Matukio ya ukatili wa kijinsia nchini yaongezeka hususan kwa wanawake na watoto

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
3,115
2,000
Kamati ya Bunge la Tanzania ya Huduma na Maendeleo ya Jamii imesema kumekuwa na ongezeko la matukio ya ukatili wa kijinsia nchini hususan kwa wanawake na watoto kutoka watu 31,996 mwaka 2016 hadi 43,487 mwaka 2018.

Akiwasilisha taarifa ya Kamati hiyo Mwenyekiti wa kamati hiyo, Peter Serukamba amesema bungeni leo Alhamis Februari 6 2020 amesema kuwa ongezeko la asilimia 35.9.

“Madhara yanayotokana na ukatili huo ni makubwa ikiwemo kuumizwa vibaya, kupata ulemavu wa viungo, madhara ya kisaikolojia na hata kupoteza maisha kwa baadhi ya watu,”amesema Serukamba.

Amesema kutokana na hilo, Kamati hiyo inashauri Serikali kuweka utaratibu wa kuzishauri halmashauri kutenga fedha kwa ajili ya utekelezaji wa uhamasishaji wa namna bora ya kupunguza ukatili huo na hata kujikinga na kutoa taarifa katika vyombo husika ikiwemo polisi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom