simu Yanaweza Kusababisha Wewe Kupigwa Radi Kama Mvua Hizo Zimeambatana Na Radi.

Pia Si Hadi Kuwe Na Mvua Kukiwa Na Radi Tu Unaweza Kupata Madhara Kama Unatumia Vitaa Vya Umeme(Simu,Decoder n.k)
 
Hakuna connection yoyote kati ya vifaa kama simu,wireless earphones,Laptop n.k na radi. Wala radi haiwezi kumuathiri mtumiaji wa vifaa hivyo (unconnected devices) .Hii ndiyo madhara ya askari wetu kuishia darasa la saba na kukosa elimu juu ya mambo madogo kama haya
Sure
 
Iko hivi; radi hupiga sehem yenye mlolongo wa kwenda ardhini ambao umejitokeza juu!

Kutumia simu wakati wa mvua iliyoambatana na radi hakuwezi kusababisha mtumiaji kudhulika na radi;

Kwanini?
Kwa sababu simu hutumia masafa ya wireless ( unconnected) ambayo ni electromagnetic waves kutoka kwenye antenna au minara ya simu. Mawimbi haya hayawezi kuwa conductor au kipitishi cha umeme wa radi.

Mtumiaji wa simu anaweza tu kudhurika kwa radi endapo;
1.atakuwa ameunganisha simu yake kwenye extension cable ( kebo) anapochaji simu. Ikiwa radi itaingilia mfumo wa wiring za nyumbani basi simu itapokea umeme mwingi kupita kiasi na kupelekea madhara kwa mtumiaji.

2. Pia cha kuzingatia sana, zima TV ikiwa unatumia antenna, TV cable, au dish maana umeme wa radi unaweza kupitia dishi hadi ndani haraka sana na kuleta madhara.
 
Mkuu wa polisi hapa Arusha katutahadhalisha matumizi ya simu wakati wa mvua yanaweza kusababisha RADI.

Hii kweli inawezekana jamani?

Wenye kujua hili naomba ufafanuzi
Nimegugu kama RC wangu nikapata hii...jielemishe
Screenshot_20220219-153637_Chrome.jpg
 
Hakuna connection yoyote kati ya vifaa kama simu,wireless earphones,Laptop n.k na radi. Wala radi haiwezi kumuathiri mtumiaji wa vifaa hivyo (unconnected devices) .Hii ndiyo madhara ya askari wetu kuishia darasa la saba na kukosa elimu juu ya mambo madogo kama haya
Mkuu, umeanza vizuri sana, ila umemalizia vibaya sana!
 
Iko hivi; radi hupiga sehem yenye mlolongo wa kwenda ardhini ambao umejitokeza juu!

Kutumia simu wakati wa mvua iliyoambatana na radi hakuwezi kusababisha mtumiaji kudhulika na radi;

Kwanini?
Kwa sababu simu hutumia masafa ya wireless ( unconnected) ambayo ni electromagnetic waves kutoka kwenye antenna au minara ya simu. Mawimbi haya hayawezi kuwa conductor au kipitishi cha umeme wa radi.

Mtumiaji wa simu anaweza tu kudhurika kwa radi endapo;
1.atakuwa ameunganisha simu yake kwenye extension cable ( kebo) anapochaji simu. Ikiwa radi itaingilia mfumo wa wiring za nyumbani basi simu itapokea umeme mwingi kupita kiasi na kupelekea madhara kwa mtumiaji.

2. Pia cha kuzingatia sana, zima TV ikiwa unatumia antenna, TV cable, au dish maana umeme wa radi unaweza kupitia dishi hadi ndani haraka sana na kuleta madhara.
umemaliza kila kitu,ambaye hata elewa hapa basi hatokaa aelewe maisha yake yote
 
Hakuna connection yoyote kati ya vifaa kama simu,wireless earphones,Laptop n.k na radi. Wala radi haiwezi kumuathiri mtumiaji wa vifaa hivyo (unconnected devices) .Hii ndiyo madhara ya askari wetu kuishia darasa la saba na kukosa elimu juu ya mambo madogo kama haya
Acha ujinga. Mawimbi ya simu yanaingiliana na ya simu esp ikiwah
Iko hivi; radi hupiga sehem yenye mlolongo wa kwenda ardhini ambao umejitokeza juu!

Kutumia simu wakati wa mvua iliyoambatana na radi hakuwezi kusababisha mtumiaji kudhulika na radi;

Kwanini?
Kwa sababu simu hutumia masafa ya wireless ( unconnected) ambayo ni electromagnetic waves kutoka kwenye antenna au minara ya simu. Mawimbi haya hayawezi kuwa conductor au kipitishi cha umeme wa radi.

Mtumiaji wa simu anaweza tu kudhurika kwa radi endapo;
1.atakuwa ameunganisha simu yake kwenye extension cable ( kebo) anapochaji simu. Ikiwa radi itaingilia mfumo wa wiring za nyumbani basi simu itapokea umeme mwingi kupita kiasi na kupelekea madhara kwa mtumiaji.

2. Pia cha kuzingatia sana, zima TV ikiwa unatumia antenna, TV cable, au dish maana umeme wa radi unaweza kupitia dishi hadi ndani haraka sana na kuleta madhara.
Hapo 2 sio kuzima tu. Disconnect kabisa
 
may be ikiwa connected kwenye socket ambayo inabeba umeme,lightining inaweza kustrike wire wa umeme na kuwa conducted through it na kufikia simu yako iliyokuwa connected hapo.
 
askari wa Tz ni vilaza, ona sasa komrediz wamepaniki , siredi ya tatu hii tangu ile barua ya ovyo ya yule kilaza itoke

hakuna konekshen yoyote kati ya radi na simu
 
Watu hawasomi. Maarifa yamejaa mitandaoni.
Hakuna connection ya radi na vifaa ambavyo ni wirelessly connected.
 
Hakuna connection yoyote kati ya vifaa kama simu,wireless earphones,Laptop n.k na radi. Wala radi haiwezi kumuathiri mtumiaji wa vifaa hivyo (unconnected devices) .Hii ndiyo madhara ya askari wetu kuishia darasa la saba na kukosa elimu juu ya mambo madogo kama haya
Kuna mwalimu wangu wa Arusha Technic College,aliwahi kutuambia hv kuwa mtu hawez dhurika akiwa anatumia vifaa vya umeme

Lakin huku kwetu kuna matukio kama manne yaliwah kutokea watu kupigwa na radi wakat wakiwa wanatumia vifaa vya kielectronic

Matatu ni ya watu wanabonyeza simu,tukio moja walipigwa watu watatu pamoja na huyo aliekuwa ana bonyeza sm,kwasasa huku kwetu ukitumia sm wakat mvua inanyesha watu wanakukimbia au wanakufukuza

Tukio lingine alkuwa mchunga ng'ombe anasikiliza redio,alikutwa ameanguka ameshakufa tayar na redio imepasuka

Kutokana na maneno ya mtaalam wangu(mwalimu),nimeconclude kuwa ukiwa ndan kama unatumia kifaa cha kielectronic huwez pigwa radi ila kifaa kinaweza pata tatzo radi ikipiga
Lakin kama utakuwa nje ya nyumba ukiwa unatumia kifaa cha kielectronic basi utapigwa na radi
 
Mwaka 2012 pale UDOM,College of Social Science and Humanities palikua na manyunyu yaliyoambatana na radi.
Kuna mshkaji mmoja alikua na wenzake watatu, yeye akawa anaongea na simu hivyo akawaacha hatua kadhaa akawa anaendelea kuongea kwenye simu.
Ilishuka radi ikamchukua pale pale yule mshkaji waliokuwa karibu yake walijeruhiwa.
Mtalaamu mmoja akasema kuna baadhi ya simu hazijawekwa system ya earth ili kuzuia radi hivyo ni vema tuwe makini.
Kutoka 2012 mpaka leo 2022, ni miaka 10 labda kuna maboresho makubwa yamefanyikwa kwenye simu zote.
 
Back
Top Bottom