Matukio ya uchaguzi wa Marekani!! Weka tukio lako hapa!

mr mkiki

JF-Expert Member
Sep 22, 2016
5,584
11,659
Birmingham Albama, Msimamizi Mkuu kawazuia wakala wa upinzani kuingia Kwenye vituo vya kupiga kura..,Wakala wa Republican amegundua uwepo wa wapiga kura feki kutokea Kawe ambao wameshawasili mara tu gwajiboy alipishinda ubunge.

Wakala wa Republican hapa Kansas amegundua kuna kituo kina majina ya Wameksiko tupu...ndio ameoandishiana na bosi wa Uhamiaji hapa kituoni...ila Mkuu wa Sherrif amemuweka ndani.
Wamemuonya akileta fujo wanamfungulia kesi ya Ugaidi.

Msimamizi wa uchaguzi jimbo la Maryland amewaambia wananchi hakuna kulinda kura, wakishapiga kura warudi nyumbani

Mkurugenzi wa tume ta uchaguzi marekani amesema wamarekan wanahitaji maji, barabara na umeme..hivyo wagombea waeleze sere na sio matusi.

Kamanda wa Kanda Maalum Michigan amesema "Tuhuma za Kura fake ni mambo ya mitaani tu watu waendelee kupiga kura"
Zoezi linaendelea bila MAWAKALA.

Weka matukio yako hapa.
 
Kuna mshindani wa Trump&Biden anayetokea chama kidogo kiitwacho Orange Party yeye jana alitangaza kuendelea na kinyang'anyiro hicho huku akisema anaamini atashinda uchaguzi huo kwa kishindo,yaani kama vile mchezaji wa mpira anavyofunga bao kwny dakika ya 89.
 
Back
Top Bottom