Matumizi holela ya vidonge vya uzazi wa mpango vyaongeza Saratani ya matiti kwa mabinti

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,501
9,280
Ongezeko la saratani kwa wasichana latisha

TAASISI ya Saratani Ocean Road (ORCI), imebainisha kuwapo ongezeko la saratani ya matiti kwa wasichana nchini, kunakochagizwa na matumizi holela ya vidonge vya uzazi wa mpango.

Imesema wasichana wenye umri kuanzia miaka 25 ndio kundi lililothibitika kuwa katika hatari hiyo, kutokana na kutumia vidonge hivyo kinyume cha taratibu.

Hayo yalielezwa jana na Daktari Bingwa wa Utafiti wa Saratani wa ORCI, Samuel Kandali, wakati akizungumza na Nipashe kuhusu mwezi wa uelimishaji wa jamii kuhusu saratani ya matiti.

Alisema kuanzia mwaka jana idadi ya wagonjwa wanaopata saratani ni kuanzia miaka 25 hadi 54, tofauti na miaka ya 2008/9, ambapo walikuwa wakipokea wagonjwa wa kuanzia miaka 64.

“Hatujafanya utafiti kuhusu sababu za wasichana wadogo kupata saratani hii, isipokuwa sababu kuu ni matumizi ya vichocheo vya homoni za mwili aina ya dawa za uzazi mpango kwa wasichana wadogo,” alisema Dk. Kandali.

Alieleza zaidi kuwa, suala hilo limebainishwa wazi na wanafunzi wa Chuo cha Ufundi cha Ufundi Stadi (VETA) Kipawa, ambao walikiri wazi kutumia vidonge hivyo bila kufuata ushauri wa daktari.

“Wanafunzi wamekiri wazi wanatumia vichocheo vya mwili, bila mpangilio wakati mwingine kutumia dawa (alizitaja kwa jina) mara nne kwa mwezi hali ambayo ni hatari kwa afya zao na tunaweza sema kuwa ni moja ya sababu za kupata saratani hii,” alisema Dk. Kandali.

Aliwataka wasichana wadogo kuepuka matumizi ya vidonge vya uzazi wa mpango, bila kufuata ushauri wa daktari, ili kujinusuru na tatizo hilo.

Daktari huyo bingwa, pia alizitaka taasisi mbalimbali nchini kushirikiana kufanya tafiti kufahamu zaidi sababu za kuibuka kwa wimbi hilo la mabinti wadogo kupata saratani.

Kuhusu mwezi Oktoba wa kuhamasisha jamii kuhusu uelewa wa saratani, alisema jana walitoa mafunzo na kuwafanyia uchunguzi wa awamu, walimu na wanafunzi wa VETA Kipawa.

Alisema walifikia wanafunzi 300, walimu 30 na kufanya uchunguzi wa watu 25, ambao wote hawakubainika kuwa na tatizo hilo.

Dk. Kandali alisema waliwaeleza wanafunzi hao kuhusu visababishi vya saratani kuwa ni uvutaji tumbaku, unene uliokithiri na kutofanya mazoezi na kuwataka kubadili mfumo wa maisha kwa kuchangamsha mwili kwa mazoezi angalau nusu saa kila siku.

“Tunaendelea kutoa elimu kwa jamii kupitia vyombo vya habari kuyafikia makundi mbalimbali lengo ni kujenga uelewa kwa jamii hasa kuondokana na dhana potofu kuhusu ugonjwa huu,” alisema Dk. Kandali.

Naye Kaimu Meneja Rasilimali Watu wa VETA Kipawa, Upendo Abraham, aliishukuru ORCI kwa kuwapa elimu hiyo, ambayo itawasaidia vijana kutambua visababishi, ili kuzuia kupata ugonjwa huo.

Alisema wanafunzi 124 na wafanyakazi 24 walikuwa tayari kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi wa awali, ili kugundua kama tayari kama wana ugonjwa huo waanze matibabu.
 
Tatizo ni matumizi ya hivyo vidonge, sio kusingizia matumizi mabaya. Njia za asili zinawekea kauzibe ya kudanga, sasa wanajiua mapema!
 
Kwamba hajafanya tafit lakini ana hypotheses vitu ambavyo anadhani ni visababishi. .

Chanz cha kabsa mpaka sasa hakijathibitishwa across any age..
 
Mzungu hana mpango mzuri na mtu mweusi.

Kibaya zaidi anamtumia mweusi kumwangamiza mweusi mwenzake.

Hii midawa ndo tatizo na hii ilishasemwa miaka mingi, hawa watatumaliza ili bdae wajukuu zao wahamie huku.
 
Kwamba hajafanya tafit lakini ana hypotheses vitu ambavyo anadhani ni visababishi. .

Chanz cha kabsa mpaka sasa hakijathibitishwa across any age..
Chanzo Ni Dawa Wala Sio Kuzidisha Just Wana Ficha Ficha Tuu.
 
Back
Top Bottom