Utafiti: Aspirini huenda ikasaidia kutibu saratani sugu ya matiti

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,329
33,138
woman taking aspirin

Aspirini huenda inaweza kusaidia kupambana na saratani sugu ya matiti kwa kufanya uvimbe mgumu kutibika kuitikia tiba ya dawa za kupambana na saratani, madaktari wanasema.

Kundi la wataalamu wa Wakfu wa Christie NHS Trust, mjini Manchester, limeanza kufanyia majaribio wagonjwa wa saratani ya matiti.

Wanashuku kichocheo cha asprini kinachozuia.

Uchunguzi uliofanyiwa wanyama tayari umeonesha matokeo ya kuridhisha.

Wanawake wa makamo
Kuna ushahidi unadai kuwa aspirini inaweza kusaidia kuzuia saratani zingine na kupunguza hatari ya kuenea.

Lakini ni mapema sana kuwapendekezea watu kuanza kutumia tiba hii. Utafiti zaidi unahitaji kufanywa.

Karibu wanawake 8,000 nchini Uingereza hupatikana na saratani ya matiti kila mwaka - ambayo ni nadara sana lakini ni aina ya saratani ambayo sasa sana huwaathiri wanawake wa umri wa makamo na wanawake weusi.

Uvimbi huo hauna vipokezi zinazopatikana katika saratani zingine za matiti , kumaanisha tiba kama ya herceptin haitafanya kazi ingawa dawa zingine na matibabu zinaweza kusaidia.

'Uchungu sana'
Katika majaribio yaliyofadhiliwa na mpango wa utafiti unaoendeshwa na shirika la Breast Cancer Now- linalowasaidia wagonjwa wa saratani ya matiti, baadhi ya wagonjwa watapewa dawa ya asprini pamoja na dawa zingine za kukabiliana na saratani kabla wafanyiwe upasuaji na tiba ya mionzi maarufu chemotherapy.

Majaribio hayo yakifanikiwa kutafanywa majaribio mengine zaidi ya kimatibabu ya asprini kutibu saratani ya matiti hasa wakati ikibainika seli zasaratani zimeanzia kwenye matiti na kuenea katika maeneo mengine ya mwili.

Beth

Maelezo ya picha,
Beth alitibiwa na chemotherapy, ikifuatiwa na mastectomy na radiotherapy

Beth Bramall, 44, kutoka Hampshire alipatikana na saratani hasi ya matiti mwaka 2019.

Alisema: "Hakuna saratani nzuri lakini saratani hasi ni uchungu sana, hasa ikizingatiwa mpango wake wa tiba ya muda mrefu ambao unaashiria udhaifu wake.

"Iliniangusha, kutokana na athari za kupoteza nywele, kichefuchefu, pamoja na kuumwa na misuli, kuharisha kuvimbiwa, kuumwa na kichwa kupita kiasi, kutokwa na jasho nyakati za usiku na kujihisi kuchoka hali ambayo sijawahi kuwa nayo awali.

"Nimebarikiwa kuwa nimepata jibu kamili la kiafya kwa matibabu.

"Lakini kilikuwa kipindi kigumu cha miezi 18kwangi mimi na familia yangu.

"Natarajiwa kuendelea na matibabu kwa miaka miwili na kufanyiwa skani ya kichwa ."

Chanzo: BBC
 
Aspirin is a very old drug 😂😂, hizi partial research. the truth will be out.we wait
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom