Matumizi sahihi ya Home theatre Nyumbani

Nna Sony theatre zaidi ya miaka 7 siajawahi jutia pesa yangu ukiipangalia vizuri mziki unachujwa hasa upate ulitengenezwa vizuri au movie ila sio bongo movie
 
IMG_2861.JPG
je hii inafaa kuitwa Hi- fi ?
 
Habari wakuu hii home theater ni JVC model no. RX-E5S toleo lamwaka 2004 ni old model kwaiyo haina option ya Bluetooth,usb port wala HDMI port je kuna mbinu zakufanya iwe na hizo option mana kwaupande wa sound ipo vzr inasuuza roho kwakweli huwez kufananisha nahizi zakichina..
IMG-20180917-WA0001.jpeg
IMG-20180917-WA0006.jpeg
IMG-20180917-WA0007.jpeg
IMG-20180917-WA0005.jpeg
 
Sound system yenye true watts of power, bass, mid dolby atmos haipatikani in all in one box. View attachment 869404View attachment 869405

Ulichokisema hapa ni sahihi kabisa na wewe sio mtu wa kwanza kusikia maneno haya

“...........Sound system yenye true watts of power, bass, Dolby dts kamwe haipatikani all in one box......”

Wewe utakuwa ni mtu wa 15 kuniambia maneno haya. Mtu wa kwanza kusikia toka kwake ni sound engineer mmoja from California in 2007.
As sound system enthusiast, nimejifunza vitu vingi sana over the past 7 years na bado najifunza.
Hizi system tunazoziona kariakoo ama mlimani city za kwenye boksi moja they are too simple, low budget and are for non-sound system enthusiasts like myself and yourself
 
Nimeufuatilia huu uzi tangu mwanzo hadi post ya mwisho. Kuna vitu nimejifunza na pia nimepata kuona hulka za watu juu ya viti vyao, wapo wakurupukaji na tupo tunaojifunza.
Suala la kuchagua aina gani ya music uweke nyumbani kwako inategemeana na ushabiki wako binafsi. Mathalani mie binafsi ni mpenzi wa action na horror movies. Kwa mantiki hiyo ndio maana napenda sana home theatre kwa ajili ya kuaccomodate sound effects za movies. Ila pia ndani ya home theatre kuna options za sauti kama wataka music sound, speech, live , orchestra etc. So hapo kama wasikiliza muziki wako, unao uwezo wa kuadjust speaker ikatoa kama HiFi ukawa na 2.0 active channels ambazo ni FL & FR, (Centre na surround speakers zinakuwa turned off kwa muda huo)
Nimeona zimetajwa brand nyingi za kutisha, ila tungejadiliana kulingana na market supply yetu ingekaa poa sana. Kwa hapa TZ tunapata sana bidhaa za Asia specifically za Korea (Samsung na LG), za Japan (Sony, Panasonic kwa uchache sana, Hitachi kwa uchache pia N.K), za China ndio usiseme kwa kuwa ni more than affordable ila hatuna za Europe wala America unless uagize au utoke nayo huko.
Tunapoangalia ubora kwa hizo basi ndio maana Sony amekuwa named the best kwa kuwa wengi hatujui beyond sony.
Practically Samsung na LG upande wa Audio systems hawamgusi Sony na ndio maana wengi wamefanya Sony kama ndio benchmark.

........nitarudi...........
 
Hivi hometheatre haiwezi kuwa Hi-fi. maana hi-fi ni kipimo cha ubora wa spika kam HD kwenye picha. Hauwezi kuwa na Home theatre yenye high fidelity speakers?
 
Back
Top Bottom