Matumizi ya simu katika Mahusiano

Nashanga! Yani na karne hii ya utandawazi mtu bado unapekua simu, utakufa kwa kihoro! Watu twaweza kukuachia simu tukawasiliana kwa email....... simu zinakaririwa namba kichwani unatumia simu ya swahiba wako kuwasiliana na mpango wa nje........
 
Hapo umelenga, unajua mume unapojifanya mpelelezi wa mkeo wakati hujasomea kazi hiyo hapo ndo utata unapoanzaga. Kama huyo mwanamke sio mwaminifu we acha tu utaona usijepata presha kwa jambo usilolijua, just lipe hilo suala muda. Afu pia sometimes Gubu la mwanaume linamfanya mwanamke awe mwoga kwenye ndoa yake hivyo kuwa na nidhamu ya uwoga, hivyo kuepusha anaamua kuwa na simu nyingine kwa ajili ya kuwasiliana na ndugu, jamaa na marafiki awapo ofisini kuepusha shari. Mpe mkeo uhuru wenye mipaka na usimchukulie muda wote kama mtuhumiwa. Wapenzi mkichunguzana sana hamfiki mbali bra!!!
 
Hommie kuna wengine wanawawekea watu wao priveti investigeta, natamani hiyo pesa wangekua wanaleta pale king star tuburudike nayo!
 

Picha ninayoiona hapo ni vimwelumwelu tu,acha kuchunguza sana utapata presha bure,simu tu ungegundua ana bwana hapo hata polisi ungeenda, simu tu tena anaicha ofisini ambapo ww haikukwazi kwa lolote, achana na hayo mambo songesha maisha,mwizi zake 40 km ni kweli ina matumizi tofauti ikifika ukweli tajulikana tu.
 
Hommie kuna wengine wanawawekea watu wao priveti investigeta, natamani hiyo pesa wangekua wanaleta pale king star tuburudike nayo!
Kimsingi badala ya kutumia resources kama time na fedha kumchunguza mkeo, better ukae chini kujichunguza wewe mwenyewe tatizo ni nini hadi mke wangu anakuwa na tabia tofauti na unavyotarajia, usikute wewe ndo chanzo cha tatizo pengine huwajibiki nyumbani so dawa ni kujituma na sio kuchunguza mkeo. Kwa kweli naamini kama kila kitu kinaenda sawa, hakuna mwanandoa anayependa kurukaruka na kumdhalilisha mwenzake au ndoa yake, maana hili suala kwa ujumla wake limegubikwa na aibu kubwa.
 
mie nawashangaa kabisa siku hizi natazama yale yaliyo yangu mengine nawaachia wenye nguvu zao .............na mashida yote ya karne hii ukajilundike mawazo yasiyo na tija.


Nashanga! Yani na karne hii ya utandawazi mtu bado unapekua simu, utakufa kwa kihoro! Watu twaweza kukuachia simu tukawasiliana kwa email....... simu zinakaririwa namba kichwani unatumia simu ya swahiba wako kuwasiliana na mpango wa nje........
 
Swala kusema ni simu ya ofisini halipo..ilikuja kugundulika ana simu nyingine ni pale alipopigiwa simu yake inayojulikana ikawa haipatikani akapigiwa staff mwenzake na bila wasiwasi alijibu hebu mcheck kwenye ile simu yake nyingine....kama ni ya ofisi hata staff wenzake wasiijue?
 
maana yake mkeo anauza mechi. Na anatumia simu anayoiacha ofsn kuwasiliana na mahawara zake.

Vunja ukimya kaka,unaibiwa

 

Runner hakuna siri baina ya wanandoa? kweli? Hivi duniani humu kweli kuna binadamu ambaye hana siri zake binafsi? Hata wewe Runner una yako binafsi ambayo kamwe hujawahi kumwambia mkeo,jichunguze tu nafsi yako utakubaliana na mimi.
 
maybe ni kuboresha penzi lenu aliinunua ili awe anakutest km mtu mwingine dont take things negatively all the time.

majaribu mengine yanazua utata
 
sasa na ww ulikuwaje ukaskia hayo maelekezo ya staff mwenzie na mkeo akisema aangaliwe kwenye ile simu yake nyingine? na mtu akipewa blackberry ya ofc ataacha kuiita ya kwake? mean,huwezi kusema simu ya runner imeharibika,aletewe ingine?
 
Inaleta picha nzuri, kwamba anatofautisha pasono ishuzi na Ofisho wanz
 

Kama ni simu ya kazini sioni mbaya kuiacha kwani inategemea na kampuni anayofanyia kazi na bosi wake wanaishije, kuna kampuni nyingine ikifika muda wa kufunga ofisiunazima simu inawekwa kwenye droo kungoja kesho, mfano hai ni wifi yangu yeye anafanya kazi serikalini na alipewa simu kwa ajiliya kazini kuwasiliana na wateja ikatokea siku aliibiwa ile simu ya kazini pamoja na yake kuripoti kazini alifokewa na kuulizwa nani alimparuksa ya kwenda nayo nyumbani akaamriwa ailipe tangu siku hiyo haondoki na simu ya kazini ikifika saa10 inazimwa kwenye kabati
 
Nadhani elezea vizuri kama anaiacha ofisini wewe ulijuwaje kuwa ana simu nyingine ambayo namba yake huijuwi?ina maana utoe maelezo zaidi ili tujuwe jinsi ulivyogundua kuwa ana simu nyingine!!
 
Hommie kuna wengine wanawawekea watu wao priveti investigeta, natamani hiyo pesa wangekua wanaleta pale king star tuburudike nayo!
Hili wallah ni kama Neno la Mungu vile!..........Waambie walete hiyo sadaka King Star tunywe divai bana!

mulika mwizi mazee!
Mke/mme wako ni wako akiwa kwako, akitoka nje si wako! Ukimfuatilia sana unataka ufe siku si zako!
 
Mkuu Runner, nafikiri ingekuwa vyema sana ungetupa kisa kilichokufanya ugundue kuwa kuna simu nyingine ofisini. Labda kwa kupitia hilo ndo mtu unaweza kujudge ilikuwa ina malengo gani. Otherwise: Kuna mawili kama wengine walivyotangulia kusema yaweza kuwa positive au negative sio lazima sana iwe ni kwa kukosa uaminifu. Watu hutofautiana, wengine hawana hulka ya kuweka kila kitu wazi kwa wenzao hata kama ni mume/mke. Inategemea na namna ambavyo nyie mnawasiliana na kushirikishana ishu zenu.
 
Huyu mtu atakuwa ana tabia za wiziwizi enje ya ndoa. kwa nini aache simu officin hata kama ni ya ofici na ni ya kiganjani anatakiwa kuwa nayo through out hadi atakapoachishwa kazi ndo anarudisha...wewe mumeye be careful-wizi mtupu!!

 
funny thing,hizi simu utasema zilikuwepo enzi za adam na hawa....kumbe zimekuja juzi lol
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…