Matumizi ya Kiswahili katika Sayansi na Technolojia

Ntamb

Member
Feb 13, 2008
18
0
Waungwana,
Nimekuwa nikitafuta kamusi ya kiswahili inayoweza kukidhi fani kama za Kompyuta, Internet na Telecommunication, bila mafanikio.

Kama kuna mtu yeyote anafahamu ni juhudi gani zinafanyika ili kuhakikisha tunaweza kuwafundisha watoto wetu shule za msingi, mambo ya Information and Communication Technology (ICT).

Bila kuwepo na tafsiri nzuri tutaishia kila mwalimu kutunga neno lake. Mfano nimeona ukurasa fulani ambapo webmaster aliita 'password' :"Neno pita". Ilinishangaza kidogo. Nilitegemea kitu kama "Neno siri", "ufunguo" nk.

Thadeo.
 
Pole sana kaka kwa kutatitizika kwa hayo, lakini nafikiri hizo kamusi za maneno ya kisayansi na mawasiliano zipo na zinapatikana, tembelea Taasisi ya Kiswahili Chuo Kikuu D'salaam ulizia utazipata.

Pia kuhusu hilo la kutumia maneno ambayo hayaendani au hayaleti mashiko au usahihi wa kimaana ni tatizo letu sie wenyewe kutofatilia lugha yetu.

Japo lugha hubadilika kila siku ni lazima sie wazungumzaji wazawa tuwe kama kioo cha maendeleo hayo, si kazi ya kuwaachia wageni ambao hutuletea madudu tu katika lugha yetu.

Kwa ushauri kwa waswahili wenzangu nawaombeni tujitahidi kujisomea mambo yanayohusu lugha yetu ili ishike mizizi miongoni mwetu.

Hakika lugha yetu ya kiswahili ni shani na yenye thamani kubwa, tuilee na tuipambe.

KISWAHILI LUGHA YETU
TUIPENDE
 
Swahilian,

Niko mbali kidogo na UDSM, nitaingia kwenye tovuti yao nione kama nitapata chochote.
Nashukuru kusikia kwamba nakala zilizochapishwa zinapatikana. Basi nitatafuta mtu pale niwasiliane nao moja kwa moja.
 
Hivi kuna kikundi chochote kinachotafiti, namna ya kuhakikisha Kiswahili kinakuwa lugha ya nguvu, katika kufanikisha EAC, conflict resolutions, biashara nk. Natumaini mkakati kama huo upo, vinginevyo itakuwa ni zile siasa za Chema chajiuza na kibaya chajitembeza, nadhani.

Ukiangalia hata mashuleni kwetu, shule za msingi, mtoto anafundishwa kila kitu kwa kiswahili, halafu mara akiwa sekondari kila kitu kinageuka kuwa kwa kiingereza. Hatuoni kama hii inaleta "shock" kwa vijana wetu na kuchangia sana katika kupata elimu finyu?

Nina maana ya kikundi kinachofanya kazi nje ya serikali, na kuangalia mambo "from out of the box". Au wengine mnalionaje?
 
Thadeo: Mimi mzungu ambaye ninajaribu sana kukwepa upotoshaji wa lugha ya Kiswahili. Wengi waongeao Kiswahili kwa asili hufanya mambo mazuri na mambo mabaya katika fani za kuendeleza na kukuza lugha hiyo. Kwangu ni uraibu kupekuapekua vyanzo vya lugha nipate vielelezo vya kazi ambayo watu mbalimbali hutumia ili Kiswahili kipanuke. Narukia maneno mapya ya kikompyuta kila mara huniangukia machoni! Miongoni mwao yako yanayonipendeza na mengine yasiyonipendeza.
Ukitaka kuangalia mkusanyiko wangu wa maneno yenye uhusiano na mambo ya kitarakirishi, nitumie anwani yako ya barua pepe. (ya kwangu: klf100@iolfree.ie) Wewe utaweza kunoa na kurekebisha uteuzi wangu kama upendavyo.
Ningeweza kukuteremshia "kamusi" ndogo hii kwa njia ya mtandao. Niambie kwamba mfumo wako wa uchakataji wa matini ni Word 2003 au Word 2007.
 
Back
Top Bottom