PakaJimmy
JF-Expert Member
- Apr 29, 2009
- 16,203
- 8,724
Jana usiku CCM wamezindua kampeni ya kuchangia kampeni kwa kutumia simu za mkononi!
Makadirio ni kwamba watakusanya taslimu 40,000,000,000/=(bilioni 40)!
Mimi nilipotazama jinsi washiriki wale walivyochangamka kutoa kwa kutuma ujumbe, nilihamasika kwamba iwapo ungeanzishwa uchangiaji wa namna hiyo kwaajili ya madawati ya shule zote nchini, hakuna mtoto ambae angekaa kwenye vumbi!
Kama jana, ziliweza kupatikana milioni 20 ndani ya dakika 5 tu za uchangiaji, je kwa miaka 5 ya uongozi wa JK, wananchi wangechanga kiasi gani, na tungekuwa wapi?
Kwanini wabongo tunapenda kufanya fund-raising za 'Disposable cash, kama hizi kampeni, tisheti na harusi, unlike kuwekeza kwenye investment za kudumu kama elimu, afya na miundombinu?
Ningekuwa mimi ndo JK, ningesubiri hela yote hiyo ichangwe, kisha natangaza ghafla kwamba hakutakuwa na kampeni, hela zote zinatumika kupeleka maji, au kujenga dispensari vijijini!
NINA HAKIKA 100% KWAMBA CHAMA CHANGU KINGECHAGULIWA BILA KUPINGWA NA RAIA YEYOTE...Unaonaje?