Matumizi sahihi ya Home theatre Nyumbani

Dumelang

JF-Expert Member
Aug 11, 2011
3,203
5,703
Leo ningependa tufahamu tofauti ya music system tunazofunga ndani na matakwa yetu kwa kile tunachotaka kupata nyumbani.

Najua home theatre system ni maarufu kwa wengi wetu na wengi tunapotaka kubadili music system kutoka sub woofer za kichina tunakwenda kuzinunua hizi home theatre.

Lakin ni rahsi kusikia mtu anakuja hapa tena nakutofuraia muziki au nguvu aliotarajia japo katumia pesa nyingi.

Kupata sound bora ya muziki ni gharama kulinganisha na kipato cha Watanzania wengi wakawaida, lakini kujua sound bora ni jambo jingine, nakujua music system bora ni utaalam au uwezo binafsi.

Kwa mfano kuna baadhi yetu bass ikiwa kubwa, hio tayari ni system bora kwake, wengine ikipiga makelele sana mpaka mtaa wa sita wakasikia hata kama hakuna ubora na sound yenye viwango hiyo kwakwe ni "The Best". Kujua sound ya viwango ni jambo jingine.

Nisichoshe niende kwenye kiini.

Hi fi Audio system (high fidelity) system mara nyingi huwa na speaker mbili, zikiwa zimetegenezwa maalumu kutoa muziki katika stereo signal ikifahamika kama 2.0
1584014704403.png

Mpangilio wa speaker zake upo katika range ya bass, mid and stereo

Imetengenezwa maalum kutoa "true music" muziki halisi au walau muziki sawa sawa na ulivopangiliwa studio na watengenezaji.

1453616970155.jpg


Maana yake ukiwa na hii "hi-fi system", muziki umepata mahala pake, gonga muziki kulingana na uwezo wako utapata radha, kila chombo walau kilicho ndani ya wimbo husika utakipata kadri kilivopigwa.

Ubora hutofautiana kulingana na bei

Home theatre Audio system

Hizi zinatumia speaker nyingi kiasi, kuanzia walau tano 5.1, au sana 7.1 na kuendelea

Ile 5 ina simama kumaanisha speaker ndogo tano kwa subwoofer 1 kwa ufupi 5.1

Ni teknolojia katika ulimwengu wa kidigitali katika kuleta maisha ya cinema nyumbani mwako.

Ni maalumu kwa DVD, blue ray Disc nk. Inakupa mwonjo wa sound ya movie katika ubora wake, na ndio sababu ya speaker nyingi. Zipo speaker za louder, effects nk nk

Kwanini? Kwasababu siku hizi movies zinatengenezwa na multi sound, na effects kibao, hapa kila speaker zipo kwaajili ya kukupa feel ya movies, feel at the cinema theatre. Katika kuchangia watu humu wanajua watazichambua.

Haikupi muziki halisi, (true music) ila inaweza kukupa feel halisi ya movies, kulinganisha na Hi fi system

Imetengenezwa kwaajili ya cinema nyumbani sio muziki.


USHAURI
Nunua home theatre kama unalenga DVD au matumizi ya Audiovisual

Lakini kama unataka Kuuhisi muziki na raha zake nunua high fidelity audio system.

Nimegusia, uzoefu wenu pia ni muhimu kwa system muziki wa nyumbani/ndani
---updates---​


16/09/2018 mdau amekuja inbox na kuuliza swali hili:

Nna LG home theater ina spika 4 ndefu na moja ndogo..ila nki-connect zote znaimba mbili tu. .sasa cjajua nakosea kwenye setting au ni nini

Jibu: Kwakweli hili ni swali zuri na linatoa mwanga mkubwa wa nilichoeleza hapo juu kuhusu tofauti ya Home thietre na Hi-fi music system.

Bila shaka wengi hili mmekutana nalo na pengine lipo na hujagundua kabisa hilo suala.

Rejea topic nilisema Muziki studio unatengenezwa katika mfumo wa chanel mbili tu (2.0) stereo. yani inakuwa left and right chanel. Ndio maana pia nilieleza hi-fi system huwa kwa kawaida zinakuwa na speaker 2 tu, for left chanel and right. 2.0 stereo

Home thietre inakuwa na tano, 5.1 au saba, 7.1 nakuendelea, maana yake katika movies kunakuwa na chanel nyingi, sound, effects, kicks, stunts sound hivo zinawekwa katika chanel tofauti, na ni rahisi kama unaangalia movie ukasikia effect ya ngumi ikasikika katika spika za mbele tu, wakati huo mlio.wa gari ukasikika spika za pembeni na ikapigwa risasi ikasikika katika spika nyingine lakini sio zote kwa pamoja.

Vivyo hivyo uwezi sikia muziki katika spika zote za home thietre ispokuwa mbili tu kwasababu kwa kawaida muziki unapoandaliwa studio huwa katika chanel izo mbili, hivyo hauwezi kuwa multiplied katika spika 5 au 7, na ikitokea katika settings ikakubali (japo system bora hazina hiyo setting) basi ndio ubora wake ushakuwa affected, lazima kuna distortion katika baadhi ya spika na zile mbili Main ubora utashuka.

Unaweza pia kama ni computer inasukuma ukaweka mixer kwaajili ya speaker fill, ukajaza zote tano au saba za home thietre yako.

Na rahisisha kwakusema hujakosea kuseti home thietre yako ila unapopiga muziki wa chanel mbili 2.0 stereo, lazima nyingine zikae kimya maana hazina feed, lakini chukua movie ya holywood saizi uweke hapo zitapiga spika zote.

KARIBUNI
 
Mkuu umesahau kuongelea ukubwa wa chumba ama eneo litalotumika kwa huo mziki wako, indoor quality ni tofauti na outdoor quality. Chumba za 3x3 mziki wake lazima uwe tofauti na penthouse suite.
Ni kweli mpangilio wa muziki system ndani ni muhimu hasa kulingana na ukaaji wa chumba, udogo/ukubwa

Sound inaweza toa muziki mbaya kwasababu tu umeipangilia vibaya, au ni kubwa sana kuliko chumba/sebure husika nk

Nitarudi na ufafanuzi zaidi wa hili na kanuni za kupangilia sound system ndani.
 
Vp elimu ya mpangilio wa music system ndani?? Tunaisubiri pia mkuu..

Pia wengi wanasema hii home theater ni soround na ukiipangilia vizuri speakers unapata music mzuri..

Tupe ufafanuzi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom