Matumizi sahihi ya Home theatre Nyumbani

Leo ningependa tufahamu tofauti ya music system tunazofunga ndani na matakwa yetu kwa kile tunachotaka kupata nyumbani.

Najua home theatre system ni maarufu kwa wengi wetu na wengi tunapotaka kubadili music system kutoka sub woofer za kichina tunakwenda kuzinunua hizi home theatre .

Lakin ni rahsi kusikia mtu anakuja hapa tena nakutofuraia muziki au nguvu aliotarajia japo katumia pesa nyingi.

Kupata sound bora ya muziki ni gharama kulinganisha na kipato cha watanzania wengi wakawaida, lakini kujua sound bora ni jambo jingine, nakujua music system bora ni utaalam au uwezo binafsi.

Kwa mfano kuna baadhi yetu bass ikiwa kubwa, hio tayari ni system bora kwake, wengine ikipiga makelele sana mpaka mtaa wa sita wakasikia hata kama hakuna ubora na sound yenye viwango hiyo kwakwe ni "The Best". Kujua sound ya viwango ni jambo jingine.

Nisichoshe niende kwenye kiini.

Hi fi Audio system( high fidelity ) system mara nyingi huwa na speaker mbili, zikiwa zimetegenezwa maalumu kutoa muziki katika stereo signal ikifahamika kama 2.0View attachment 318932

Mpangilio wa speaker zake upo katika range ya bass, mid and stereo

Imetengenezwa maalum kutoa "true music" muziki halisi au walau muziki sawa sawa na ulivopangiliwa studio na watengenezaji.View attachment 318931

Maana yake ukiwa na hii "hi-fi system", muziki umepata mahala pake, gonga muziki kulingana na uwezo wako utapata radha, kila chombo walau kilicho ndani ya wimbo husika utakipata kadri kilivopigwa.

Ubora hutofautiana kulingana na bei

Home theatre Audio system

Hizi zinatumia speaker nyingi kiasi, kuanzia walau tano 5.1, au sana 7.1 na kuendelea

Ile 5 ina simama kumaanisha speaker ndogo tano kwa subwoofer 1 kwa ufupi 5.1

Ni teknolojia katika ulimwengu wa kidigitali katika kuleta maisha ya cinema nyumbani mwako.

Ni maalumu kwa DVD, blue ray Disc nk. Inakupa mwonjo wa sound ya movie katika ubora wake, na ndio sababu ya speaker nyingi. Zipo speaker za louder, effects nk nk

Kwanini? Kwasababu siku hizi movies zinatengenezwa na multi sound, na effects kibao, hapa kila speaker zipo kwaajili ya kukupa feel ya movies, feel at the cinema theatre. Katika kuchangia watu humu wanajua watazichambua.

Haikupi muziki halisi, (true music) ila inaweza kukupa feel halisi ya movies, kulinganisha na Hi fi system

Imetengenezwa kwaajili ya cinema nyumbani sio muziki.

USHAURI
Nunua home theatre kama unalenga DVD , au matumizi ya Audiovisual

Lkn kama unataka Kuuhisi muziki na raha zake nunua high fidelity audio system.

Nimegusia, uzoefu wenu pia ni muhimu kwa system muziki wa nyumbani/ndani

----------------------updates----------------
Nitakuja...

16/09/2018 mdau amekuja inbox na kuuliza swali hili:

Nna LG home theater ina spika 4 ndefu na moja ndogo..ila nki-connect zote znaimba mbili tu. .sasa cjajua nakosea kwenye setting au ni nin

JiBu: Kwakweli hili ni swali zuri na linatoa mwanga mkubwa wa nilichoeleza hapo juu kuhusu tofauti ya Home thietre na Hi-fi music system.

Bila shaka wengi hili mmekutana nalo na pengine lipo na hujagundua kabisa hilo suala.

Rejea topic nilisema Muziki studio unatengenezwa katika mfumo wa chanel mbili tu (2.0) stereo. yani inakuwa left and right chanel. Ndio maana pia nilieleza hi-fi system huwa kwa kawaida zinakuwa na speaker 2 tu, for left chanel and right. 2.0 stereo

Home thietre inakuwa na tano, 5.1 au saba, 7.1 nakuendelea, maana yake katika movies kunakuwa na chanel nyingi, sound, effects, kicks, stunts sound hivo zinawekwa katika chanel tofauti, na ni rahisi kama unaangalia movie ukasikia effect ya ngumi ikasikika katika spika za mbele tu, wakati huo mlio.wa gari ukasikika spika za pembeni na ikapigwa risasi ikasikika katika spika nyingine lakini sio zote kwa pamoja.

Vivyo hivyo uwezi sikia muziki katika spika zote za home thietre ispokuwa mbili tu kwasababu kwa kawaida muziki unapoandaliwa studio huwa katika chanel izo mbili, hivyo hauwezi kuwa multiplied katika spika 5 au 7, na ikitokea katika settings ikakubali (japo system bora hazina hiyo setting) basi ndio ubora wake ushakuwa affected, lazima kuna distortion katika baadhi ya spika na zile mbili Main ubora utashuka.

Unaweza pia kama ni computer inasukuma ukaweka mixer kwaajili ya speaker fill, ukajaza zote tano au saba za home thietre yako

Na rahisisha kwakusema hujakosea kuseti home thietre yako ila unapopiga muziki wa chanel mbili 2.0 stereo, lazima nyingine zikae kimya maana hazina feed, lakini chukua movie ya holywood saizi uweke hapo zitapiga spika zote.

KARIBUNI
Asant kwa elimu
 
duuuh niliona mwisho ni 11.2. Kumbe kuna 13.2
1537275225220.png

The Denon Flagship AVR-X8500H powers the next generation of home theater with the world’s first 13.2 channel receiver that supports the latest immersive audio formats, including IMAX Enhanced, Dolby Atmos, DTS:X and unparalleled music playback options, thanks to our built-in HEOS technology, Apple AirPlay 2, and Amazon Alexa voice compatibility for seamless control.
 
View attachment 869994

dola ngapi hii huko amazon
 
Vp elimu ya mpangilio wa music system ndani?? Tunaisubiri pia mkuu..

Pia wengi wanasema hii home theater ni soround na ukiipangilia vizuri speakers unapata music mzuri..

Tupe ufafanuzi.
Mfano vile vitoto vya spika unavihang kwenye angle za sebure yako juu kweny kona zote nne, halafu saaa baba lao unaweka chini kweny kona, na ili ikite zaidi usiweke ndani ya ile case ya tv, weka kweny sakafu, chini itangulie kikapeti ya manyoya... Baba ndani utapapenda
 
Nimeufuatilia huu uzi tangu mwanzo hadi post ya mwisho. Kuna vitu nimejifunza na pia nimepata kuona hulka za watu juu ya viti vyao, wapo wakurupukaji na tupo tunaojifunza.
Suala la kuchagua aina gani ya music uweke nyumbani kwako inategemeana na ushabiki wako binafsi. Mathalani mie binafsi ni mpenzi wa action na horror movies. Kwa mantiki hiyo ndio maana napenda sana home theatre kwa ajili ya kuaccomodate sound effects za movies. Ila pia ndani ya home theatre kuna options za sauti kama wataka music sound, speech, live , orchestra etc. So hapo kama wasikiliza muziki wako, unao uwezo wa kuadjust speaker ikatoa kama HiFi ukawa na 2.0 active channels ambazo ni FL & FR, (Centre na surround speakers zinakuwa turned off kwa muda huo)
Nimeona zimetajwa brand nyingi za kutisha, ila tungejadiliana kulingana na market supply yetu ingekaa poa sana. Kwa hapa TZ tunapata sana bidhaa za Asia specifically za Korea (Samsung na LG), za Japan (Sony, Panasonic kwa uchache sana, Hitachi kwa uchache pia N.K), za China ndio usiseme kwa kuwa ni more than affordable ila hatuna za Europe wala America unless uagize au utoke nayo huko.
Tunapoangalia ubora kwa hizo basi ndio maana Sony amekuwa named the best kwa kuwa wengi hatujui beyond sony.
Practically Samsung na LG upande wa Audio systems hawamgusi Sony na ndio maana wengi wamefanya Sony kama ndio benchmark.

........nitarudi...........
Karibu sana.
Maoni yako ni muhimu.
Tupo hapa kuelimishana and as an avid sound system enthusiat ningependa kujifunza toka kwako.
Mleta mada ameeleza vizuri sana matumizi ya hi-fi na home theaters.
Uko sahihi linapokuja suala la kuchagua aina ya gani za sound sysem ya kuweka nyumbani.
Kuna wenye kufanya hivyo kutokana na vigezo mbalimbali kama:
-budget (atanunua kutokana na uwezo wake. Kuna mwengine uwezo wake ni laki 4, while mwengine ana uwezo wa kununua MacKintosh ya milioni 30)
-brand loyalty (mfano nina ndugu yangu yeye piga ua humwambii kitu na Pioneer brand. Kuna rafiki yangu piga ua yeye ni BOSE)
-quality (hapa ndio mimi. Niko radhi nisubiri na ni-save kwa kile ninachokiona kina sound quality nzuri)
-Bass (haijalishi brand ilimradi anapata bass la kufa mtu na majirani tunakoma)
-- Bora liende: it doesn't matter
etc etc. etc.

Binafsi mimi kigezo changu ni quality sababu napenda sana kusikiliza music kwa hiyo I care much about Hi-fi kuliko home theater! Hivyo basi haina maana watu wote waniiige. Kila mtu ana uhuru na sababu zake za kununua kile akipendacho
Nikipata muda huwa nafanya research online especially www.cnet.com, then naenda stores kama Best Buy ambapo naingia department ya electronics na ku-test vile ambavyo naona vimepewa quality ratings nzuri. Nikiridhika naagiza Amazon.com
Mfano: Kuna speakers zinaitwa DEFINITIVE TECHNOLOGY nimeona zina ratings nzuri sana kwenye upande wa sound quality (Hi-fi) music oriented na si home theater
Kuzipata Tanzania ni ngumu lakini ukishuka Nairobi ama S. Africa zinapatikana ama kama una uwezo unaweza kuagiza via Amazon.com
 
Kuna mnyama anaitwa Technics alikuwepo home miaka ya 2000 huko, ni hatari kwa Hi-Fi. umeme wa dowans na richmond ulituulia mnyama wetu mpaka leo sijawahi ona madukani bongo. Yaani kila mziki unaona mzuri tu hadi bolingo dadek.
 
Karibu sana.
Maoni yako ni muhimu.
Tupo hapa kuelimishana and as an avid sound system enthusiat ningependa kujifunza toka kwako.
Mleta mada ameeleza vizuri sana matumizi ya hi-fi na home theaters.
Uko sahihi linapokuja suala la kuchagua aina ya gani za sound sysem ya kuweka nyumbani.
Kuna wenye kufanya hivyo kutokana na vigezo mbalimbali kama:
-budget (atanunua kutokana na uwezo wake. Kuna mwengine uwezo wake ni laki 4, while mwengine ana uwezo wa kununua MacKintosh ya milioni 30)
-brand loyalty (mfano nina ndugu yangu yeye piga ua humwambii kitu na Pioneer brand. Kuna rafiki yangu piga ua yeye ni BOSE)
-quality (hapa ndio mimi. Niko radhi nisubiri na ni-save kwa kile ninachokiona kina sound quality nzuri)
-Bass (haijalishi brand ilimradi anapata bass la kufa mtu na majirani tunakoma)
-- Bora liende: it doesn't matter
etc etc. etc.

Binafsi mimi kigezo changu ni quality sababu napenda sana kusikiliza music kwa hiyo I care much about Hi-fi kuliko home theater! Hivyo basi haina maana watu wote waniiige. Kila mtu ana uhuru na sababu zake za kununua kile akipendacho
Nikipata muda huwa nafanya research online especially www.cnet.com, then naenda stores kama Best Buy ambapo naingia department ya electronics na ku-test vile ambavyo naona vimepewa quality ratings nzuri. Nikiridhika naagiza Amazon.com
Mfano: Kuna speakers zinaitwa DEFINITIVE TECHNOLOGY nimeona zina ratings nzuri sana kwenye upande wa sound quality (Hi-fi) music oriented na si home theater
Kuzipata Tanzania ni ngumu lakini ukishuka Nairobi ama S. Africa zinapatikana ama kama una uwezo unaweza kuagiza via Amazon.com
Umeongea bonge moja ya point mkuu. Ila the most important thing hapo nimeona kwa wengi wetu budget ni kikwazo kikubwa sana aisee. Mathalani mtu umwambie achukue HiFi ya 800k au HT ya the same price lazima akuone wewe mwanga. Mwisho wa siku anaamua kuchukua zake Lige au Aborder subwoofer, ignoring the taste and sound quality of a quality entertainment unit (HT au HiFi). Mie binafsi ni mhanga wa budget ila najitahidi kujipanga nipate satisfaction.
Nilikuwa nina Home Theatre ya Samsung HT-F456 ila sikuridhika na sound qulity yake, nikauza na kufanya upgrade ya Sony BDV E3200. It has reasonable sound quality and features
 
Karibu sana.
Maoni yako ni muhimu.
Tupo hapa kuelimishana and as an avid sound system enthusiat ningependa kujifunza toka kwako.
Mleta mada ameeleza vizuri sana matumizi ya hi-fi na home theaters.
Uko sahihi linapokuja suala la kuchagua aina ya gani za sound sysem ya kuweka nyumbani.
Kuna wenye kufanya hivyo kutokana na vigezo mbalimbali kama:
-budget (atanunua kutokana na uwezo wake. Kuna mwengine uwezo wake ni laki 4, while mwengine ana uwezo wa kununua MacKintosh ya milioni 30)
-brand loyalty (mfano nina ndugu yangu yeye piga ua humwambii kitu na Pioneer brand. Kuna rafiki yangu piga ua yeye ni BOSE)
-quality (hapa ndio mimi. Niko radhi nisubiri na ni-save kwa kile ninachokiona kina sound quality nzuri)
-Bass (haijalishi brand ilimradi anapata bass la kufa mtu na majirani tunakoma)
-- Bora liende: it doesn't matter
etc etc. etc.

Binafsi mimi kigezo changu ni quality sababu napenda sana kusikiliza music kwa hiyo I care much about Hi-fi kuliko home theater! Hivyo basi haina maana watu wote waniiige. Kila mtu ana uhuru na sababu zake za kununua kile akipendacho
Nikipata muda huwa nafanya research online especially www.cnet.com, then naenda stores kama Best Buy ambapo naingia department ya electronics na ku-test vile ambavyo naona vimepewa quality ratings nzuri. Nikiridhika naagiza Amazon.com
Mfano: Kuna speakers zinaitwa DEFINITIVE TECHNOLOGY nimeona zina ratings nzuri sana kwenye upande wa sound quality (Hi-fi) music oriented na si home theater
Kuzipata Tanzania ni ngumu lakini ukishuka Nairobi ama S. Africa zinapatikana ama kama una uwezo unaweza kuagiza via Amazon.com
Asante sana wewe pamoja na wadau wengine kwakuwa chachu ya uzi huu. Sasa naona watu wanaopenda Muziki systems.

Kwakweli wengi wetu hatupati radha ya muziki halisi kama ulivonyongwa studio ni vile hatujui tu.

Ni sawa na Movies unaangalia kwenye chogo TB au flat ya mchina unahs umeona movie kila kitu kumbe kuna TV zinakupa radha ya picha halisi kama walivokusudia Hollywood.
 
Nikiwahi kusema hivi;
Ukanzisha uzi unao ona unaweza kuwagusa watu wakahitaji bidhaa iliyoelezewa basi ndiyo muda wa ku...make Money .

Ndg Dumelang next time think twice about business baada ya kutoa elimu wengi wanakuwa na hitaji la bidhaa.
Wazo zuri lakini pia changamoto ya nchi zetu hizi nikipato duni. Na sysytem za muziki ni gharama sana
 
Ulichokisema hapa ni sahihi kabisa na wewe sio mtu wa kwanza kusikia maneno haya

“...........Sound system yenye true watts of power, bass, Dolby dts kamwe haipatikani all in one box......”

Wewe utakuwa ni mtu wa 15 kuniambia maneno haya. Mtu wa kwanza kusikia toka kwake ni sound engineer mmoja from California in 2007.
As sound system enthusiast, nimejifunza vitu vingi sana over the past 7 years na bado najifunza.
Hizi system tunazoziona kariakoo ama mlimani city za kwenye boksi moja they are too simple, low budget and are for non-sound system enthusiasts like myself and yourself
Very true my friend.
 
klipsch hawa.

Hawa jamaa kuunda speaker wako vizuri sana.
klipsch ni hatari sana. ni very expensive but ukifanikiwa kupata hizo speakers particularly RP280F or RP280FA with dolby atmos , RP450C na hizo woofers atleast dual effect SW115. aiseee utafurahi sana. Na receiver Ku support Dolby Dts X kama hizo Denon Yahama hata Onkyo. Sasa usually ukiweza Kuweka from 7.2 ch hiyo ni superb. Sasa unaweza ukaamua receiver ikabaki kuwa pre amp tu. Halafu ukatafuta Amplifiers zingine kwa ajili ya ku power your 7 cones. Na nyingine ya ku power your subs( Though Klipsch sw115 ni powered.) Usually Emotiva is my best brand.
 
Back
Top Bottom