Matumizi ya Neno Mkuu JF.

Stroke

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2012
Posts
40,147
Reaction score
51,298
Naona siku za hivi karibuni neno Mkuu limepungua kasi katika matumizi yake ila kwa wakongwe sio geni sana.

Matumizi ya neno Mkuu yalikuja kutokana na hulka ya watumiaji wa JF kutotumia majina halisi.

Hulka ya kutotumia majina halisi au "fake Id' ilileta kuficha the real identity ya member.

Kwakuwa the real identity ya member haifahamiki, hivyo member wakaamua kuanza .matumizi ya neno "mkuu" kupeana heshima tu kwani "fake Ids" zinaficha status ya mtu.

Huwezi juwa elimu, kipato , umri , jinsia au cheo chake. Hivyo neno mkuu linabeba yote hayo.

Yangu machache. ( my few cents).
 
Unaingiza kiasi cha pesa ukiitwa hivyo? Kwangu mimi binafsi haijalishi nimekua humu kwa muda gani ila neno mkuu kwangu mimi ninaichukulia km salute au kufanya appreciation ya kile mtu amesema ndani ya mada husika au kumuwasilishia utambuzi wa heshima, hio ni kwa mimi ukiona nimekuita mkuu maana yake umeeleta kitu kimenigusa na nime-appreciate kile umesema and you deserve kua appreciated na hii mara nyinyi ni kwa wale wenye heshima wale namna gani naruka nao namna gani hivyo yaan

Nasikia usingizi ila silali sahizi
 
Ungependa litumike vipi mkuu.
Naona kama Mdau limekaa poa

Huwa natumia ndugu, rafiki, nk

Nyimbo zote za kidini zenye neno mkuu napata ukakasi kuzisikiliza

I have mental issues
 
Naona kama Mdau limekaa poa

Huwa natumia ndugu, rafiki, nk

Nyimbo zote za kidini zenye neno mkuu napata ukakasi kuzisikiliza

I have mental issues
Mdau linakuwa limited sana mkuu,

Maana huyu anakuwa mtu ambaye mnahusiana katika mambo fulani.

Majority ya members hatufahamiani utambulisho wetu halisi.
 
Mdau linakuwa limited sana mkuu,

Maana huyu anakuwa mtu ambaye mnahusiana katika mambo fulani.

Majority ya members hatufahamiani utambulisho wetu halisi.
Mtaani naitwa Mwenyekiti, faza, mshua, mwarabu...haya majina ambayo nimeyazoea

Nikiwa shuleni walikuwa wananiita Albino, sope, fataki....

JF tupumzishane kwenye majina

Kama mdau halifai

Tuitane waheshimiwa kama wanavyoitana bungeni

Hili ni bunge pia
 
Sasa mkuu ndugu pamoja na uwasilishaji wa hoja yako mimi nitapenda nikuulize swali moja
 
Kuna verified members tunawajua kwa sura na kazi wanazofanya hasa hawa wanaotumia majina yao halisi still tunaendelea kuwaita mkuu. Mfano ni huyu member maarufu anayepaita humu jamvini na nyuzi huziita bandiko
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…